Kwanini Serikali inamwogopa Lissu?

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,233
2,000
Vijana wote wa CCM wamejazana humu kila kukicha wanaanzisha Topic za kumkashifu na kumsimanga Tundu Lissu, mtu asiye na hatia aliyepigwa risasi zaidi ya 10 na watu wanaoitwa "wasiojulikana " zilifyatuliwa risasi 38,kumi ndo zikampata.

Dada yangu Faizafox aliweka uzi humu wenye kuonyesha ni kiasi gani aliguswa na kushangazwa na tukio hilo japokuwa naye ni CCM member, dada huyu anadai hakutarajia Kama Tanzania anayoijua imefikia hapa.

Serikali ilikana kuhusika na tukio hilo, lakini serikali hiyo hiyo imejaa hofu juu ya huyu mtu.

Nilishangaa Sana, Balozi tena anayeiwakilisha nchi Ktk taifa kubwa kusigina kwenye Media na mtu aliyeonewa, serikali inadai kuchafuliwa na Tundu Lissu kimataifa.

Ukisikiliza mahojiano ya Tundu Lissu na international media hakuna sehemu yoyote anakoichafua serikali zaidi ya kulalamika Kwanini serikali haijawakamata wasiojulikana?

Eti hadi Dereva awepo, ina maana Kama Dereva angeuawa uchunguzi ungefungwa? mbona ni hoja ya kitoto Sana kutolewa na Jamhuri ?

Inanishangaza Sana ndugu zangu Mods kufumbia macho Topic zinazomwandama Tundu Lissu kwa kila aina ya kashfa.

Ni hao hao Vijana wa CCM waliojazana humu walifurahia sana wakati muasisi wa JF Maxence Melo alipokuwa akisota Segerea kwa kukataa kuwapa Police majina ya wakosoaji wa serikali.

Na leo hao hao wamejaza Topic kibao humu za kumkashifu Tundu Lissu na bado wanadunda JF.

Ule msemo "The guilty are always afraid " una jenga maana kubwa mno juu ya uoga wa serikali kwa Tundu Lissu.

Badala ya kuwatafuta watuhumiwa Serikali inatafuta wahanga wa tukio.

Asante Mungu Dereva Yupo Belgium, Taarifa za uhakika nilizonazo endapo Dereva angeenda kuhojiwa ni kwamba kibao kingemgeukia yeye, sasa hivi angekuwa Segerea, ni Kwanini?
Lengo la washambuliaji ilikuwa ni lazima na Dereva afe.

Bahati mbaya mno kwao, Dereva aliwaona na kuwatambua baadhi, kuna mmoja wao aliwahi kuonana na Dereva huyo Ktk Bar moja (jina limefichwa) jijini Dar.

Kwamba hawahusiki, na hawa wajui wahusika ila wanaogopa hadi kivuli cha Lissu.

Mwaka jana nikiwa Australia, rafiki yangu Ross aliniuliza, "vp endapo angeshambuliwa waziri, je? Watuhumiwa wasingekamatwa? " Nilimwambia jibu analo.

Mbaya zaidi makosa waliyofanya bado hawataki kukoma wanapanga makosa mengine tena zaidi ya haya, mtakuja kuyaona.
Niishie hapa.Sent using Jamii Forums mobile app
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,725
2,000
Niweke vizuri, ccm na serikali hawamwogopi Lissu bali wanamchukia. Wanamchukia maana ana uwezo wa kujenga hoja na ushawishi kuliko mwenyekiti wao. Kibaya zaidi anaweka maovu yao hadharani hapo ndio wanaingia wazimu.
 

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
7,034
2,000
Niweke vizuri, ccm na serikali hawamwogopi Lissu bali wanamchukia. Wanamchukia maana ana uwezo wa kujenga hoja na ushawishi kuliko mwenyekiti wao. Kibaya zaidi anaweka maovu yao hadharani hapo ndio wanaingia wazimu.
Uovu mbaya kuliko wote upo ndani ya chagadema, sema ndo hivyo, kivuli chenu cha kujikimu kimaisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,295
2,000
Niweke vizuri, ccm na serikali hawamwogopi Lissu bali wanamchukia. Wanamchukia maana ana uwezo wa kujenga hoja na ushawishi kuliko mwenyekiti wao. Kibaya zaidi anaweka maovu yao hadharani hapo ndio wanaingia wazimu.
Kingine ni kwamba anaongea kiingereza kizuri bila shaka
 

sikongefdc

JF-Expert Member
Oct 18, 2017
1,236
2,000
Vijana fanyeni kazi, yani serikali ( mhimili wenye jeshi, mamlaka umuogope muhuni mmoja mnyoa kiduku?). Kuliko taifa litumbukie kwenye machafuko ni bora huyo ms.e,ngerema atangulie yeye ili kulinda wananchi safi wasio na hatia. God bless Africa, God bless Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom