Kwanini sitaki kujua kipato cha mke wangu?

Kwanini sitaki kujua kipato cha mke wangu?

hata ukijua haikisaidii kitu...hawa viumbe ni shida,la muhimu apambane tu ili aweze kukidhi mahitaji ya familia yake...kuerelay pesa ya mwanamke hata kama kwaasilimia ndogo tu ni headache wakuu
 
Inashangaza sana, hivi kweli natoka nyumbani kwangu giza narudi giza in the name of looking for money inakuwaje wale ninaowapenda kuliko chochote wasijue ninapata nini huko ninakotumia muda wangu na wao mwingi hivi. Je kama anaweza kunisaidia nikapata mahali bora kuliko hapa nilipo sasa. Ninachopata ni kwa ajili yao hao wengine ni ziada tu.

Na hata kama akiniachia majukumu nitafanya pale ninapoweza lakini isiwe kwa makusudi.

Umeongea vizuri sana Power to the People. "Unatoka asubuhi sana na kurudi usiku sana sio kwa ajili yako, bali kwa ajili ya wale unaowapenda..." Maneno ya busara sana!!
 
Last edited by a moderator:
Hivii hata kufanya estimation haiwezekani khaaa mbona mishahara ya nchi hii inajulikana kulingana na kazi ya MTU labdaa!!!.... Kama ni mfanyabiashara....but the rest unakadiria tu lazima utakua hapohapo au hachezi mbali

Mfano kama ni bank teller hivi hata huyu utashindww kumkadiria salary yake hahahhahhh

Kaaazi kwelikweli!!!!!!!!!!!!
 
kukiwepo na mawasiliano mazuri mshahara utaufahamu bila kuuliza hadi zile za asante kwa kazi utazijua
 
Ahsante Hute kwa wewe ulie na akili,naamini hapo ulipo hujui hata kilo moja ya nyama ni sh ngapi?mimi mjinga but this is my life experience najua natoka wapi naenda wapi na ninafanya nini?heri yako mjanja.
kilo ya nyama inategemea unanunua duka gani mzee, ni kuanzia alfu 6000 hadi alfu 10,000.utasemaje sijui? halafu, usifikiri unaongea na mtoto mdogo, mimi nimeoa kitambo lakini sijapata bahati mbaya ya kuwa na ndoa dodoki kama ya kwako. ndio maana nimekupa pole.

ila kwa ufupi ni kwamba, ukiona umeshindwa kuwa kiongizi wa familia basi wewe sio mume halisi wa hiyo ndoa, unaweza kuwa ni moja wapo tu wa wanaume wa hiyo ndoa. mwanaume unategemewa uwe unajua mshahara na kipato chochote cha mkeo na chakwako muwe mnashea na kupanga mipango pamoja na hela zile mnazitumia pamoja.

wajibu wa kutumikia familia sio wa baba peke yake kama wote mna kipato, na mnatakiwa kufanya mambo kwa umoja kwasababu mnalala kitanda kimoja. ktk ndoa ukiona mmoja wapo anafanya mambo yake kisirisiri hataki mwenzie ajue, hapo hamna ndoa. hivyo jitathimini ujione kama wewe upo kwenye ndoa au upo kwenye utumwa. by the way, ndugu zako wanalijua hili? umeoa mwanamke wa wapi? usijekuwa umelishwa limbwata mzee, nenda church wakakutapishe kwa maombi utafunguka.
 
kilo ya nyama inategemea unanunua duka gani mzee, ni kuanzia alfu 6000 hadi alfu 10,000.utasemaje sijui? halafu, usifikiri unaongea na mtoto mdogo, mimi nimeoa kitambo lakini sijapata bahati mbaya ya kuwa na ndoa dodoki kama ya kwako. ndio maana nimekupa pole. ila kwa ufupi ni kwamba, ukiona umeshindwa kuwa kiongizi wa familia basi wewe sio mume halisi wa hiyo ndoa, unaweza kuwa ni moja wapo tu wa wanaume wa hiyo ndoa. mwanaume unategemewa uwe unajua mshahara na kipato chochote cha mkeo na chakwako muwe mnashea na kupanga mipango pamoja na hela zile mnazitumia pamoja. wajibu wa kutumikia familia sio wa baba peke yake kama wote mna kipato, na mnatakiwa kufanya mambo kwa umoja kwasababu mnalala kitanda kimoja. ktk ndoa ukiona mmoja wapo anafanya mambo yake kisirisiri hataki mwenzie ajue, hapo hamna ndoa. hivyo jitathimini ujione kama wewe upo kwenye ndoa au upo kwenye utumwa. by the way, ndugu zako wanalijua hili? umeoa mwanamke wa wapi? usijekuwa umelishwa limbwata mzee, nenda church wakakutapishe kwa maombi utafunguka.

