Kwanini shetani anaogopa kuua mwanadamu?

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,507
Reaction score
45,128
FB_IMG_1459534434755.jpg

SHETANI ni kiumbe ambaye alikuwa Malaika na akiishi Mbinguni siku zile kabla hajaFanya uasi. Mwenyezi Mungu alimpenda na kumpatia nguvu na uwezo mwingi na kumfanya Malaika Pendwa huko mbinguni.

Baada ya UASI - Kujifanya yeye ni kama mwenyezi Mungu, Mungu alimpa adhabu ya KUMTUPA HAPA DUNIANI; ambapo ameungana nasi baada ya sisi wanadamu kutumbukia kwenye dhambi ya asili iliyosababishwa na udanganyifu wake kwetu.

SHETANI hayupo huru bado yupo kifungoni KUZIMU na amefungwa miaka 6666; ingawa yupo kule na timu yake bado amekuwa kinara wa maovu mengi hapa duniani, bado anashindana na uwezo wa Mwenyezi MUNGU na ubishi uliopo ni kwamba atahakikisha sisi wanadamu tunaacha kumwabudu Mwenyezi Mungu na tumwabudu yeye pekee yake.

SHETANI anataka kutuaminisha kwamba NGUVU ZAKE ni kali na zinatenda au kutoa majibu mubashara kwa wale watakaotaka kutumia kuringanisha na zile za MWENYEZI MUNGU ambazo unaweza kuomba ukazisubiri hadi ukazeeka na usizipate.

Lakini pamoja na hayo yote SHETANI ni Muoga mno wa kutoa ROHO YA MWANADAMU - Je umewahi kujiuliza ni kwa nini??? Fanya utafiti huo kwa kina.

Lakini cha ajabu MWANADAMU yeye haogopi kutoa roho ya mwanadamu mwenzake, iwe kwa maslahi yake au ya watu wengine, yawe ya kidini ama ya kisiasa lakini HAOGOPI kumuua mwanadamu mwenzake.

Mwanadamu hajajifunza kwa nini SHETANI ambaye pamoja na kuzijua baadhi ya SIRI ZA UUMBAJI WA MBINGU na DUNIA kwa nini abakie kuwa muoga mno wa kutoa UHAI WA MWANADAMU ? (Kumwaga damu ya Mwaandamu)

EEE MWANADAMU ULIYEZALIWA NA MWANAMKE - ACHA KABISA ACHA KABISA KUUA BINADAMU WENZAKO - ADHABU YAKE JUU YAKO WEWE NA KIZAZI CHAKO HADI CHA TATU NA NNE.

(Ujumbe mubashara kwa wauaji wote - acheni mara moja)

Tunaamini KIZAZI cha WAUAJI ni kizazi cha KAINI ambacho kililaaniwa milele baada ya MAUAJI ya Nduguye Abel.
cain-slaying-abel-jacopo-palma-1590.jpg
 
Sasa Kwanini wengi huua kwa kutumia nguvu za shetani?????
 
Shida ya shetani ni kuhakikisha ulimwengu wote unamsujudu yeye. Mwanadamu Kiumbe aliyependwa sana na Mwenyezi Mungu wakati wa uumbaji atahakikisha anamteketeza na anakuwa wa kwake.. Shetani Hataki apate hukumu peke bali yeye pamoja na wanadamu wote.

Kwa mfano Shetani ndiyo hupandikiza chuki ambazo zinakupelekea wewe kuua mwanadamu mwenzako, ukishatenda hivyo tu yeye hutoka eneo hilo na kukuacha uhangaike na dhambi ile. Wengi baada ya kutenda dhambi ile huchanganyikiwa na kuishia kujinyonga ama kufa kwa kihoro.
 
Je, ni kweli watu wengine wanauliwa kwa manufaa ya mfano Taifa?????
Bado hapo ni shetani.

Je, anayefanya hivyo hana dhambi eti kutokana na nafasi aliyonayo????
 
Sasa Kwanini wengi huua kwa kutumia nguvu za shetani?????
Kazi kuu ya Shetani ni
Kuua
Kuiba
Kuharibu
Vile ambavyo vimeumbwa na Mungu.
Mambo hayo anayafanya kwa wale tu ambao hawamwabudu Mwenyezi Mungu aliyeumba Mbingu na Nchi.
Kwa wale wanaomwabudu Mungu Shetani hawezi kuwadhuru kwani Mungu mwenyewe anawakinga na kuathiriwa na nguvu za Shetani.
Hivyo basi kama humwabudu Mungu kwa dhati au unamwabudu Shetani kwa kujua au kutokujua, wewe upo kwenye hatari ya kudhuriwa na Shetani mda wowote akikukusudia kwakuwa huna kinga Mungu.
Shetani anaua.
 
Shetani anasingiziwa mengi
Binafsi Mimi nishawahi kumwona shetani
Yupo Na sura kama ya JIWE
tena amechubuka kama maganda ya korosho
Lakini cha ajabu shetani anamwogopa Sanaa Mangi.
 
Hizi zote ni nadharia tu, tunasingizia vitu tusivyoviona ili kujipa matumaini ya makosa yetu kila siku.

So many questions could be asked of the devil and God. Why did God allow so much to happen to the people he loved the most, why death, why didn't the devil perish.... if he knew that Adam would sin, why did he allow all this to happen.

Kuna wakati unaweza kufikiri hadi nje ya horizon, and that's when blasphemy begins.
 
Kabla cjamaliza kusoma uzi wako maomba nikurekebishe kidogo. Kwamba shetani hakuwa malaika bali alikuwa katika malaika ila na yeye alikua na umbile lake tofauti kabisa na malaika.
 
