EJM_
JF-Expert Member
- Jul 8, 2011
- 3,836
- 2,119
Nimekuwa nafuatilia siasa za dunia na hasa kutoka Afrika, lakini kuna kitu ambacho katika siku za hivi karibuni kimeanza kuniboa na kunifanya nifikirie mara mbili kuhusu hizi siasa.
Leo hii kumekuwa na matukio ya kuudhi yanayenda kwa jina la siasa, kibaya ni kwamba matukio haya yamekuwa yakichukua maisha ya watu, kuharibu mali na kuleta hofu na wasiwasi kwa wengine. Je hii ndio Tanzania tuitakayo? Je ndiko tunakotaka tufike?
Leo hii kila tukio likitokea tunagawanyika makundi mawili, kwani kila kundi linatoka na maelezo yake tofauti na ya kundi jingine, kwasababu watanzania tumegawanyika tayari kiitikadi, hatuna hata muda wa kufikiri bali kufuata itikadi zetu zinakotupeleka. Napenda nikiri kutoka moyoni mwangu kwamba nachukia siasa ya nchi yangu Tanzania hapa ilipofikia, nachelea kusema kwamba nawachukia wanasiasa wote wanaotaka kutufikisha kwenye hali tete.
Wito wangu kama mwananchi ni huu, tayari wananchi tumeshagawanyika kiitikadi. Tunaendelea kugawanyika kiimani na tena inaletelea uadui unaopelekea mtu mmoja kuwa tayari kupoteza uhai wa mwingine kwa manufaa yake. Hebu tuacheni tuwe watanzania wenye amani, kuheshimiana, kupendana na kusaidiana. Naamini yeyote yule atakayesababisha hali hiyo kupotea sio tu kwamba hatasamehewa na watanzania, bali pia Mungu hatamsamehe.
Walioko madarakani na wanaotaka kuingia madarakani wote nyie mmekuwa chanzo cha kuiharibu nchi yetu, kamwe hatutawasamehe, tuachieni nchi yetu kama nyinyi mmechoka na nendeni huko mnakodhani ndio kwenu.
Kwa uchungu nawasilisha
- Watawala kutotaka kutoka madarakani kwa gharama yoyote ile
- Wapinzani kutaka kuchukua utawala kwa gharama yoyote ile