Kwanini TANESCO isivunjwe?

Ikivunjwa ndio umeme hautakatika ? Tuache ujingaa......tukomae serikali iwe setious kuwekeza miundo mbinj kisasa tuweze kufikia .....sehemu umeme ukatile only sababu maintenance sio kuvunjaa tuache siasaa
Ukilivunja utapata makampuni ya mabwawa ya maji tu (vyanzo vya umeme), wasambazaji tu (nguzo na nyaya - miundombinu) na wanaonunua umeme na kuuza tu (luku tu). Kila mtu atafanya kazi yake inayomlipa kuliko hivi sasa wafanyakazi wa tanesco hata kama hakuna umeme wanalipwa vilevile. Serikali ijiondoe kwenye biashara ya umeme kama vile ilivyouza na kutaifisha mashamba makubwa ya umma, nyumba za umma na mashirika na viwanda vya umma.
 
Kila nchi kuna wapumbavu wake. Kule magharibi na marekani kuna mfumoko mkubwa wa bei za vitu kwasababu ya upumbavu wao, kuna homeless wengi kuliko huku. Huku tz kuna ujinga mkubwa kama huu wa umeme unaokatika bila wahusika kujali maisha ya majumbani, maofisini, mitaani nyakati za usiku, viwandani na kwenye biashara na huduma zinazotegemea uwepo wa umeme. Kukatika kwa uwewe kuna watu wengi sana wanapoteza maisha au kuahirishiwa matibabu, kuna viwanda vinafungwa na wafanyakazi kukaa bure au kuondoka kwenda nyumbani, kuna mitaji ya wauza juice, mabarafu, samaki na hata vipindi vyuoni kuahirishwa. Ni upuuzi tu kaka lakini dawa yake sio kuikimbia nchi bali kuliondoa tatizo kwa mikono, sauti, maandishi yetu na akili zetu. Kuwaondoa wasiofanya vizuri na kuwaweka watu wanaokerwa na hali ya mambo inapokwenda vibaya. Fikiria watu wanapumbazwa na vitu vidogo kama kununua magoli na kusahau shida ya umeme. Utafurahi vipi kushangilia goli uwanjani wakti ukirudi mtaani na nyumbani kwako kuna giza totoro.
Poleni sana.

Labda kuna siku mtaamka.

Maana niliona wakina mama wanajifungulia chini ila waziri wa afya anao machawa mtandao wa X kwa ajili ya kujibu mashambulizi ikiwemo kubuni picha za uongo na kukanusha hali haiko hivyo.
 
Mipango yetu sisi haingalii vipaumbele bali siasa na upigaji. Ukiniuliza mimi nini iwe ndo vipaumbele vyangu nchini kuanzia umuhimu wake ningeanzia na 1. kuimarisha kilimo, uvuvi na ufugaji kwa sana, 2. baada ya hapo ningehamia kwenye madini na mali asili zetu, 3. Ningeimarisha sekta ya bandari na uchukuzi 4. Umeme mwingi, maji na viwanda 5, Kwenye elimu na afya saaana.
 
Ukilivunja utapata makampuni ya mabwawa ya maji tu (vyanzo vya umeme), wasambazaji tu (nguzo na nyaya - miundombinu) na wanaonunua umeme na kuuza tu (luku tu). Kila mtu atafanya kazi yake inayomlipa kuliko hivi sasa wafanyakazi wa tanesco hata kama hakuna umeme wanalipwa vilevile. Serikali ijiondoe kwenye biashara ya umeme kama vile ilivyouza na kutaifisha mashamba makubwa ya umma, nyumba za umma na mashirika na viwanda vya umma.
Nadhariaaas tuuu.....ile huduma kutoka serikalk kwa wananchi wakitaks wafanye pure business .....wabinafshishe ......tutashindwa kununua umeme...hasa vijijini.....walio ajira rasmi na wafanya biashara wakubwa tuuu wataweza....
 
