Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Watu wanasema unapokuwa na njia ambayo kwa miaka mingi haizai matunda na bado unaing'ang'ania badala ya kutafuta njia mbadala ya kutatua tatizo, wewe una tatizo la akili.
Suala la upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi, mijini na vijijini, limekuwa jambo ambalo limeumiza kichwa serikali kwa miaka mingi sana. Kuna wakati huduma hii ilikuwa chini ya mamlaka ya serikali mija kwa moja - Idara ya Maji chini wa Wizara. Hili halikufaniliwa.
Utaratibu wa huduma za maji uliopo sasa ndio unachanganya kuliko hata huko nyumba. Tunashindwa kuelewa nani hasa ndio mwenye mamlaka kaitika suala la maji. Unakuta Wiara ipo, na serikali za miji zipo, na mwisho wa siku haieleweki nani ana mamlaka zaidi ya mwenzake.
Kuna Board za maji zimeanzishwa lakini ni kama hazina meno, zipo zipo tu!
Sasa wakati umefika tutafute namna mpya ya kushughulika na suala la maji nchini. Tunapaswa kufikira kwa makini uwepo wa Shirika la Maji la Taifa, ambalo majukumu yake yatakuwa kama lilivyo TANESCO, na pia kuwa na Rural Water Access Agency, ambayo majukumu yake yatakuwa kama ilivyo REA. Shirika hili linaweza kuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kulipa uzito au Wizara ya Maji ikibidi
Kwa upande wa Shrika la Maji, hili litapaswa kujiendesha kibiashara. kwa ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya. Ruzuku toka serikalini inaweza kuwapo mwanzoni lakini baada ya muda fulani tutatarajie lijiendeshe kwa faida.
Ni kweli huko nyuma tulikuwa na NUWA (National Urban Water Authority) , na lengo lilikuwa zuri bali lilikumbwa na mihemuko ya kisiasa enzi za ubinafsishaji likatenguliwa. Tuanzishe kitu bora zaidi.
Rural Water Access Agency, kama ilivyo REA, itapewa ruzuku toka serikalini, na pia kutakuwa na levy (tozo) toka kwenye bili za maji za Shirika la Maji la Taifa kwa ajili ya kuendeleza upatikanaji wa maji vijijini.
Ningependa sana Kitila Mkumbo watafakari kwa makini pendekezo hili na kulifikisha kwa Magufuli ili lifanyiwe utekelezaji.