Kwanini Simba na Yanga hazichezi saa nane mchana?

Jibu limeshajibiwa ni biashara tuu
Kikubwa ujue ukikosea kupanga ratiba ligi yako itakuwa mbovu

Azam,voda na Tpbl ndio waliokaa na vilabu wakapanga

Hivi unajua simba akicheza saa 8 dar mechi za SAA 10 mbeya na kagera hazitaangaliwa uwanjani na hata kwenye tv
mkuu umeniacha hapo? kwamba Simba akicheza Saa nane sisi mashabiki wa Mbeya City tutaacha kwenda kuangalia timu yetu saa kumi? Huku mnakokuita mikoani kuna ushabiki wa kitofauti sana. Huko Dar mtu akikuambia ye Simba basi ni Simba kweli. Huku mikoani tunamiliki timu mbili. Akicheza Simba mchana basi asilimia ndogo ya mashabiki wa Simba wataingia kuisapoti Mbeya City na asilimia kubwa ya mashabiki wa Yanga wataingia kuisapoti ukiacha ile asilimia nyingine ya wazawa halisi. Ndivyo ilivyokuwa wakati tuna timu ya Majimaji, haikuwa kukosa mahudhurio hata icheze muda mmoja na Simba na Yanga.

Kuliko kuteseka ni kheri kugawana maumivu.
 
Kaka Mimi sijawahi fika dar
Ila ndio nakuambia season 2018/2019 mechi ya simba na As vita ilisababisha kuna mechi Prison vs Alience walilipa tiketi watu watatu halafu hata uwanjani hawakwenda at the same day yanga na lipuli mechi haikuwa na watu ilihali hizo mechi nilikuwa za saa 10 halafu simba yeye ilikuwa saa 1

Nchi hii ni simba/yanga sasa huwa shabiki wa yanga/simba anataka amuone mpinzani anavyoteseka
 
Ndio maana kuna mdau hapo juu nimemuuliza tunakwama wapi ikiwa huko tunakokuita duniani kote kuna timu kubwa zinacheza mapema na biashara zinaenda kama kawaida. Huoni kwamba kwa utaratibu huu timu ndogo zitaendelea kuwa ndogo na kubwa kuwa kubwa kwa kuwa tu tunazifavour kubwa? Kama umewahi kucheza mpira unaijua adha ya kucheza kwenye jua kali hasa la saa nane. Kibiashara wanaweza kuwa sahihi lakini kwenye kuinua soka letu wanakosea.
Katika hali inayoendelea sasa ni kweli kwamba mchezo wa soka Tanzania unazinufaisha timu kubwa kibiashara na kiafya.
Sababu ni nyingi.
 
Kifupi ishu hapo ni Tv coverage....Ukweli mchungu ni kwamba mechi zinazofanya biashara hiyo iendelee ni mbili tu...so ili kuendelea kui brand ligi hiyo wadhamini wanajitahidi kuonyesha mechi nyingi hivyo kuzitenganisha muda na nyingine kuchezwa saa nane ni kuwapa timu ndogo Tv coverage ni kwa faida yao..maana Azam wanapata pesa kwa Simba na Yanga tu na cha ajabu hizo timu zinazolalama zinahitaji pesa za Azam kuliko Simba,Yanga au Azam.

Kitendo cha kutaka Simba na Yanga zicheze mchana ni kutia Nazi kwenye Supu kwani hizo ndo biashara yenyewe.

Ni either hizo timu nyingine zikubali kucheza saa nane au zionyeshwe mechi chache...hapo unaitoa Azam maana yenyewe itaonyeshwa tu hata icheze saa nane.
NB: This is Africa
 
Back
Top Bottom