Habari Wakuu wangu! Japo nimechelewa lakini si mbaya nami nikaweka hili.
Kwanza napenda kuweka wazi imani yangu, kwamba katika UMOJA mimi ni muumini, na katika aina yoyote ya UMIMI mimi si muumini hata kwa ukaribu. Katika Utaifa mimi ni muotaji wa AFRIKAMOJA, lakini ni katika Ustawi wa mtu mweusi si kujifurahisha! Hivyo katika hili jambo, muhimu kwangu si kuendeleza Muungano , bali ni kufikia USTAWI wa mwanaafrika wa mipaka hii ya kwetu(TZ). Ni kuhakikisha UENDELEVU wa elements BORA na SAHIHI za mtu mweusi, kiuchumi, kisiasa na kitamaduni hayo ndio MAENDELEO. Hivyo tunapojadili aina bora ya Muungano si ile ambayo itafanya udumu bali ni ile itakayo-guarantee UENDELEVU tajwa, kama hakuna namna hiyo basi HAKUNA HAJA YA KUUNG'ANG'ANIA MUUNGANO! Binafsi ninaamini katika Nchi 1, Taifa na Serikali 1. Kama alivyosema Mkuu
notradamme, kwamba serikali 1 ni suluhisho sahihi la kuleta ustawi wetu na kuudumisha Muungano, lakini ni ngumu haswa kuifikia, naungana naye moja kwa moja. Ngumu sana kufikia lakini INAWEZEKANA, muhimu ni kutokukwepa gharama sahihi za Umoja kwa vigezo batili vya kulinda Demokrasia, kama hatuwezi kumudu gharama hizo basi tusilazimishe kuungana kwa namna isiyofaa, HAITATUSAIDIA zaidi ya kupoteza muda. Tusimame leo tupaze sauti zetu kushawishi raia kuvunja muungano, maana wote namna sahihi ya muungano tunayoiona ni impractical 'just a wishful thought', sasa kufumba macho na kugeukia nyingine kwani Kuungana nani kasema lazima!? Lengo ni kulinda Muungano au kuleta Ustawi wa mtu mweusi?
Ikumbukwe kuwa tunaposema Nchi Taifa na Serikali Moja si kuwaunganisha wazanzibar na watanganyika kiutawala tu, bali ni kuwa na Imani moja, Dira moja-FIKRA MOJA katika kuhakikisha ustawi wa TANZANIA. (Mkuu wangu
Mchambuzi anaita ni wishful thoughts, nachofurahi hata yeye anazo, ila tu hajaona uwezekano wa kuwa hai, ni hatua nzuri kuwa nazo tu, nikutie moyo Mkuu wangu you are not thinking in vain-those wishful thoughts are real/practical) Aina nyingine ya Umoja mbali na hii ni Unafiki. Tunataka tuzike Utanganyika wetu na Uzanzibari wetu chini (imani, itikadi, historia, desturi, mienendo, mitazamo) uzaliwe UTANZANIA, zao la Uzanzibar na Utanganyika kwa mujibu wa Nyakati na Mazingira yetu mahususi, ni ngumu sana lakini zaidi ya hilo ni Unafiki, ni bora kuvunja kilichopo!
Mkuu wangu
Mchambuzi anataja baadhi ya faida za Serikali 3 over 2 nadhani na 1 katika uzi wake. Ningependa kuziongelea hapa, kwa kuhusisha na practical na wishful thoughts iliyoibuka katika uzi huu!
(a) Kupata Fursa ya Ushindani. Hivi kweli tunaweza ku-guarantee good katika ushindani wa Utanganyika na Uzanzibari chini ya kivuli chepesi cha Utanzania? Kwanini hli ndio lisiwe impractical? Only 7 union affairs, ni kwa namna gani yanaweza kumfanya mzanzibari kumbeba mtanganyika akamuacha mzanzibari mwenzake? Kwa namna gani Utanzania unaweza kuubeba Uzanzibari na Utanganyika? Mkuu
Fundi Mchundo amegusia hili, Utanzania haiwezekanni kusimama mbele ya uzanzibari na utanganyika. Tena chini ya fikra hizi hizi za wao makafiri, wao waarabu, wao wakoloni, wao tunawabeba,n.k(hakuna anayekataa uwepo wake) ni ushindani gani tunaouona unawezekana? Gharama za kuondoa hilo ni kuwa na FIKRA/IMANI/ITIKADI MOJA ya kujenga Taifa moja katika kila kitu chake. Tukishndwa hilo, Je, haitotokea kama alivyosema Mkuu
Nguruvi3, serikali tatu means mwenye kisu kikali ndiye atakayekula nyama!? Undava-Undava! Nani atakula na nani atashindwa? Kwenye ushindani aina hiyo kula nyama kwa kisu chako kikali si kulitumia jasho la mwenzako? Tuko tayari kujenga matabaka ya namna hiyo, kwa gharama gani? Je, kufikia Ustawi wetu hapo ni practical ama wishful thoughts? Kwanini tuamue bora liende tu badala ya kuuvunja kabisa Muungano?
....nitarudi.....
"(b) Kupata Fursa ya kubadilishana uzoefu. (c) Kupata nafasi ya kuishi Self Rule pamoja wakati huo huo kuishi Shared Rule. (d) Kuruhusu Demokrasia. (e) Kulinda right of people to self determination, kwa hoja kuwa hakuna upande uliotayari kupoteza their identities and autonomy. (f) Kupata Ufanisi. Kupunguza kodi na gharama nyinginezo!"