Kwanini Serikali isiruhusu watu na kampuni binafsi wanunue kahawa mkoani Kagera?

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,027
Kuna mambo mengine nchi hii yanashangaza na kusikitisha kweli.

Mtu kalima kahawa zake, kwa pesa zake na nguvu zake halafu unampangia amuuzie nani. KCU imekusanya kahawa za wakulima halafu huu karibu mwezi wa 3 hawajawalipa pesa yao.

Hiki chama cha ushirika hakina maana tena bora waache watu wanunue tu kahawa. Zamani ilikuwa lazima kukiuzia walau kipindi kile kilikuwa kina maana kwakuwa kilikuwa kinawapa wakulima miche bora, kilikuwa kinasomesha watoto, kilikuwa kinajenga mashule.

Haya yote kwa sasa hakuna, yani KCU ni sawa na kampuni tu kama kampuni nyingine. Halafu mbaya zaidi niliona mkuu wa mkoa wa Kagera kwenye TV miezi kadhaa iliyopita akijinasibu kwa kuiagiza KCU iwalipe wakulima pesa yao ndani ya siku mbili.

Majaliwa mzee wa mashirika ya Umma iangalie KCU imeua zao la biashara Kagera, maana kwanza kahawa bei chini na kulipwa nako shida.
 
Kiufupi serikali inachangia pakubwa sana kuwadhoofisha wakulima, ila hapana shaka yote yatakwisha maadam mkombozi kaja,wanyonyaji na watu wasiojali maisha ya wengine kwa kuwa wao hawapati shida yatakomeshwa.
 
Lissu hatajenga barabara, shule wala zahanati maana hayo ni maendeleo ya vitu.

Atakachokifanya ni kuwafukuza wamachinga barabarani maana hayo ndiyo maendeleo ya watu.
 
CCM inataka Watanzania waendelee kuwa makapuku ili iendelee kuwakanya kichwani na kuwatukana.
 
Lisu hatajenga barabara, shule wala zahanati maana hayo ni maendeleo ya vitu
Atakachokifanya ni kuwafukuza wamachinga barabarani maana hayo ndiyo maendeleo ya watu
Unawaza kwa kutumia masaburi ndugu Etwege . Mada inasema kuhusu kahawa wewe umemtaja Lisu, huna akili kabisa mkuu
 
Kuna mambo mengine nchi hii yanashangaza na kusikitisha kweli.

Mtu kalima kahawa zake, kwa pesa zake na nguvu zake halafu unampangia amuuzie nani. KCU imekusanya kahawa za wakulima halafu huu karibu mwezi wa 3 hawajawalipa pesa yao.

Hiki chama cha ushirika hakina maana tena bora waache watu wanunue tu kahawa. Zamani ilikuwa lazima kukiuzia walau kipindi kile kilikuwa kina maana kwakuwa kilikuwa kinawapa wakulima miche bora, kilikuwa kinasomesha watoto, kilikuwa kinajenga mashule.

Haya yote kwa sasa hakuna, yani KCU ni sawa na kampuni tu kama kampuni nyingine. Halafu mbaya zaidi niliona mkuu wa mkoa wa Kagera kwenye TV miezi kadhaa iliyopita akijinasibu kwa kuiagiza KCU iwalipe wakulima pesa yao ndani ya siku mbili.

Majaliwa mzee wa mashirika ya Umma iangalie KCU imeua zao la biashara Kagera, maana kwanza kahawa bei chini na kulipwa nako shida.
Haya mambo hayafanywi kwa bahati mbaya,huu utaratibu wa kishenzi upo tangu miaka ya 90!,
Sasa hv ni kuwapa umaskini wakulima tu,na kuipa ccm pesa za bure.
Unajiuliza kwa nini wakulima wa kahawa,korosho,chai,pamba walazimishwe kuuza mazao yao kwa vyama vya ushirika,kwa nini be mtu asiuze anapotaka?

Maana Kama Mkulima ameendelea kuwa maskini Richa ya kuwepo vyama vya ushirika,Basi huo utaratibu ni mbovu
 
KNCU,SHIRECU,KCU,NYANZA zote baada ya kuonekana zina nguvu sana ya Kifedha miaka ile ilibidi waziue kimakusudi kabisa.

