Nadhani hapa kuna kitu hakieleweki vizuri na naamini tatizo litakuwa ni "umagharibi" tunaouiga kila iitwapo leo, hivyo vitabu mnavyonukuu juu ya nadharia ya mwili mmoja havijasema mke akija kwako ajihusishe na miradi ya maendeleo, havijasema jasho la mwanamke liliwe na mwanaume, hivyo kama mwanamke alipata nafasi ya kuwa na chanzo cha mapato kabla hajaja kwako hivyo ni vyake achana navyo,
ndio kuna wakati mke huweza kuleta mabadiriko chanya kwenye familia kutokana na PESA yake, lakini hii haikupi haki ya we kuhoji au kuona kwamba alistahili kufanya hivyo, kama kichwa cha familia huwezi kuwa na tabia za aina hii, na kwa wale ambao huweka salary zao mezani ili kupanga matumizi ya pamoja basi na wawape hao wake zao sifa za "ukichwa wa familia" yaani 50/50.
Pasipo kukwepesha maneno jambo la kujifanya unafuatilia mambo ya PESA ya mkeo limekuwa chanzo cha migogoro mingi ya ndoa za kileo/kisasa, kwani tunawabebesha majukumu wake zetu wakati huo akili zao zikiwa zimefundishwa kwa mme we "ua/pambo" nenda katunzwe..