Tareman
Member
- Jun 3, 2019
- 53
- 33
Habari zenu wana JamiiForums?
Leo nimekuja na hili suala ambalo nimejaribu kulitafutia uvumbuzi ila sijafanikiwa.
Jumamosi ya tarehe 13/05/2023, nikiwa ndani ya uwanja wa JK T2 jijini Dar es Salaam nilishuhudia mambo ambayo sikutegemea kama yanaweza kutokea hususani kwenye maeneo kama yale yenye ugeni wa kila aina.
Kuna walinzi wenye kuvaa nguo za kiraia kazi yao ni kufunga tairi za gari kwa chuma lenye mnyororo hasa kwa magari yote madogo yanayo park mule ndani kwa madai ni gari zenye kujihusisha na biashara ya Uber na Bolt.
Kwa kweli nilitamani sana kusikia ni nini hasa lengo lao juu ya kile wanachokifanya dhidi ya hizo biashara ya tax mtandao, niliamua kumfuata mmoja wa wale wafungaji wa magari nilijaribu kumhoji ni kwanini wanafunga ila hakuwa na jibu alisema yeye kapewa tu kazi ya kuzifunga gari ndogo zote zitakazo park ndani ya uwanja kwa muda wa dk10 hadi 15.
Ghafla kulizuka mabishano ya wamiliki wa hizo gari zilizofungwa na kupelekea kuitwa kwa Meneja Finance ila hakuwa na muda wa kuja hivyo alikuja msaidizi wake.
Nikaamua kumfuata na yeye ili kumhoji juu ya hicho kilichotokea ila majibu yake hayakuniingia akilini maana alisema wameamua kukataza Tax mtandao kwa sababu za usalama wa wateja wao, akaniambia dereva uber na Bolt wanaruhusiwa kushusha tu abiria na sio kukaa humu ndani.
Pia nikamuuliza na kama kuna abiria wake anayetakiwa kumpokea na bado hajafika nalo limekaaje: akaniambia masuala ya kubeba abiria anatakiwa wasubiriane huko huko nje ya uwanja na sio humu.
Kwa majibu yake nilishangaa ila nilipata kufahamu kuwa Tax za uwanja wa ndege wamiliki wake ni viongozi wa mule ndani kutokana na majibu yake.
Kwenu wana JF kama kuna mwenye ufafanuzi zaidi katika hili naomba nayeye anitoe kibanzi nilicho nacho maana bado nawaza kila mmoja kwenye sekta yake akijiamulia kuweka sheria zake ni nani atakayekuwa salama?