Kwanini Shilingi ya Kenya ina thamani kuliko Shilingi ya Tanzania?

Wakuu hapa nina noti ya 2mil ya zimbabwe sema imechakaa
Msaada nikipeleka kuchange napata sh ngapi?
2,000,000 zimbwabwe dollar=tsh?
 
Kwanza nikutoe tongotongo. Currency ya nchi kuwa juu haimanishi kuwa na uchumi uko juu Sawa, currency kuwa juu au chini inaathiriwa na monetary na fiscal policy ya nchi husika kulingana na nini inachotaka nchi husika. Pia kumbuka ksh ipo karibu Sawa na yen ya Japan.
Maelezo hayatoshi mkuu
 
Mimi huwa naona ni digits tu ndio huwa tunatofautiana,ila sio Uchumi kukua.kwa mfano,
Shilingi 10000 ya Tanzania ni Sawa na Ksh 450 lakini hapo haimaanishi hiyo 450 ni rahisi kupatikana ukiwa kenya.ni kwamba malipo yaleyale ya tsh 10000 kwa tanzania na kwa kenya ni 450.yani mzazi fukara wa kenya hawezi kumpa mwanae 450 akatumie shuleni ni hela kubwa pia kwao.
Nadhani umezungumzia kwenye ground (uhalisia), safi sana. Hata mtu ambaye hana background of economics ataelewa 👏🏽
 
Uzuri hela ya Kenya inaenda kushuka mdogo mdogo sema huwezi kunufaika na hili Kama huna inshu kununua kutoka kenya kuja kuuza Tanzania Mana we utanunua kwa gharama chini Kenya na kuja kuuza kwa bei Ile Ile ulokuwa unauza awali.

Saiz exchange rate n Ksh 1 kwa Tsh 21.45
 
Kulingana na nadharia ya Purchasing Power Parity (PPP), fedha za nchi zina thamani inayolingana. Thamani ya pesa inapimwa kulingana na baskets of goods and services it can buy. Kama mbuzi mmoja kwa pesa ya Kenya anauzwa sh elf moja na mbuzi 'huyo huyo' kwa Tanzania akawa anauzwa kwa Tsh elfu ishirini then 1,000 ya Kenya itakuwa sawa na Tsh 20,000 ya Tanzania.
 
Lets say mtanzania una laki moja na mkenya ana laki moja. Mkenya pesa yake ina power kuliko yako. Kwa maana ya kwamba wote mki exchange na dollar mkenya anakua ana dollar nyingi kuliko ww. So kama ana dollar nyingi inamaana anaweza akanunua vitu vingi kutoka kwako kuliko ww utakavonunua kutoka kwake. Kwa maana hiyo. Atakufanya ww ulazimike kufanya kazi nyingi kuliko yeye ili ku cover kiasi alicholuzidi kwenye biashara.

Au put it this way. Imagine dunia ingekua na pesa moja. Ingekua rahidi kunielewa. Kwa sababu kungekua hakuna haja ya kutumia nguvu kukuelewesha maana mkenya sasa angetakiwa kuja na laki moja ya tanzania kununua magunia 2 ya mahindi na sisi tungeweza kwenda kenya na laki moja kununua magunia mawili ya mahindi.

Lakini kwa sababu thamani ni tofauti. Ndo maana mkemya anaweza kuja na laki moja akanunua magunia 10 ya mahindi wakati wewe ukienda na laki moja kenya unanunua gunia moja.( mfano)
Mkenya mwenye laki ni sawa na matanzani mwenye milioni mbili na laki tatu,zingatia hilo kwanza.

Yaani nguvu na thamani ya kuitafuta hiyo pesa inakwenda kwa ratio hiyo.
Usiseme mkenya akiwa na laki na mtanzania akiwa na laki.
 
Mkuu iwe mtiti isiwe mtiti. Inatakiwa ujiulize ni kwann basi kusiwe na thamani moja basi. Swali linaanzia pale kwann kuwe na tofauti ya thamani. Swala sio ugumu wa upatikanaji. Hata dollar mbona inatuzidi thamani lakini mbona ni rahisi kuipata ukiwa marekani. Ugumu wa kupata pesa sio kipimo
Ndio maana pesa ya biashara ikawa $.
Lakini kuna mahela kibao yanaizidi thamani.

Lengo ni kuweka rula kwenye biashara.ukiona unazipata $ kwa urahisi tu,ujue uko pazuri.
 
Umuhimu wa kusoma unaonekanaga kwenye mada kama hizi.
Umuhimu wa kusoma nini? Kama ni kusoma hii elimu ya darasani basi usimlaumu aliyetoa hiyo comment. Huwezi kujua kila kitu hapa duniani hata wewe binafsi hujui mambo mengi tu tena basic kwenye profession ambazo hujazisomea au hata kwenye profession yako pia. Hivyo usimdhihaki mtu mwingine ambaye ameuliza swali kwa lengo la kujifunza.
 
