Impotent ilishaelezewa humu mara kibao.Jamani mimi kidogo kiingereza kinanipiga chenga, sasa naomba mnisaidie tafsiri sahihi ya KISWAHILI katika maneno haya ambayo yote nimeyasikia kutoka mjengoni Dodoma
1. FAKI YU
2. IMPOTENTI
Nawasilisha
Nyerere: "waswahili wana mambo ya ajabu. mambo ya kijinga jinga yakisemwa kwa kiingereza, wanashangilia kana kwamba ni mambo mema"
Hayo ni baadhi ya maneno aliyoyasema baba wa taifa Mwl Julius K. Nyerere katika moja ya hotuba zake.
Tusi alilolitoa Serukamba ndio tusi kubwa kuliko yote yaliyowahi kutolewa bungeni mpaka sasa. Tofauti na mengine yeye lake amelitoa kwa kiingereza kiasi kwamba naibu spika ameliona ni jema hivyo kutomchukulia hatua yoyote.
Hata majadiliano yanayoendelea sasa miongoni mwa wananchi na viongozi ni kuhusu "utovu wa nidhamu" wa Tundu Lissu wa kuomba miongozo na taarifa kila mara hivyo kutimuliwa bungeni na wenzake waliokuwa wakipinga kitendo cha naibu spika kumtoa nje. Hili la Serukamba halizungumzwi kama ni tusi kuu bungeni.
Tatizo ni kama alivyosema Nyerere, katukana kwa kiingereza hivyo spika na naibu wake hawaoni kuwa ni tusi. Waziri mkuu haoni kuwa ni tusi. Aibu!
Ili uwe Mbunge au Spika unatakiwa uwe na sifa gani?Naibu Spika ni Afisa wanyamapori kiprofesheni, hivyo tusimlaumu sana wajameni. Kitendo cha mnyama mmoja aliyesimama kumnyea mnyama mwingine aliyekaa au aliyejilaza ni kawaida sana tu kule mbugani na zizini.
Ndugu yangu, wapo watu wengine walipewa tu ubunge hata hawahusiki wala hawakustahili kivile. Cheki waliomo:-Hivi Ndugai si alikuwa mesenja tu mle bungeni,kutumwa vikaratasi na kina Mzindakaya,ubunge aliupatapataje?!
Nilichojadili sio sifa ya kuwa Mbunge. Mjadala ni busara ya mtu. Kama Naibu Spika busara yake ilimtuma kutokereka na neno F*#@ YOU lililo nje ya kanuni ambalo alilisikia vizuri tu wala asishituke, badala yake akakereka dhidi ya mtu anayeomba mwongozo kwa mujibu wa kanuni, nadhani busara yake inaweza kuonekana kirahisi.Ili uwe Mbunge au Spika unatakiwa uwe na sifa gani?
Hakuna sehemu inayotaka uwe na sifa km za TUNTEMEKE SANGA (R.I.P.}
Hakuna sehemu inayotaka uwe na umri mkubwa
Unachotakiwa uwe na Umri wa miaka 18 na Elimu ya Msingi
sasa sijui Ndugai ana tofauti ipi au mnalazimisha tu?
Hakuna Mbunge yeyote ila serukamba tu ndiye aliyeomba Radhi kwa neno lilomtoka la Tusi kati ya Wabunge wote waliotamka Matusi ndani ya Ukumbi kwa hiyo sionoi haja ya kushupalia mtu aliyekiri alipotoka licha ya kuwa kuna mtu alimsababishia hasira hizo
(Star Tv Naibu Spika kakiri humo Ukumbini huwa kuna matusi mengi sana amabayo vinasa sauti viakuwa mbali kunasa)
By saronga
Jamani naomba tafsiri sahihi ya KISWAHILI katika maneno haya ambayo yote nimeyasikia kutoka mjengoni Dodoma
1. FAKI YU ------------------- Maana yake unakandamizwa
2. IMPOTENTI -------------------- Maana yake Huwezi kukandamiza