Miaka mingi toka nchi yetu imepata Uhuru, lakini mpaka leo ina kero nyingi mno. Nafikiri viongozi kuna sehemu kubwa tu wanashidwa kufanya vitu kwa ajili ya waliowadhamini
 
Hakuna umeme hata dar es salaam, viwanda, majumbani na kwenye biashara hakuna umeme, ni shida na hasara ya matrilion inapatikana: Mvua zinanyesha nchi nzima, mabwawa yamejaa na mafuriko kila kona ya nchi. Kwanini umeme hakuna?

Kipindi cha ukame mnasingizia mabwawa yamekauka na mabwawa yakijaa unasingizia miundombinu mibovu na hakuna anaeonekana kusikitishwa kwaajili ya nchi kukosa umeme. Kwa kipindi kirefu tunaambiwa kuwa maji yaliyoingia bwawa la nyerere yanamudu kuwasha mashine ya kufua umeme, baada ya hapo mvua zikaendelea kujaza mito na mabwawa hadi mafuriko kutokea, lakini unamsikia kiongozi anasema labda mwezi February 2024 ndio mashine ya kwanza inaweza kuwashwa ili kufua umeme, maneno na kauli ambayo haionyeshi kuwa kuna udharura wa upatikanaji wa umeme nchini. yaani hakuna userious wowote kwenye kauli wala muonekano wa msemaji, hovyo.

Shida ni nini, muundo wa tanesco, wafanyakazi wa tanesco, viongozi wa tanesco, wizara ya nishati au serikali nzima?
Ule utaratibu wa kuweka watu kwenye viroba na kupotezwa unatakiwa uendelee,hii nchi utani ni mwingi sana.
Kuna baadhi ya watu ni lazima wapelekwe mbinguni Ili nchi itulie.

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Nchi imeangukia kwa wafanyabiashara wa mafuta, solar, gas na magenereta pamoja na vipuri vyake, usitegemee mabadiliko ndani ya serikali ya CCM, wako wamiliki wa mabasi huko huko CCM ndo mana mpaka nauli zinapanda.
Kataa CCM na upinzani kwa maendeleo ya nchi,. Vijana wa 90's tunahitaji kuunda chama pinzani Cha ukweli sio njaa.
Kwaiyo tubadilishe uingozi
 
Na bado jitu linasimama na kusema anaupiga mwingi.

Hawa watu wanaovaa mashati makubwa na yule wa tai ya bendera ya taifa ni useless kabisa
 
Mipango yetu sisi haingalii vipaumbele bali siasa na upigaji. Ukiniuliza mimi nini iwe ndo vipaumbele vyangu nchini kuanzia umuhimu wake ningeanzia na 1. kuimarisha kilimo, uvuvi na ufugaji kwa sana, 2. baada ya hapo ningehamia kwenye madini na mali asili zetu, 3. Ningeimarisha sekta ya bandari na uchukuzi 4. Umeme mwingi, maji na viwanda 5, Kwenye elimu na afya saaana.
Nadhani unapata halisi ya hichi kituko kinachoitwa chipukizi.

Ni dalili tosha hakuna uongozi wenye maono nilitarajia watu wafanyiwe grooming tofauti ila naona familia zinaandaa mazingira ya kulinda ulaji walioupata kwa dezo .

Vitu viwili tu ndio vitaiinua Tanzania tena , katiba mpya itakayotambua na tume huru na chama kingine cha siasa .

Hauwezi kunishawishi kwamba miaka 62 watu ni wale wale then yawepo mabadiliko never!

Tutaendelea kuona familia chache zikipishana kwenye corridors of power halafu watu wakibakia kuitwa wanyonge na huduma za msingi hawana.

Nilikuwepo huko mwezi November kuna vitu vilinisikitisha sana mpaka unashangaa na kujiuliza hii nchi ina uongozi kweli au ni state capture?
 
Kwani yule naibu waziri mkuu kashindwa kuziondoa changamoto za umeme?

Si.mlisema Makamba hawezi aondoke ili aingia mtu mahiri (sukuma gang ) mwenzenu mambo yatakuwa sawa?

Haya Sasa mvua zinanyesha mpk milima inaporomoka lkn umeme ni wa mgawo. Na sukuma gang Biteko yupo tu katiba macho.