Anaogopa kuuwa kwa sababu amefungwa jela akitoka ataanza kuuwa Ova
 
Je, ni kweli watu wengine wanauliwa kwa manufaa ya mfano Taifa?????
Bado hapo ni shetani.

Je, anayefanya hivyo hana dhambi eti kutokana na nafasi aliyonayo????
SHETANI hafurahii kabisa Familia, Ukoo ama nchi ikiwa na amani, Yeye kazi yake ni kuleta mifarakano kati yenu ili yeye apate kufurahia utukufu wake - nia ni kuona Dunia nzima inakuwa cya hini himaya ya kishetani.

Kwa mfano nchi ikiwa na amani muda mrefu, yeye atafanya mbinu zote hata ikiwezekana kuwatafutia kiongozi ambaye either yeye atakuwa chanzo cha uovu ama ninyi watawaliwa ndiyo mtakuwa chanzo. Sasa mkianza mabishano lazima atawapa ujasiri wa kuuana, mkishamwaga damu yeye anafurahi na atamwambia Mwenyezi Mungu unaona hao, nilikwambia wote watakuwa kwenye himaya yangu tu.

Kumbuka SHETANI pamoja na kuwa kifungoni bado ana nguvu kubwa mno ya kupenya katika kila nafsi ya Mwanadamu na kujaribu kufanya yake - so we;re all not safe - sababu akishakukuingia wewe hutajijua, utafanya maamuzi unayoyajua wewe bila kujali madhara yatakayofuatia.

Kwa mfano ulishaona mtu na akili zake timanu akawachinja watoto wa kuzaa mwenyewe - tena wadogo kiasi kile?
 
Anaogopa kuuwa kwa sababu amefungwa jela akitoka ataanza kuuwa Ova
hapo tuliulize kafungwa ila anatuma nguvu zake toka KUZIMU hadi Duniani na zinatenda kazi, Je akiwa HURU itakuwaje??
 
Kabla cjamaliza kusoma uzi wako maomba nikurekebishe kidogo. Kwamba shetani hakuwa malaika bali alikuwa katika malaika ila na yeye alikua na umbile lake tofauti kabisa na malaika.
Sawa, Pointi yangu ni kuwa alikuwa among the leaders wa Mbinguni akimsaidia Mwenyezi Mungu kwa ukaribu - kwa mantiki hiyo anajua baadhi ya SIRI za uumbaji na ndiye aliyewafundisha wanadamu kuzitengeneza na kuziumia nguvu hizo (Tunaita nguvu za giza) ambazo ndizo wanadamu wanazitumia kuuana ama kutesana wao kwa wao huku yeye akichekelea.
 
Kabla cjamaliza kusoma uzi wako maomba nikurekebishe kidogo. Kwamba shetani hakuwa malaika bali alikuwa katika malaika ila na yeye alikua na umbile lake tofauti kabisa na malaika.
Alikuwa na umbile gani? Na kwanini yeye alikuwa na hilo umbile tofauti na wengine?
 
FB_IMG_1459534434755.jpg

SHETANI ni kiumbe ambaye alikuwa Malaika na akiishi Mbinguni siku zile kabla hajaFanya uasi. Mwenyezi Mungu alimpenda na kumpatia nguvu na uwezo mwingi na kumfanya Malaika Pendwa huko mbinguni.

Baada ya UASI - Kujifanya yeye ni kama mwenyezi Mungu, Mungu alimpa adhabu ya KUMTUPA HAPA DUNIANI; ambapo ameungana nasi baada ya sisi wanadamu kutumbukia kwenye dhambi ya asili iliyosababishwa na udanganyifu wake kwetu.

SHETANI hayupo huru bado yupo kifungoni KUZIMU na amefungwa miaka 6666; ingawa yupo kule na timu yake bado amekuwa kinara wa maovu mengi hapa duniani, bado anashindana na uwezo wa Mwenyezi MUNGU na ubishi uliopo ni kwamba atahakikisha sisi wanadamu tunaacha kumwabudu Mwenyezi Mungu na tumwabudu yeye pekee yake.

SHETANI anataka kutuaminisha kwamba NGUVU ZAKE ni kali na zinatenda au kutoa majibu mubashara kwa wale watakaotaka kutumia kuringanisha na zile za MWENYEZI MUNGU ambazo unaweza kuomba ukazisubiri hadi ukazeeka na usizipate.

Lakini pamoja na hayo yote SHETANI ni Muoga mno wa kutoa ROHO YA MWANADAMU - Je umewahi kujiuliza ni kwa nini??? Fanya utafiti huo kwa kina.

Lakini cha ajabu MWANADAMU yeye haogopi kutoa roho ya mwanadamu mwenzake, iwe kwa maslahi yake au ya watu wengine, yawe ya kidini ama ya kisiasa lakini HAOGOPI kumuua mwanadamu mwenzake.

Mwanadamu hajajifunza kwa nini SHETANI ambaye pamoja na kuzijua baadhi ya SIRI ZA UUMBAJI WA MBINGU na DUNIA kwa nini abakie kuwa muoga mno wa kutoa UHAI WA MWANADAMU ? (Kumwaga damu ya Mwaandamu)

EEE MWANADAMU ULIYEZALIWA NA MWANAMKE - ACHA KABISA ACHA KABISA KUUA BINADAMU WENZAKO - ADHABU YAKE JUU YAKO WEWE NA KIZAZI CHAKO HADI CHA TATU NA NNE.

(Ujumbe mubashara kwa wauaji wote - acheni mara moja)

Tunaamini KIZAZI cha WAUAJI ni kizazi cha KAINI ambacho kililaaniwa milele baada ya MAUAJI ya Nduguye Abel.
cain-slaying-abel-jacopo-palma-1590.jpg
mi kama nimekuelewa tofauti!!!yaani ni kama unamzungumzia mtu flani...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom