Kwanini sitaki kujua kipato cha mke wangu?

Kwanini sitaki kujua kipato cha mke wangu?

.labda unijuze wewe mkuu pale ulipouliza nakunukuu
1: Mtapangiliaje mipango ya maendeleo ya familia.
2: Mtapangiliaje bajeti ya miradi yenu....bila kujua kipacho CHENU.
Je hujaona hapo kwamba tayari umeingilia matumizi ya kipato cha mwanamke?..na kwa kufanya hivyo ni kujaribu kuleta usawa kati ya mwanamke na mwanaume jambo ambalo ni hatari kwa uhai wa ndoa..na pia katika ile post niliyokukoti uliongeza kwamba bila kujua mapato ya mkeo anaweza kujiingiza kwenye biashara haramu, YES inaweza kutokea, lakini si LAZIMA kwani wakati wote ndege wafananao huruka PAMOJA, hivyo basi haramu yake ni yako kabla au hata baada ya ndoa.
Mwisho kabisa ya mwanamke yafanywe na mwanamke na ya kwetu wanaume tuwajibike kwayo!!!
Ikiwa lengo la mwanamke kufanya kazi ili kusaidiana katika kuihudumia familia, haiwezi kuwa ni jambo la ajabu kwa wenza kujuana vipato vyao....kwa kuwa wao lengo lao ni moja ambalo ni kuboresha familia.....kwa wanandoa wanawajibika katika kuijenga familia yao...sidhani kama kitendo cha kupanga bajeti za miradi yenu ya kifamilia huku ukimuhusisha mkeo kwa kuwa na yeye pia ana kipato si kumuingilia matumizi yake.....kwa sababu jambo linalofanywa hapo lina manufaa kwenu wote.....ubinafsi ni sumu mbaya kwenye NDOA.....
 
Ikiwa lengo la mwanamke kufanya kazi ili kusaidiana katika kuihudumia familia, haiwezi kuwa ni jambo la ajabu kwa wenza kujuana vipato vyao....kwa kuwa wao lengo lao ni moja ambalo ni kuboresha familia.....kwa wanandoa wanawajibika katika kuijenga familia yao...sidhani kama kitendo cha kupanga bajeti za miradi yenu ya kifamilia huku ukimuhusisha mkeo kwa kuwa na yeye pia ana kipato si kumuingilia matumizi yake.....kwa sababu jambo linalofanywa hapo lina manufaa kwenu wote.....ubinafsi ni sumu mbaya kwenye NDOA.....

.wasema " lengo la mwanamke kufanya KAZI ni kusaidiana katika kuihudumia familia" hivyo basi walirudia jambo ulilolikataa hapo juu nambari 58 , kuihudumia familia ni kutumia PESA ya mwanamke, labda nijaribu kukumbusha jambo moja Tarime One alisema kwanza alimsoma mkewe hivyo basi yeye kufanya vile ilikuwa ni ushindi na amani kwenye ndoa yake, ila asijue kwamba anachokifanya ni kufuata kanuni za asili ambazo zinauendesha huu ulimwengu.
Kunaweza kuwako na aina kadhaa/mitindo ambapo ndoa zinajengwa
1: Wote wawili me na ke mnaanza katika hali duni na kupanda taratibu hadi kilele cha mafanikio, NAHISI WE UMELITAZAMA SANA HILI JAMBO KATIKA NDOA HII, nirekebishe kama nimekosea.
2: Me na Ke wote tayari wamejijenga kiuchumi na wanatoka familia zenye PESA, hapa pia tutazungumza tofauti.
3: Ke ana kipato zaidi ya Me, na pia familia yake ni bora zaidi ya Me, hapa tusiseme chochote manake bila Ustaarabu au hekima za Ke sijui!!!!
4: Me ana kipato zaidi ya Ke, wakati huo huo familia ya Me ni zaidi ya Ke.
Na aina nyingine na nyingine yategemea na namna tu utavyoweza kucheza na hali, sasa ukilitazama jambo hili kwa mapana yake mwisho wa siku litaibua mambo mengi zaidi, lakini jambo la msingi katika kumfanya mme abaki na Ukichwa wa nyumba na asifanye vile utakavyo wewe...
 
Sasa unataka iwe siri ili ukahonge au ili iweje


Ni honge ili iweje???????????? ili nijengeeee, maisha hayana kanuni, wanawake tukifiwa na waume zetu, familia inasahau kuwa marehemu alikuwa na familia, matokeo yake wanatolea macho hadi kijiko, aisee!!!!!!!!!!! muda wa kupigiana kelele sina, Lakini pia hata nikifa najua wanangu wataonyeshwa kibanda nitakachoacha kisheria hata kama baba yao ana asset pia, maana wamama tukifa wanaume wanaanzisha familia mpya matokeo yake watoto wa marehemu wanakuwa wahanga kwa mama wa kambo, ni hivo tu.
 
tufanye vyote as a man usijemuachia zile traditional responsibility mkeo eg kulipa kodi ya nyumba, kama mnajenga kiwanja ulinunua ww or both, unga, mchele si mbaya ukimuachia mambo ya mboga, matibabu lipia mme, umeme luku, maji
fenicha za muhimu kitanda unachomfanyia operation, meza ya chakula, ada watoto
unaweza muachie mke stationary na nguo mafuta mapazia business lipia ww fremu
 
Back
Top Bottom