Kwanini Serikali yetu isitumie mbinu hii ili kufikisha maji sehemu ambazo zinahitaji wa maji kwa uharaka ilo kukabiliana na tatizo la maji

fundi bishoo

JF-Expert Member
Jun 26, 2018
12,956
22,650
Habari wakuu kwema?

Kutokana na changamoto ya nchini kwetu la tatzo la maji safi nchini mi naona kama serikali yetu pendwa ikitumia mbinu ya kuweka mabomba ya maji makubwa yategwe juu yaani kama zilizopita lines za tanesco.

Zile nguzo ambazo zinakuwa zimetegwa sasa bomba la maji ili lisiweze kuanguka lifanyiwe namna yyte ili zisipelekwe hata na upepo yaan kwa kutega hivyo naona wataokoa muda kuliko kuanza kuchimba chimba umbali mrefu.

Imagine mtu anachimba kutoka masaki mpka Gongo la Mboto tena kwa sururu jambo ambalo unakuta linachukua mwezi ila kwa kutega bomba juu zitachukua week kadhaa tu na hata matengenezo yake yatakua nafuu na haraka na pia wataweza kuwadhibiti wezi wa maji ya dawasco.

Pia hii huduma itakua nzuri maana kuna watu tunakaa maeneo ambayo mpka leo maji hayajafika na hatuoni dalili za maji kufika.

Ahsanteni sana naitwa fundi bishoo

yes biShoo haswaaaaaaaaaH
 
IMG_5122.jpg
 
Bomba la maji likijaa hewa ni hatari sana angalia duniani kote maji hupita chini isipokuwa kwenye maeneo fulani ambapo bomba husika huwekwa reinforcement ya hali ya juu. Wacha yapite chini na ndio asili yake
 
Bomba la maji likijaa hewa ni hatari sana angalia duniani kote maji hupita chini isipokuwa kwenye maeneo fulani ambapo bomba husika huwekwa reinforcement ya hali ya juu. Wacha yapite chini na ndio asili yake
Aaaaah hapo sasa nimekuelewa ww ndo u.enipa sababu ya kitaalamu kabsa lakini endapo zitawekwa bomba ambazo kama za cguma au za cement kama za makalavati ya kuptsha maji machafu ya mitaroni hii zile s haziingz upepo
 
Nawaza bomba zitavokuwa zimetapakaa huko juu mkuu
😁😁😁 sio kam zitakua hovyo hovyo hapana iLa zinakua kwenye mpangilio mzuri tena unakuta zinanakshiwa na rangi nzuri just imagine pia itatumika kama vivutio vya utaLii pia ujue tutakua na mfumo wa kipekee duniani
 
Msukumo hutumika kuyafanya maji yafike kule kwa wahitaji, na kama mabomba yakiwekwa juu halafu bomba likapasuka basi hasara si ya idara ya maji tu bali ni ...inaweza ikasababisha vifo kutokana na shoti za umeme, kuharibu vitu ambavyo si rafiki na maji.. mfano sokoni kuna wauza mchele, unga, n.k. Hiyo itakuwa ni hasara.

Imagine umo chooni(Vile vyoo vyetu vinavyoangalia mbingu) unakula zako raha duniani, mara unaona bomba limekufata, linakuogesha 😆.

Njia rahisi ni kuwepo tu kwa vituo vingi. Waweke mabomba ya kuanzia Inchi 2 na kuendelea ili mwenye uhitaji ataunganisha karibu.
 
sio kam zitakua hovyo hovyo hapana iLa zinakua kwenye mpangilio mzuri tena unakuta zinanakshiwa na rangi nzuri just imagine pia itatumika kama vivutio vya utaLii pia ujue tutakua na mfumo wa kipekee duniani

oy mkuu hii kitu ungetoa mchoro ingekuwa rahis kueleweka sana
Em fanya mpango wa picha ya mchoro mkuu
 
Msukumo hutumika kuyafanya maji yafike kule kwa wahitaji, na kama mabomba yakiwekwa juu halafu bomba likapasuka basi hasara si ya idara ya maji tu bali ni...
Hhahahhhah mkuu nimekupata vyema acha uzi ufungwe ila amini ipo siku hii idea yngu itatumika tu kwenye nchi zetu afrika mashariki trust my words chief sio leo wala keaho miaka 50 mbele huko
 
Mkuu hilo zoezi ulisha wahi kuliona nchi gani? Ili tufanye pilot study zaidi
 
Mkuu hilo zoezi ulisha wahi kuliona nchi gani? Ili tufanye pilot study zaidi
Nimegoogle apa sasa hv nmeona kenya wametumia ila very local naoan wameweka mitaa ya kibera😁😁😄 kampuni inaitwa shefco nadhani
 
Tupo tunaiangalia kwa undani plea bargaining kwanza.

Sad truth, "Focus ya serikali sio kumpa urahisi mtanzania ndio maana hakuna Sheria hata zinazompa urahisi, everything is hard than a stone in this country"

Tunasema maji ni uhai ila ni mtihani kuyapata katika baadhi ya maeneo.
 
Back
Top Bottom