Kwanini Tanzania bado tupo gizani kwa Sheria kandamizi za viongozi wa juu wa serikali kuwa na kinga ya kutoshtakiwa

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,615
3,909
Tanzania ni taifa ambalo tumekuwa gizani sana kuhusiana na sheria zetu/ katiba yetu inayolinda viongozi wa juu wa umma kutoshitakiwa pindi wanapofanya jinai katika utumishi wa umma, hii inawafanya kupuuza wananchi waliowachagua kutekeleza ya kwao katika utumishi wao na siyo ya wananchi

Tumeona awamu zote zinapita kwa kashifa mbalimbali ya mikataba tata yanasemwa tu lakini hakuna maamuzi na hata umma ukisikia fedha zimeibwa walio wengi nikupongezana na kuambiana kwamba chukua chako mapema maisha ni hayahaya, ifike tuseme kwamba zama zimebadilika hakuna aliyejuu ya sheria binadamu wote ni sawa viongozi hao siyo mungu kiasi kwamba wanafanya mema katika nchi,

Ombi langu kuna kila sababu ya kufuta sheria hizo ili viongozi waliopo madarakani wajue wanachotakiwa kukifanya katika utumishi wao , waliowengi tumeona wamelitia hasara taifa hili kwa mambo mbalimbali yabayohusu mikataba mbalimbali, jambo hakuna sababu yakulifumbia macho mbele ya jamii ya watu milion 61.3 sheria ifutwe haraka haina afya katika taifa hili , wanasiasa walio wengi badala ya kutumikia wananchi wengi wamebaki kupongezana kwa manufaa yao wenyewe huku waliowengi wakiumia

Ni wakati wa kuamka tuache kulala nchi hii hakuna aliyejuu ya sheria kilasiku wanafanya mabadiliko ya sheria mbalimbali lakini oneni wenyewe hilo eneo hawaligusi kabisa kwani wanajuwa ni mwiba kwao, nimeshuhudia mabadiliko ya sheria mbalimbali zenge mapungufu lakini eneo hilo limefumbiwa macho ni wakati sasa swala hili kulipigia kelele kabla nchi yetu haijakongoroka na mapapa hawa wa wezi wa mali za umma.
 
haya mateso ni mhimu tunayatoe maana inawezekana ! sheria hii irekebishwe haraka
 
Hii inatokana na dhamira mbaya inayokusudiwa kufanywa na viongozi na pengine sio hao wajuu sana hata hawa watendaji wajuu wa taasisi wengi hawajui Sheria lakini kila wakati ni kuandama watumishi na wananchi wanao waongoza.
Muheshimiwa Raisi ile tume ya utumishi kuna wakati inaamua kesi za kipuuzi sana ambazo wateule wa Raisi au waziri wamefanya kwa kuogopa wanao waongoza.
 
haya mateso ni mhimu tunayatoe maana inawezekana ! sheria hii irekebishwe haraka

Mkuu uko sahihi sana kwenye bandiko lako namba moja. Mifumo yote ya nchi iko dhaifu kutokana na baadhi ya viongozi kuwa na kinga ya kutoshtakiwa hasa rais. Lakini sitegemei hali hiyo kubadilika kwa hii katiba ya maridhiano. Ingekuwa katiba baada ya machafuko huenda kila mtu angeweza kuwa chini ya sheria.
 
Hii sheria watakuwa wamekopi kutoka kwa mabeberu uingereza bila kujali kwamba sheria hiyo kwa nchi kama Uingereza inamhusu malkia au mfalme. Sasa kuwawekea viongozi watendaji kinga ya kutoshtakiwa ni jambo la ajabu ambalo huenda linapatikana kwenye hii nchi ya wadanganyika pekee.

Chukulia nchi kama Marekani, rais anaweza kuwa convicted mahakamani na kushtakiwa, kule China kwao sheria haina macho, hata rais anaweza kupigwa kitanzi kama walivyo raia wengine. Vinginevyo wajipe vyeo vya kifalme au kimalkia ili tujue wana hadhi hiyo ya kutoshtakiwa, kinyume na hapo ni ufisadi wa mamlaka.​
 
Back
Top Bottom