Pole sana usilolijua ni usiku wa kiza,kuendelea kubishana na wewe unaedai una ndoa ya muda mrefu😀😀😀
 
Kujua kipato cha mkeo sio mjadala...unanitia mashaka kama una 12 kwenye ndoa..ivyo ni vitu vidogo sana kujua.
 
kilo ya nyama inategemea unanunua duka gani mzee, ni kuanzia alfu 6000 hadi alfu 10,000.utasemaje sijui? halafu, usifikiri unaongea na mtoto mdogo, mimi nimeoa kitambo lakini sijapata bahati mbaya ya kuwa na ndoa dodoki kama ya kwako. ndio maana nimekupa pole. ila kwa ufupi ni kwamba, ukiona umeshindwa kuwa kiongizi wa familia basi wewe sio mume halisi wa hiyo ndoa, unaweza kuwa ni moja wapo tu wa wanaume wa hiyo ndoa. mwanaume unategemewa uwe unajua mshahara na kipato chochote cha mkeo na chakwako muwe mnashea na kupanga mipango pamoja na hela zile mnazitumia pamoja. wajibu wa kutumikia familia sio wa baba peke yake kama wote mna kipato, na mnatakiwa kufanya mambo kwa umoja kwasababu mnalala kitanda kimoja. ktk ndoa ukiona mmoja wapo anafanya mambo yake kisirisiri hataki mwenzie ajue, hapo hamna ndoa. hivyo jitathimini ujione kama wewe upo kwenye ndoa au upo kwenye utumwa. by the way, ndugu zako wanalijua hili? umeoa mwanamke wa wapi? usijekuwa umelishwa limbwata mzee, nenda church wakakutapishe kwa maombi utafunguka.

usipende saaana kulalamika ujue kipato cha mkeo andaa tu mazingira ya upendo atajiongeza tu.

fanya majukumuvyako maana ukitaka mfanye pasupasu mtagombana tu maana akikupangia zamu yakuosha vyombo, kunawisha watoto wakijinyea hutaweza
 
Mkuu,haya mambo ya ndoa yanatushinda kwa kutokujua mambo madogo,yawezekana kuna watu wakaniona mpuuzi au mjinga but kuna kitu nilikiona toka kwa wife na msukumo toka kwa ndugu zake,na kipindi hicho nilikua sijafanikisha malengo yangu na kupitia tabia hiyo niliyokutana nayo nashukuru ilinifanya nijitambue na nikasema kabisa sitakuja kutaka kujua kipato chake au kuulizia,na nashukuru nimeweza na baada ya kuona simfatilii na mambo yanakwenda poa amekua mpole na kuchukua position yake kama mke.
Ninakuwa mwansjf wa kwanza kukuelewa
 
Wanandoa ambao ni mwili mmoja.....hawawezi kufichana mambo yoyote yanayowahusu....kuanza kufichana au kutojishughulisha na mambo yanayomhusu mwenzio ni dalili mbaya ya ndoa inayoelekea kuvunjika....wanaume
tumeagizwa kuwaongoza wanawake katika njia iliyonyooka kwa kuwa sisi ndio viongozi wao na hili ni jukumu letu wanaume....
Na kumuongoza mwanamke si kwa mabavu wala kwa mangumi bali kwa majadiliano na maafikiano ynayolenga kuleta amani ndani ya nyumba na sio mifarakano.....na hapo ndio inapotimia dhana ya mwanaume kuwa kiongozi...
 
Mkuu,haya mambo ya ndoa yanatushinda kwa kutokujua mambo madogo,yawezekana kuna watu wakaniona mpuuzi au mjinga but kuna kitu nilikiona toka kwa wife na msukumo toka kwa ndugu zake,na kipindi hicho nilikua sijafanikisha malengo yangu na kupitia tabia hiyo niliyokutana nayo nashukuru ilinifanya nijitambue na nikasema kabisa sitakuja kutaka kujua kipato chake au kuulizia,na nashukuru nimeweza na baada ya kuona simfatilii na mambo yanakwenda poa amekua mpole na kuchukua position yake kama mke.

.naunga mkono hoja, pamoja na kwamba kuna wanaojifanya kutokuelewa ila njia hii ni muhimu hasa kama unataka mke aitambue nafasi yake, vinginevyo lazima atakupanda kichwani na story za haki sawa...PESA ya mke huna haja ya kuifahamu hata kuipangia bajeti, ngoja siku nioe tu..uliko ndiko nakoelekea...
 
Mimi Mume Wangu ajui kipato changu na tupo fresh aya Semeni iyo ni uamuzi Wa mtu bhana acheni mambo yenu .
 
Tarime one

Hongera mkuu!
Wewe una busara sana. Na ninyi mnaomuona mjinga huyu mnanishangaza sana ninachojua mimi amani ndio kila kitu na yeye ameamua kutafuta amani ya nyumba yake kwa style hiyo. Haina maana kujua kipato chake kama kujua huko kutawanyima amani. Alafu tumeambiwa tuishi na wake zetu kwa akili.

Ukishamjua mke wako mkono wa birika hela yake haimtoshi unadhania atakua tayari kusema anapokea shilingi ngapi. Na hizo ndio tabia za mtu mchoyo hayupo tayari kuweka wazi kipato chake ili tu usitumie nae na hizo ndio hisia zake. Sasa ukimfahamu mtu wa namna hiyo hakuna sababu.

Kaka hongera endelea kumpotezea kama hilo linakupa furaha na amani katika ndoa yako. Hawa waliozoea kelele kwenye nyumba zao achana nao.
 
Last edited by a moderator:
Na ukiona mke anaficha kipato.ujue wazazi/ndugu wanashida na wanataka wasaidiwe kila Mara.ila ni lazima ujue kipato chake.naye ajue chako
 
Back
Top Bottom