Kwanini serikali ya CCM inazidi kukopa fedha wakati tuna deni la trilion 22?

Mtumishi Wetu

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
5,712
1,906
Wakuu salaam,

Kama serikali hii ya CCM ina huruma na watu wa Tanzania kwa nini inangangania kukopa fedha zaidi kwenye mabenki na mashirika ya kimataifa wakati tunalo deni la Trillion 22?

Kweli hawa wakubwa zetu wana huruma na Watanzania, fedha zoote hizo wana kopa ili wazifanyie nini, ni shughuli za maendeleo au matumizi ya anasa?

Kuna ukweli wowote uchumi wa nchi hii unakua kwa 7%?

Tafadhari hebu tutafakari kuhusu hilo, au ni mlengo wa kuangamiza taifa letu kulitumbukiza kwenye utumwa wa madeni???
 
Mtumishi Wetu,

Serikali ya CCM ipotayari kuwaweka Watanzania wote rehani ili mradi iendelee kuwa madarakani. Vyama vya upinzani vimeifanya serikalli yetu kuwa katika wakati mgumu sana hasa kwenye suala la maendeleo katika nchi yetu.

Wanapohojiwa kuwa hakuna maendeleo yaliyofanyika katika nchini hawana la kusema kwani fedha za walipa kodi zinaishia katika matumbo ya wachache.

La kufanya ni kukopa ili kuonyesha kuwa kuna maendeleo yaliyofanywa na CCM, wakati ni madeni tunarudhisha vizazi na vizazi vijavyo.

Tutafakari sana Watanzania tunapelekwa wapi na aina ya viongozi tulio nao na chama chao. WANATUANGAMIZA.
 
Last edited by a moderator:
Sababu ya kwanza: Lazima kutimiza ahadi za kampeni

Sababu ya pili: Haijulikani nani atakuwa rais come 2015, hivyo shauri yake juu ya madeni atakayokutana nao

Sababu ya tatu: Serikali hii inakoma 2015, ni wakati wa kusanyakusanya. Sasa watakusanya wapi kama mahela hakuna?
 
mnduoeye

Hiyo ni kweli maana kama wanahitaji kubembea na fedha za budget ni zile zile si lazima wakope ili waonekane wanafanya maendeleo? Tanzania isisile, tumevishwa zigo zito la madeni nani wa kutuokoa?

Last edited by a moderator:
Mimi na wewe ndio mwokozi wa nchi yetu yenye madini na raslimali lukuki ambazo tunawagawia wageni kwa 10%.Hamasisha watu 20,washauri rafiki zako 20 wahamasishe watu 20 kila mmoja alipo wajiandikishe kupiga kura na waende kupiga kura 2015 tuondoe hawa mafedhuli wanaotuuza ndani ya nchi yetu.SISI WATANZANIA TUKOMBOE NCHI YETU CHINI YA WAFEDHULI HAWA.
 
Wakuu salaam,

Kama serikali hii ya CCM ina huruma na watu wa Tanzania kwa nini inangangania kukopa fedha zaidi kwenye mabenki na mashirika ya kimataifa wakati tunalo deni la Trillion 22?

Kweli hawa wakubwa zetu wana huruma na Watanzania, fedha zoote hizo wana kopa ili wazifanyie nini, ni shughuli za maendeleo au matumizi ya anasa?

Kuna ukweli wowote uchumi wa nchi hii unakua kwa 7%?

Tafadhari hebu tutafakari kuhusu hilo, au ni mlengo wa kuangamiza taifa letu kulitumbukiza kwenye utumwa wa madeni???

Serikali haina pesa,pesa iko kwa viongozi..kwa nn wasikope ili wao wanenepe?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Haieleweki magamba wana maana gani.wabunge wanaliona hili?.mimi naidai taasisi moja iliyoko chini ya tamisemi zaidi ya milioni 50 tangu 2010.fikiria nimetoa huduma kwenye taasisi hii kwa kukopa benki,saccos, vikoba na riba zake zinapanda tu.sijui nitalipwa lini.nimetembelea taasisi hii mpaka nimechoka.kwanza walisema fedha zimeenda kwenye uchaguzi,sasa wanasema wamepeleka madeni wizarani!wanajf nipeni njia nitapataje fedha zangu?
 
Mimi na wewe ndio mwokozi wa nchi yetu yenye madini na raslimali lukuki ambazo tunawagawia wageni kwa 10%.Hamasisha watu 20,washauri rafiki zako 20 wahamasishe watu 20 kila mmoja alipo wajiandikishe kupiga kura na waende kupiga kura 2015 tuondoe hawa mafedhuli wanaotuuza ndani ya nchi yetu.SISI WATANZANIA TUKOMBOE NCHI YETU CHINI YA WAFEDHULI HAWA.
Mkuu hiyo ni sawa kabisa, ila huyu atakaye ingia madarakani atakuta kuna nini, kama sio mzigo wa madeni????
 
Najaribu kuwaza
Wasipokopa na national coffers zikawa tupu watu wakakosa mishahara na huduma muhimu itakuwaje?
Lakini ndugu yangu kumbuka, kuanzia asubuhi hadi jioni mafuta yanauzwa, VAT zinakusanywa, kodi zinalipwa fedha kibao zinakusanywa kila kona, fedha zoote hizo zinakwenda wapi???

Haieleweki magamba wana maana gani.wabunge wanaliona hili?.mimi naidai taasisi moja iliyoko chini ya tamisemi zaidi ya milioni 50 tangu 2010.fikiria nimetoa huduma kwenye taasisi hii kwa kukopa benki,saccos, vikoba na riba zake zinapanda tu.sijui nitalipwa lini.nimetembelea taasisi hii mpaka nimechoka.kwanza walisema fedha zimeenda kwenye uchaguzi,sasa wanasema wamepeleka madeni wizarani!wanajf nipeni njia nitapataje fedha zangu?
Pole mkuu ni bora ukamfuata waziri wa hiyo taasisi ukapresent kesi yako, mwambie utamtoa kwenye media (press), lakini chunga wasije kukulimboka!!!

Hawawatofautishii raia kati ya Economic development na economic growth...hizo 7% ni growth na si development jamaani so maisha mabovu bado yataendelea kuwa Bongo kama tunakopa tu na mwisho wa siku tutawekwa bond kabisa!!

"How can we follow leaders when they are corrupt one??"....
 
My Brother Tanzania woote tumewekwa rehani, hatuwezi kufurukuta watachukua kila kitu wanavyotaka, hata udogo wetu kama Kahama mine watachukua sisi tutaangalia tuu!!!

Wewe unaijua vizuri bajeti ya gvt au umejisikia kuandika.
Kipindi cha Mheshimiwa Mkapa mbona alikuwa anajitahidi kulipa madeni hadi akabakiza deni kidogo, je kukopa bila mkakati wa kulipa ndio kuijua vizuri badgeti???

Hawa wanajiandaa kuondoka, Lakini Mungu saidia watarudisha tu hela zote.
Haki ya Mama Lazima waonyeshe Hela Ilipo.
Fedha zoote walizoficha Uswiss, Caymans Island, Off Shore Acct zote tunahitaji fedha zetu, waliofilisiwa ni Watanzania walala hoi, wakae wakijua kuwa tunataka fedha zetu!!!MTU ETI ANASAMEHE WEZI WA MABILLION WA EPA, mbona wanangangana na wezi wa halmashauri, wepi wezi wakubwa???

Wanakopeshwa pesa.zikifika tz wanaziiba tena wanaenda kuhifadhi kwenye mabenki nchi za huko walikokopeshwa.
Hapo mzungu ndio anapochoka na Miafrika
 
Wanakopeshwa pesa.zikifika tz wanaziiba tena wanaenda kuhifadhi kwenye mabenki nchi za huko walikokopeshwa.
Hapo mzungu ndio anapochoka na Miafrika
Naona wamegundua mabenki ya kiarabu Kuwait, Qatar, Abdhabi, hadi Baharin sijui kama kweli hao watatupa data za fedha za wizi kama ulaya!!!!

Back
Top Bottom