Kwanini Serikali isipunguze Matumizi ya Fedha za Kigeni ?

Kwanini Serikali isipunguze Matumizi ya Fedha za Kigeni ?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
17,572
Reaction score
27,406
Kama taifa kuhangaika kutafuta Pesa za wengine kwa uhai na mustakabali wa taifa letu ni kuwa tegemezi. Sina shida kabisa na watu binafsi / wafanyabiashara kutafuta hizi pesa kulingana na mahitaji yao na nini wanataka, hao siwapangii ila kuna matumizi yanayohitaji pesa hizi yasio ya lazima na hivyo kuweka rehani ustawi wa jamii yetu. Matumizi hayo ni kama ifuatavyo

Huduma za Matibabu za Watumishi wetu tunaowalipa, ili watutengenezee Huduma ila wao wanakwenda Nje kutibiwa
Sina tatizo kabisa na mtu binafsi hata akiamua achume pesa zake nchini na kuamua kabisa kuishi popote anapotaka. Lakini wale ambao tunawalipa na wanachukua kodi zetu ili wadumishe hospitali zetu lakini wao hawataki kutumia maboresho hayo, inaleta ukakasi. Watu hawa wakiwa katika utumishi wetu inabidi tuwalazimishe watumie huduma tunazotumia sisi hapa nchini; huenda kwa kufanya hivyo wataboresha... (what is Sauce for the Goose is Sauce for the Gander)

Miradi ya Ndani ambayo ingeweza kufanyika kwa Nguvu kazi za Ndani na bila kuhitaji Mikopo ya Aina yoyote ifanyike Ndani

Matibabu / Dawa ambazo tunaweza kutengeneza under license zitengenezwe ndani; Na zetu za Asilia tuziboreshe au kuzifanya kuwa Synthetic
Sasa hivi dawa nyingi ni forumulas ambazo zinajulikana na Kampuni za ndani zinaweza kutengeneza Dawa hizo cha kufanya zitengeneze kwa Brand name yao ambapo hii itapunguza uhitaji wa kununua madawa haya kutoka nje

Kupunguza Uagizaji wa Mafuta / Petroli
Kwa magari ya Serikali na kuwa lobby wenye malori na mabasi ya mikoani kuweza kufunga gesi asilia (CNG) ambayo tunayo nchini ili itumike.., na hili liende sambamba na kuongeza vituo za kujazia mafuta hasa mikoani ambapo mabasi ya abiria yanapita ili kuwe na uwezekano wa Gari kutoka point A mpaka B kwa kuweza kujaza njiani bila tatizo

Kuacha Kabisa kutegemea LPG katika Mapishi ya Nishati Safi kwa kuwa na Mbadala wa Umeme ambao tunazalisha na ni Bei Nafuu kwetu

Tuanzie Tulipo, Tufanye Tunachoweza na Tutumie Tulichonacho​
 
Unaongelea huuhuu umeme ambao hauwezi kufika Kagera/Kaskazini mpaka Tununue Uganda/Ethiopia
 
Unaongelea huuhuu umeme ambao hauwezi kufika Kagera/Kaskazini mpaka Tununue Uganda/Ethiopia
Hauwezi kufika au hatutaki kuufikisha; Kama ni bei rahisi kuuchukua Uganda kuufikisha Kagera basi tuuchukue Kagera after all mpaka daika hii hapo Kagera na vijiji vyote Unit moja ni 100 Tshs tofauti na mtungi wa gesi tunaogawa bure lakini kwa mtumiaji utakuwa kama Tshs 300/ kwa unit


Na hata kama haufiki au ni gharama issue ni kuhakikisha unafika na kupunguza gharama na sio kununua cha mwingine wakati tunaweza kuboresha chetu.. Yaani ni kama pipa lako la maji linavuja badala ya kuziba na kukinga mvua bure unanunua kila siku ndoo moja moja kutoka pipa la jirani yako (which costs more kwa siku moja tu kama ungeziba pipa lako)
 
Ukipunguza wewe inatosha
Mimi ni Serikali ? Au unajua maana ya Serikali ?

Moja mimi au mtu binafsi yoyote hakusanyi wala kulipwa Kodi; (Hivyo kumpangia mtu binafsi matumizi ya pesa zake itakuwa ni udikteta na kukosa busara)

Mbili; Serikali inakusanya Kodi kwahio hio Pesa sio yake ni ya sisi walipa Kodi ambao tuna Haki ya kuongelea Matumizi yake...
 
Mimi ni Serikali ? Au unajua maana ya Serikali ?

Moja mimi au mtu binafsi yoyote hakusanyi wala kulipwa Kodi; (Hivyo kumpangia mtu binafsi matumizi ya pesa zake itakuwa ni udikteta na kukosa busara)

Mbili; Serikali inakusanya Kodi kwahio hio Pesa sio yake ni ya sisi walipa Kodi ambao tuna Haki ya kuongelea Matumizi yake...
Mtajuana wenyewe
 
Mtajuana wenyewe
Ungefahamu kwamba kila ukinunua bidhaa au kutumia bidhaa unalipia Kodi indirectly; au hizo bidhaa zina bei hio kubwa sababu kuna kodi ndani yake au hata miamala..., basi ungejua hata wewe ni mwenyewe.... i.e. Pesa Serikali inayotumia au kukopa ni YAKO
 
Back
Top Bottom