Kwa wasiojua hata scholarship ya Reg. Mengi kwenda kusoma ulaya miaka hio ilitoka KNCU,ukiona mpk chama cha ushirika kinaweza kupeleka watu kusoma ulaya tena miaka hio na bado kinafanya miradi kibao mingine ya kijamii ujue nguvu ya fedha ilikuwepo.

So hali ya umaskini wa wakulima walionao kupitia hivyo vyama vya ushirika sio hali ya bahati mbaya imetengenezwa kwa makusudi maalumu.
 
Lissu hatajenga barabara, shule wala zahanati maana hayo ni maendeleo ya vitu.

Atakachokifanya ni kuwafukuza wamachinga barabarani maana hayo ndiyo maendeleo ya watu.
We unaona kuwa machinga ni kitu cha maana.Yaani umezaliwa hapa duniani uje uwe machinga! Nchi itaendelea kwa kuwa na mamilioni ya vijana barabarani wakichuuza ? Hivi machinga wanazalisha nini kwa mfano?

Machinga ni kati ya kundi kubwa linalosababisha nchi za Afrika zisiendelee kwa sababu hakuna wanachozalisha, wanaitia serikalu hasara, hawana faida wanavuta Oxygen ya bure.
 
KNCU,SHIRECU,KCU,NYANZA zote baada ya kuonekana zina nguvu sana ya Kifedha miaka ile ilibidi waziue kimakusudi kabisa.

Kwa wasiojua hata scholarship ya Reg. Mengi kwenda kusoma ulaya miaka hio ilitoka KNCU,ukiona mpk chama cha ushirika kinaweza kupeleka watu kusoma ulaya tena miaka hio na bado kinafanya miradi kibao mingine ya kijamii ujue nguvu ya fedha ilikuwepo.

So hali ya umaskini wa wakulima walionao kupitia hivyo vyama vya ushirika sio hali ya bahati mbaya imetengenezwa kwa makusudi maalumu.
Mkuu pale shinyanga kuna shule inaitwa Buluba ilijengwa na SHIRECU kitambo lakini huwezi fananisha na vishule hivi vya kata.Vile vyama vingekuwa na nguvu nchi ingekuwa mbali sana.
 
KNCU,SHIRECU,KCU,NYANZA zote baada ya kuonekana zina nguvu sana ya Kifedha miaka ile ilibidi waziue kimakusudi kabisa.

Kwa wasiojua hata scholarship ya Reg. Mengi kwenda kusoma ulaya miaka hio ilitoka KNCU,ukiona mpk chama cha ushirika kinaweza kupeleka watu kusoma ulaya tena miaka hio na bado kinafanya miradi kibao mingine ya kijamii ujue nguvu ya fedha ilikuwepo.

So hali ya umaskini wa wakulima walionao kupitia hivyo vyama vya ushirika sio hali ya bahati mbaya imetengenezwa kwa makusudi maalumu.
Umegusa mahala pake, serikal iliingiza siasa na kuhakikisha vyama vyote vyenye pesa nyingi vinafilisika ili kuua uchumi wa wakulima na vyama vyenyewe

Wakat ule ilikuwa bei ni mbaya sokon, KNCU kwa mfano iliweza kuwapa bei nzur wakulima na mwaka unaofuata kama bei ikiwa nzur wanakata kidogo kidogo
 
Hivi wakulima wanalazinishwa kupanda kahawa,chai, pamba,tumbaku nk? Kwa nini wasihamie kulima mazao mengine ?

Tatizo sio serikali tatizo ni akili ya mkulima kupiga hesabu ya mapato na matumizi.Kama mapato Hamna si unaachana na hilo zao!

Elimu elimu,elimu.Waacheni hao wakulima waendelee kuvikopa vyama kwa kupangiwa bei, wanaupendo na hivyo vyama na hawana shida na hela.Tanzania's a imejaa fursa kwa nini ung'ang'anie zao moja tu.
 