Umuhimu wa kusoma nini? Kama ni kusoma hii elimu ya darasani basi usimlaumu aliyetoa hiyo comment. Huwezi kujua kila kitu hapa duniani hata wewe binafsi hujui mambo mengi tu tena basic kwenye profession ambazo hujazisomea au hata kwenye profession yako pia. Hivyo usimdhihaki mtu mwingine ambaye ameuliza swali kwa lengo la kujifunza.
Yeye mwenyewe alielewa...nan amebeza? Khaa hebu punguza hate za ajabu ajabu ...mie nimelerate na yanayoendelea sasa jf wasomi vs vilaza! Hebu nitue
 
Mahindi bei ipo juu kuliko dar watu wamekata mitaji hadi wengine tunauguza depression mixer presha
Unanunua gunia la mahindi 45000 , ulisafirishe. Hadi manzese dar halafu unakuta gunia hilo bei ya soko ni 35000
Ukiwa na gunia 300 plus , kuzimia na. Kuanguka inakuwa ni option rahisi, kuliko kukomaaa ukagongwe na magari kwa mawazo
Wasalimie isaka hapo
 
Wakuu turejee.

Huwa najiuliza. Wanaohusika ku adjust (kupandisha na kushusha) thamani ya pesa kwenye mataifa ya kidunia ni nani (najua hii process haifanyei na mungu inafanywa na binadamu)

Pia nilikua najiuliza, Kenya mbona sometimes uchumi wake unayumba lakini thamani yake ya pesa inanaki palepale licha ya kwamba tanzania kuna mali za kutosha na nguvu kazi. Na sisi ndo tunalisha almost east africa nzima. Kama sisi ndo tunategemewa kwa nn sisi ndo pesa yetu isiwe na value kuliko pesa ya nchi yoyote inayo tuzunguka east afrika. Tunafeli wapi.

Pia tunajua nchi kama Kenya thamani yake ya pesa ni kubwa kuliko yetu inakua na advantage kubwa sana kutulalia. Kwa maana ya kwamba. Kwa kazi ile ile atakayofanya Mkenya na Mtanzania.

Mkenya ata gain more akitumia pesa yake. Kwa maana ya kwamba mkenya akija na pesa yaje Tanzania anaweza akanunua magunia ya chakula mengi zaidi kuliko wewe ukienda kenya na tsh. Kwa hiyo hii inampa mkenya advantage ya kutofanya kazi nyingi kama mtz.

Hii ni opinion yangu. Kama una i-challenge. Naomba uje kwenye mada.
Aje Zitto hapa atudadavulie hii mada
 
Kwanza nikutoe tongotongo. Currency ya nchi kuwa juu haimanishi kuwa na uchumi uko juu Sawa, currency kuwa juu au chini inaathiriwa na monetary na fiscal policy ya nchi husika kulingana na nini inachotaka nchi husika. Pia kumbuka ksh ipo karibu Sawa na yen ya Japan.
Hujajibu
 
Ukitaka kujua tulifikaje hapa inabidi uanzie kwenye vita ya kagera na after effects zake then uje kwenye masharti ya ifm na wb kwa Nyerere kutaka serikali ishushe thamani ya shilingi yake ili ipate misaada..since then tumeweza ku maintain the gape difference bt not catch up to them.
Yeye hajui ,mjibuni ache mbwembwe
 
Kuhusu nani anaudjust sijui.
kuhusu pesa fulani kua kubwa kuliko nyingine,...hio haireflect uchumi wa sehemu ama nchi husika....kinachoangaliwa ni PPP=Purchasing Power Parity,...uwezo wa hio pesa kufanya manunuzi katika sehemu husika,usd 2,ni sawa sawa na Iran rial 80,000 lakini usd 2 Iran unapata kikombe cha kahawa,marekani hupati....hapo means kwa value ile ile purchasing power ya rial ipo juu Kuliko US dollar.......ukubwa wa pesa haupimwi kwa wingi wa masifuri bali hupimwa kwa wingi wa uwezo wa manunuzi
 
N nouma juzi nilituma pesa kwenda kenya kupitia m-pesa. Mambo yalikuwa hivi
1.100,000tsh=4,444ksh
2.350,000tsh=15,400ksh.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
Hio 4,444ksh ni pesa ya mshahara mkubwa tu wa mtu Kenya,na huwezi kumiliki hata kipande cha ardhi kulima.
Ila laki 1 Tanzania ni mshahara wa kibarua tu,na hio laki moja unaweza kodi/kununua ardhi mwaka mzima na kulima.....hapo utaona pesa ipi ina thamani Kati ya Ksh ama Tsh?
 
Back
Top Bottom