Never and never again kwa sukuma gang.
Swala la Umeme ni Aibu nzima ya Serikali na CCM,

Mgao wa umeme/kukatika katika umeme sio swala la Awamu hii wa la swala la Sukuma Gang, Usitegemee Gun shot solutions/overnight process Kwa swala la Umeme,
Tumeshindwa kama nchi kuwa na vipaumbele/Scale of preference over limited resources,Poor planning/projections na ushauri mbovu au kutofanya kazi Kwa watendaji wa Tanseco.
Kama nchi tujifunje kukamilisha jambo 1 effectively,Toka awamu ya Mkapa/JK/JPM/SSH umeme no shida,Ukame haujatifunza chochote, mwisho hongera Kwa JPM huko aliko Kwa audacity yake ya Bwawa la Umeme,

Tuna shida ya vipaumbele vyingi Kwa wakati mmoja matokeo hatuja yaona tunaamka na mengineyo.

I declare interest not Sukuma Gang or die hard fans of late JPM.
 
Nchi imeangukia kwa wafanyabiashara wa mafuta, solar, gas na magenereta pamoja na vipuri vyake, usitegemee mabadiliko ndani ya serikali ya CCM, wako wamiliki wa mabasi huko huko CCM ndo mana mpaka nauli zinapanda.
Kataa CCM na upinzani kwa maendeleo ya nchi,. Vijana wa 90's tunahitaji kuunda chama pinzani Cha ukweli sio njaa.
Vijana wa miaka ya 90 Hawa wanaolegeza suruali chini ya makalio?
 
Ikivunjwa ndio umeme hautakatika ? Tuache ujingaa......tukomae serikali iwe setious kuwekeza miundo mbinj kisasa tuweze kufikia .....sehemu umeme ukatile only sababu maintenance sio kuvunjaa tuache siasaa
Serekali inayoweza kuingia madarakani kwa kupora uchaguzi haiwezi kuwa serous. Serekali zinazokuwa serious ni zile zinazojua kubaki madarakani ni kutokana na uwajibikaji. Kama wanaweza kuingia madarakani kwa mbeleko ya vyombo vya Dola, usitegemee uwajibikaji wowote serious hapo.
 
Niliagiza samaki kutoka mwanza wote wameharibika, ni upuuzi mtupu, maana kuwasha generator usiku kucha kupoza samaki na juice kwenye majokofu ni ghali sana.
1.Kwa nini usingewakaanga?
2. Kwa nini msingewala kwa mfululizo waishe haraka?
 
Hili Shirika lina ujinga mwingi sana. As such it is a Non performing Organization...
 
Watu hao wa dili ndo vinara wa kusema ".... anaupiga mwingi" wote walio kwenye hizo system kwenye profile zao pictures za social medias mara nyingi wamemuweka bimdashi.
 
Hakuna umeme hata dar es salaam, viwanda, majumbani na kwenye biashara hakuna umeme, ni shida na hasara ya matrilion inapatikana: Mvua zinanyesha nchi nzima, mabwawa yamejaa na mafuriko kila kona ya nchi. Kwanini umeme hakuna?

Kipindi cha ukame mnasingizia mabwawa yamekauka na mabwawa yakijaa unasingizia miundombinu mibovu na hakuna anaeonekana kusikitishwa kwaajili ya nchi kukosa umeme. Kwa kipindi kirefu tunaambiwa kuwa maji yaliyoingia bwawa la nyerere yanamudu kuwasha mashine ya kufua umeme, baada ya hapo mvua zikaendelea kujaza mito na mabwawa hadi mafuriko kutokea, lakini unamsikia kiongozi anasema labda mwezi February 2024 ndio mashine ya kwanza inaweza kuwashwa ili kufua umeme, maneno na kauli ambayo haionyeshi kuwa kuna udharura wa upatikanaji wa umeme nchini. yaani hakuna userious wowote kwenye kauli wala muonekano wa msemaji, hovyo.

Shida ni nini, muundo wa tanesco, wafanyakazi wa tanesco, viongozi wa tanesco, wizara ya nishati au serikali nzima?
Kwa nini ivunjwe, wakati wahujumu wenyewe ndio hao hao watakao inunua tiniseco
 
Back
Top Bottom