Halafu huyo lisu hata kufanya kampeni bagamoyo na chalinze anatumia helkopta,hivi akipata Urais si ndio hatojenga bara bara atakuwa anapita juu kwa juu na kuacha mashimo ya barabarani bila mpango!
mtu anakuambia hayo ni maendeleo ya vitu si maendeleo hivi wanaojidai wanamuelewa sijui wanamuelewaje?mi simuelewi.5 tena kwa JPM na hizo kahawa hatutaki kang'omba (walanguzi wa kununua kwa bei ya chini) na kumnyonya mkulima.
Unawaza kwa kutumia masaburi ndugu Etwege . Mada inasema kuhusu kahawa wewe umemtaja Lisu, huna akili kabisa mkuu
 
Hivi wakulima wanalazinishwa kupanda kahawa,chai, pamba,tumbaku nk? Kwa nini wasihamie kulima mazao mengine ?
Tatizo sio serikali tatizo ni akili ya mkulima kupiga hesabu ya mapato na matumizi.Kama mapato Hamna si unaachana na hilo zao! Elimu elimu,elimu.Waacheni hao wakulima waendelee kuvikopa vyama kwa kupangiwa bei, wanaupendo na hivyo vyama na hawana shida na hela.Tanzania's a imejaa fursa kwa nini ung'ang'anie zao moja tu.
Mkuu iliwahi tokea wakulima wakataka kung'oa hayo mazao wapande mazao mengine kama retaliation juu ya wanachofanyiwa walitishiwa kukamatwa na kuwekwa ndani.
 
Na ndio maana unasikia kwenye vyombo vya habari wakulima wa Kahawa wanakamatwa wakiwa wanasafirisha na kufanya biashara ya Kahawa kimagendo na nchi jirani (Uganda) i.e wanapitisha njia ya panya

Sent from my D5322 using JamiiForums mobile app
Ni kweli waganda wanatoa bei zaidi ya KCU na mtu analipwa mara moja, KCU inachukua kwa bei rahisi na hailipi sijui wanauza ndo wanarudi kulipa maana ...
 
Kule Zanzibar hata ukikutwa umehifadhi karafuu kwenye ghala lako unaitwa tajiri kubwa.
Kule mtwara ukimuuzia kangomba korosho unaitwa tajiri kubwa na ukienda kuuza korosho lazima urudi nyumbani na mnunuzi aone shamba lako, bila kuliona hakupi pesa. Kule Mbeya ukilima mchele mwingi ujue utatuuzia watu wa Dar kwa Bei ya kutupa. Huwezi kuuza Uganda.
 
Hivi wakulima wanalazinishwa kupanda kahawa,chai, pamba,tumbaku nk? Kwa nini wasihamie kulima mazao mengine ?

Tatizo sio serikali tatizo ni akili ya mkulima kupiga hesabu ya mapato na matumizi.Kama mapato Hamna si unaachana na hilo zao!

Elimu elimu,elimu.Waacheni hao wakulima waendelee kuvikopa vyama kwa kupangiwa bei, wanaupendo na hivyo vyama na hawana shida na hela.Tanzania's a imejaa fursa kwa nini ung'ang'anie zao moja tu.
Kuna sehemu zingine hao wakulima wanalazimika kulima hayo mazao kutokana na ardhi yao kutokubali/ kutostawisha mazao mengine
 
Hivi wakulima wanalazinishwa kupanda kahawa,chai, pamba,tumbaku nk? Kwa nini wasihamie kulima mazao mengine ?

Tatizo sio serikali tatizo ni akili ya mkulima kupiga hesabu ya mapato na matumizi.Kama mapato Hamna si unaachana na hilo zao!

Elimu elimu,elimu.Waacheni hao wakulima waendelee kuvikopa vyama kwa kupangiwa bei, wanaupendo na hivyo vyama na hawana shida na hela.Tanzania's a imejaa fursa kwa nini ung'ang'anie zao moja tu.
Mkuu nilikua nakuheshimu sana. Mfano kwetu kunastawi mpunga tu. Unataka kuniambia kwasababu haturuhusiwi kuuza mpunga nje ya nchi nianze kulima chai?
Mkuu. Usirudie tena kuandika utumbo.
 
Halafu serikali hiyo hiyo ndo inatoa report na kusema Kagera ni maskini wakati waliikuta iko vzr kabla ya uhuru
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom