Kwanini serikali isichapishe Pesa nyingi za kutosha? Gharama za kuchapisha Pesa Kwa nchi zipoje?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Habari za weekend!
Nipo hapa napata bia huku nikitafakari sana!
Nina maswali yananiijia kichwani sipati majibu; naombeni wataalamu mnitoe tongo tongo hapa!
1. Hivi kama serikali kuna wakati huwa inafikia kuomba msaada Wa pesa kutoka Kwa matajili, je kwanini isiwe inachapisha Pesa nyingi moja kwa moja za kutosha?
2. Katika kuchapisha Pesa serikali huangalia vigezo gani? Na je kuna gharama yeyote ambayo nchi hulipa ili kuchapisha Pesa?
3. Kitu gani kinatofautisha thamani ya Pesa kutoka taifa moja kwenda jingine? Yaani kitu gani kinaleta tofauti ya thaman ya shilling elfu moja ya Tanzania iwe tofauti na Kenya?
NOTE; mwenzenu zaman nilikuwa nazan B.O.T ni kama stoo ya Pesa, ambapo baada ya kuchapishwakuchapishwa nyingi nilijua huhifadhiwa pale!
 
yaani pesa inatolewa ili upewe pesa
kuna campani moja ya kutengeneza pesa ina tawi Kenya
garama ya kutengeneza pesa inayatofautiana kutokana na quality ya Karatasi
huwezi chapisha pesa nyingi maana watu wataacha fanya kazi kwa bidii
ni hayo tu kwa uchache
 
kuchapisha pesa nyingi kuta sababisa mfumuko wa bei(inflation) hivyo itapelekea kuongezeka kwa bei ya bidhaaa n.k
 
Habari za weekend!
Nipo hapa napata bia huku nikitafakari sana!
Nina maswali yananiijia kichwani sipati majibu; naombeni wataalamu mnitoe tongo tongo hapa!
1. Hivi kama serikali kuna wakati huwa inafikia kuomba msaada Wa pesa kutoka Kwa matajili, je kwanini isiwe inachapisha Pesa nyingi moja kwa moja za kutosha?
2. Katika kuchapisha Pesa serikali huangalia vigezo gani? Na je kuna gharama yeyote ambayo nchi hulipa ili kuchapisha Pesa?
3. Kitu gani kinatofautisha thamani ya Pesa kutoka taifa moja kwenda jingine? Yaani kitu gani kinaleta tofauti ya thaman ya shilling elfu moja ya Tanzania iwe tofauti na Kenya?
NOTE; mwenzenu zaman nilikuwa nazan B.O.T ni kama stoo ya Pesa, ambapo baada ya kuchapishwakuchapishwa nyingi nilijua huhifadhiwa pale!
Soma economics kijana utaelewa aya mambo
 
yaani pesa inatolewa ili upewe pesa
kuna campani moja ya kutengeneza pesa ina tawi Kenya
garama ya kutengeneza pesa inayatofautiana kutokana na quality ya Karatasi
huwezi chapisha pesa nyingi maana watu wataacha fanya kazi kwa bidii
ni hayo tu kwa uchache
Wataachaje mkuu wakati kama sahiv watu wanafanya kazi Kwa mkopo? Zikiwepo si ni bora zaidi?
 
“Kama kutakuwa na makundi mawili, badala ya kuwa benki na jamii, iwe mwana jamii mmoja na mwingine, wasingeweza kuendesha mfumo wa ukopeshaji kwa kanuni nyepesi tu, kwamba, mkopeshaji hawezi kukopesha kile asicho kuwa nacho, kama sinavyo fanya benki. Ni benki za biashara tu na taasisi zingine za fedha ndizo zinazo weza kukopesha pesa hewa wanazo zatengeneza kwa kukopesha.”
Profesa Irving Fisher, mwanauchumi kwenye kitabu chake 100% Money
“Nipe nguvu ya kutawala sarafu ya nchi na sitajali ni nani anaye tunga sheria”
Amschel Rothschild
“Somo linalo husiana na mambo ya fedha, kwenye nyanja zote za masomo ya uchumi, ndilo somo ambalo ugumu utatiwa au kutumiwa kwa makusudi ili kuficha au kupoteza ukweli (kuhusiana na suala zima la fedha)”
John Kenneth Galbraith, Mwanauchumi na Mwandishi.
“Suala ambalo limefanyiza ubaya kwa karne, na ambalo itabidi lipiganiwe ili liondolewe, punde tu au baadaye kidogo, ni wananchi dhidi ya taasisi za fedha (benki)”
Lord Acton (1834-1902, Mwanahistoria wa England
Pesa inatoka wapi?
Hili linaweza kuwa swali la mwaka.
Na hakuna wa kulijibu, siyo mwanauchumi wala mfanyabiashara, wala huwezi kulipata jibu lake kwenye machapisho na majarida ya kiuchumi, wala siyo la kiserikali, wala kwenye vipindi maalum vya kiuchumi kwenye luninga yako, mbadala wa wapi lipo jibu la swali hilo lazima upatikane, na ashakum siyo matusi.
Katika moja ya vitu ambavyo vimetawala au kuendesha maisha yetu ya kila siku ni; Pesa.
Pesa ni nini, au inatoka wapi, ni swali jepesi, lenye majibu mepesi ambayo kwa namna moja ama nyingine, huwa hakuna anayejitolea kuyajibu, ni kama vile pesa yenyewe kupitia utaratibu wa kuitumia au inavyo tumika inatoa jibu la maswali hayo, inajijibu yenyewe, tunaona kwenye luninga, kwenye matangazo ya biashara, kwenye vitabu vikubwa vilivyo vunja rekodi za mauzo na filamu, maswali haya huwa yanajijibu yenyewe huko. Kutokana na majibu hayo ni kuwa, watu wengi unaondoka na majibu ya kuamini kuwa pesa zinatengenezwa na serikali.
Kwamba serikali ndiyo inayo printi noti za fedha na sarafu zake. Kwamba serikali ndiyo inayo printi sarafu na noti ni kweli kabisa, ila huo siyo ukweli wote.
Ukweli wote ni upi?
Benki, huo ndiyo ukweli wote.
Tuashumu kuwa benki inakopesha fedha ilizo pewa kama amana na wateja wake, ingawa huo siyo ukweli, tunaashumu tu. Unapo kwenda benki kuchukua mkopo, benki inakupa mkopo huo baada ya kusaini mkataba ambao utakutaka wewe kulipa fedha hizo na riba juu.
Dhamana ya ahadi hiyo, ambayo ni maarufu kama, ‘dhamana ya mkopo’ huwa ni mali zisizo hamishika au zinazo hamishika ambazo zinamilikiwa kihalali na mkopaji au na mdhamini wa mkopaji. Kisha kama wanavyo fanya wana mazingaombwe, benki wanageuza mkataba huo baina yao na mkopaji kuwa ndiyo fedha anazo pewa mkopaji. Ndiyo kama mazingaombwe vile, huwezi kuja kwangu, tukaandikishana mkataba wa kukopeshana, nami nikaugeuza mkataba huo kuwa ni fedha unazo taka, ila benki inafanya maajabu hayo kila siku, ila macho yetu hayaoni.
Huwezi kuamini, ila huu ndiyo ukweli kuhusu namna benki zinavyo fanya kazi.
Vitu hueleweka zaidi kwa mifano, ngoja ni kupe kahadithi kidogo kama mfano wa namna ambavyo benki wanavyo fanya hayo mazingaombwe.
Hapo zamani za kale, kila kitu kilitumika kama fedha, ili mradi kiwe kinabebeka na watu wawe na imani kuwa kinaweza kubadilishwa na kingine chenye thamani kama yake. Hivyo mazao, mifugo, na bidhaa nyinginezo zilitumika kama pesa. Vitu vya thamani kama vile dhahabu na fedha vilivutia zaidi kwenye hili, navyo vilitumika katika biashara hii, iliitwa Barter Trade.
Mtu mmoja ambaye hapa tutamuita Sonara, kutokana na kazi yake ya kuyeyusha hivi vito vya thamani na kuviweka katika maumbo mbalimbali, yeye alikuja na wazo, kutokana na kwamba biashara yetu ya kubadilishana vitu inakumbana na kikwazo cha ‘thamani’ na inakuwa ni vigumu wakati mwingine haki kufanyika katika aina hii ya biashara ni vigumu kwa sababu hakuna kipimo maalum cha ‘thamani’ kwa bidhaa zote, Sonara akapendekeza jamii imruhusu atumie kipaji chake atengeneze sarafu za fedha na dhahabu ambazo zitatumika kama kipimo cha thamani kwa bidhaa mbalimbali.
Bidhaa ambazo upatikanaji wake ulihitaji nguvu na shughuli nzito basi thamani ya bidhaa hiyo itakuwa kubwa kuliko ile ambayo uzalishaji wake haukuhitaji nguvu na akili nyingi. Sonara akapewa mikoba na kuanza kutengeneza sarafu za fedha na dhahabu.
Sonara akatengeneza chumba maalum chenye mlango mkubwa na mzito, na huko akazimimina sarafu zake za fedha na dhahabu na akaweka walinzi juu kuhakikisha hakuna anaye cheza na ‘mayai’ yake. Watu nao wakalipenda wazo la Sonara, wakaleta fedha na dhahabu zao kwa wingi zihifadhiwe na Sonara, naye akiwachaji malipo kidogo kwa huduma hiyo.
Sonara akapata wasiwasi, endapo watu wote watakuja kuchukua dhahabu na fedha zao, yeye atabaki na kitu gani?
Sonara akatengeneza risiti, kwa wale wanao leta dhahabu na fedha kwake, risiti hizo zilibeba thamani ya dhahabu au fedha zilizo hifadhiwa na muhusika. Risiti hizo zikawa zinaweza kutumika mbadala wa fedha na dhahabu, yaani ukiwa na risiti hizo ni sawa na kumiliki kiasi cha dhahabu au fedha kilicho andikwa kwenye risiti hizo. Na kama ukipenda unaweza ukarudi kwa Sonara na risiti hizo na Sonara akakupa dhahabu au fedha halisi, hii itategemea na thamani iliyo andikwa kwenye risiti hiyo.
 
Back
Top Bottom