Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,156
- 31,049
Kuna mambo mengine nchi hii yanashangaza na kusikitisha kweli.
Mtu kalima kahawa zake, kwa pesa zake na nguvu zake halafu unampangia amuuzie nani. KCU imekusanya kahawa za wakulima halafu huu karibu mwezi wa 3 hawajawalipa pesa yao.
Hiki chama cha ushirika hakina maana tena bora waache watu wanunue tu kahawa. Zamani ilikuwa lazima kukiuzia walau kipindi kile kilikuwa kina maana kwakuwa kilikuwa kinawapa wakulima miche bora, kilikuwa kinasomesha watoto, kilikuwa kinajenga mashule.
Haya yote kwa sasa hakuna, yani KCU ni sawa na kampuni tu kama kampuni nyingine. Halafu mbaya zaidi niliona mkuu wa mkoa wa Kagera kwenye TV miezi kadhaa iliyopita akijinasibu kwa kuiagiza KCU iwalipe wakulima pesa yao ndani ya siku mbili.
Majaliwa mzee wa mashirika ya Umma iangalie KCU imeua zao la biashara Kagera, maana kwanza kahawa bei chini na kulipwa nako shida.