kwanini SANDA

Rjohn

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Posts
613
Reaction score
130
Mambo vp chitchat User?
leo napenda tujuzane kidogo kwanini sis binadamu tukifa huvishwa nguo maalu ijulikanayo kama SANDA?
je kuna ulazima mtu kuzikiwa hyo ama vp kifupi mwenye historia ya hilo vazi anifungue
 
ha ha ha ha! sidhani kama humu ndani kuna mtu aliyewahi kufa...
 
vipi mkuu safari ndio imewadia ama?
 
Mambo vp chitchat User?
leo napenda tujuzane kidogo kwanini sis binadamu tukifa huvishwa nguo maalu ijulikanayo kama SANDA?
je kuna ulazima mtu kuzikiwa hyo ama vp kifupi mwenye historia ya hilo vazi anifungue

Hivi siku hizi marehemu huvalishwa sanda??? Mbona huwa naona wanavalishwa nguo nzuuuri?? Wengine huvalishwa Shela zao, suti zao, ama nguo nzuri walizokuwa wanazipenda?????
 
dooo kuna meng duniani
 
Swali juu ya swali,je lazima sanda iwe nyeupe?
 
Jamani,any updates kwa mnaojua? MziziMkavu kuna sababu zozote kisayansi?
Kwa walio Waislam snochet

Ni wajibu kumvika sanda nzuri maiti, au thamani ya sanda itokane na mali ya maiti, ndugu zake, jamaa zake, na isiwe sanda ya thamani kubwa, na avikwe maiti sanda hiyo kwa utaratibu alofundisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم bila kuzidisha chochote, na amesema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم“Mmoja wenu anapomvika sanda ndugu yake, basi amvike sanda iliyo nzuri akiweza.” [Muslim, Abu Daawuud, na Ahmad]. Na makusudio ya sanda nzuri ni ile sanda ilio safi na yenye kutosha kumsitiri maiti mwili wake wote, na sio kufanya israfu katika sanda kwa kununua sanda ya thamani kubwa kama alivyofafanua Imaam ‘Abdullaah bin Mubaarak.

· Endapo maiti huyo hakuwa na uwezo wa kuwa na sanda basi jamaa zake wenye kuhusiana naye watakuwa na wajibu wa kuandaa sanda kwa ajili yake. Nao ni watu wake kama baba yake, babu, mwanae wa kiume au mtoto wa mwanae (mjukuu). Na endapo wote hao watashindwa au atakuwa hana jamaa, basi litakuwa jukumu la ‘Baytul Maal’, yaani litatolewa fungu kutoka katika hazina ya Waislam kama ipo, na kama haipo basi litakuwa jukumu la Muislam yeyote aifahamuye hali ya huyo maiti.

· Kinachopasa kumkafini maiti ni nguo itakayomsitiri mwili mzima.

· Sanda inapendeza iwe nyeupe kwa Hadiyth isemayo: “Vaeni nguo nyeupe kwani ni vazi bora katika mavazi yenu, na mkafiniane kwazo” [Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, na Ibn Maajah kaisahihisha].

· Vipande hivyo vya sanda hutiwa harufu nzuri ya aina ya ubani uliosagwa, kisha hukunjwa moja juu ya nyingine na pia hutiwa kwenye sanda hiyo ‘Hanuut’ aina ya unga wenye harufu nzuri ambayo ni maalum kwa maiti na kisha baada ya hapo maiti hulazwa juu ya hiyo sanda iliyotiwa vitu hivyo, na hulazwa chale.

· Ukubwa wa shuka hizo za sanda unatakiwa uzidi kimo cha maiti kutegemea na urefu na upana wa maiti. Kuongezwe futi mbili kuzidi kile kimo cha maiti, kwa mfano kama maiti ana urefu wa futi sita, basi urefu wa shuka uwe futi nane na upana uwe futi sita ili stara iwe nzuri zaidi.

· Baada ya kutandikwa sanda, maiti atalazwa juu yake akiwa amefunikwa sehemu zake za siri; juu ya kitovu hadi chini ya magoti yake. Itachukuliwa ncha ya upande wa kulia na iletwe hadi kifuani mwake, na ncha ya kushoto itafanywa hivyo hivyo, akishafunikwa na sanda hizo wakati huo huo itachomolewa ile shuka au taulo aliyokuwa amesitiriwa nayo sehemu zake za siri. Utaratibu huo utafuatwa kwa shuka ya pili na ya tatu. Kisha sanda hiyo husokotwa mwisho wake na kuanza kufungwa ili isije ikaachia sehemu yeyote na kulegea; husokotwa ncha ya hivyo vipande vya sanda upande wa kichwani na miguuni na kufungwa kwa kamba zilizotayarishwa. Na hufungwa nchani na katikati ya mwili hizo kamba kuweka himaya tu sanda zisiachie na kufunuka maiti, bila kukazwa kamba hizo. Na anawezwa maiti kufungwa mafundo matatu hadi saba kulingana na uimara na mahitajio.

· Mpaka hapa, maiti itakuwa tayari kwa ajili ya kutekelezewa jambo la tatu ambalo ni kuswaliwa.

· Maiti ikishafikishwa kaburini na kuingizwa kwenye mwanandani, zinaweza kamba hizo kufunguliwa au kuachwa hakuna neno.

· Kukikosekana vitambaa kama ilivyotajwa juu, huruhusiwa kumkafini maiti kwa vazi la kawaida kama shuka ya chini (kikoi) na nguo ya juu kama kanzu au shati ila ni bora zaidi kutumia mfumo uliotajwa mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…