Kwanini standup Comedian wakiume Bongo wanapenda kuigiza mambo yakike ?

vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
3,959
2,000
Mimi nimfuatiliji mzuri wa stand up comedian wa hapa Tanzania ambapo kwasasa naona Dar na Arusha zinafanya vizuri (hongera) ila cha kushangaza ni kuwa asilimia kubwa ya standup comedian wa Dar wanapenda kuigiza mambo ya kike, yaani ongea ya kike, mapozi ya kike na wakati mwingine mavazi ya kike, je inamaana mambo yakike ndio yanachekesha sana huko Bongo Dar es Salaam au ndio Kale katabia pendwa ka kina wanaume wa Dar es Salaam ?

Nawasilisha

.
1147333
 

Baba Swalehe

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
17,072
2,000
Mambo ya wanawake ni ya kuchekesha sana

Ingawa hawatakiwi kufanya hivyo

Ni ulimbukeni tu !

Kama wajinga wanaume wanaoandika maneno kama

Tyu , enx , xaxa , my na mengineyo !
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
56,242
2,000
Habari nzima ya stand up comedy imetokea Marekani.

Ukiangalia Marekani, stand up comedians wakubwa wote wameiga ku act kike.

Kitendo cha kua act ni kuchukua role iliyo tofauti nawe, na kuiweza vizuri. Hivyo actor anaweza ku act kama daktari, wakati yeye si daktari, au ku act kama askari wakati yeye si askari etc.

Ukiangalia stand up comedians wa Marekani kuanzia kina Richard Pryor mpaka Martin Lawrence, Steve Martin mpaka na Chris Rock, wote wame act kike.

Tyler Perry katika comedies zake (movies)ame act kama Madea. Mwanamke.

Martin Lawrence katika movies zake za "Big Momma" ame act kama mwanamke. Tena jimama "Big Momma".

Robin Williams ame act kama mwanamke katika "Mrs. Doubtfire".

Eddie Murphy kaenda mbali zaidi, ame act kama wanawake wawili katika "The Nutty Professor".

Katika ku act, kuweza ku act vizuri roles zinazom challenge sana actor ndio kunaonekana kujua ku act vizuri zaidi.

Kwa mwanamme ku act kama mwanamke, hiyo role ina challenge sana, ni kitu ambacho si natural, inabidi mtu afanye kazi kubwa kukipatia.

Hivyo, kwa Marekani mfano, comedian kuweza ku act kama mwanamke, inaonekana amekubali kuchukua challenge kubwa, na akiiweza vizuri, anaonekana amefuzu ku act.

Pia, hata Tanzania ambako hatukuwa na stand up comedy, ukiangalia sanaa ya muziki, wanamuziki wote wakubwa wa kiume wa muziki wa bendi washaimba kama wanawake. Ukianzia Marijani Rajab na Dar International, Ukienda Marquis, JUWATA, Sikinde bendi kubwa zote waimbaji wa kiume washaimba kama wanawake.
 

Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,663
2,000
Wengi wana element za kishoga, mwanaume huchekeshi, hawa ni wavaa bikini tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom