Vyombo duni ziwani vinaweza vuna mazao mengi sana. Jiulile boat ya kivuvi ya juu kabisa ziwa vic inagharimu chini ya 15 milion hivyo wamejikuta wawekezaji huku ni wengi kuliko baharini. Na kujikuta mazao ya huku yanakuwa mengi na kufanya bei ishuke kuliko wa baharini. Kitu cha pili ni uhamaji wa watu kutoka bara kwenda pwani. Mtu anatoka bara akiwa kazoea chakula chake na kuhamia pwani hivyo muuzaji anampelekea hukohuko na ananunua ila wanaotoka pwani ni wachache sana kuja bara hivyo muuzaji anakuwa hana uhakika na wanunuzi wa mzigo wake
Unaweza ukawa kweli ila hizi habari huwa siziamini na huwa nazifuatilia google huwa sipati iliyokamiliIgombe fisherman nyumbani Mwanza nilikua nauza samaki wa kukaanga akaja mzee fulani akakuta nina sato wengi na pia sangara,akasema nimfungie sato ila akasema kama wangekua ni wa moto angependa wa kutafuna pale pale,nikamwambia zunguka huko nyuma mama anakaanga ukachukue waliotoka motoni kabisa.
Baada ya kwenda akasema basi amehairisha maana apendi sato waliokaangiwa mafuta ya sangara kwakua hao sangara waliletwa ziwa victoria yeye angali kijana.Hivyo akachukua tu sato wabichi ambao wataenda kumkaangia nyumbani kwake.Pia humu kuna uzi nilishawahi uona unazungumzia hichi kitu
Nadhani watu wanazungumzia habari ya vifaranga wa Sangara wanaowekwa kwenye ponds au vitalu maeneo ya ziwani.Unaweza ukawa kweli ila hizi habari huwa siziamini na huwa nazifuatilia google huwa sipati iliyokamili
Pole sana mzee, hivyo pia kwa mtu wa pwani samaki wa maji baridi hawapendi, maana wengine wanashombo ile mbaya.Samaki wa baharini- hawafai kuliwa kwa mtu mwenye ubongo timamu.
Radha yao mbaya
Sio watamu
Mwiko kula hawo wadudu
Kambale ukimla leo nyumba mzima shombo lake tu kesho.Sasa hawa hawawafikii vitoga, mboju, kambale, ningu,mbete, furu, kamongo n.k.
Hapo kwenye ningu na nembe a.k.a matusi ya mwanza umenikumbusha nyumbani kabisaaKanda ya Ziwa pia kuna aina nyng za samak kuna ningu, nembe ila wanaishia huko huko kwann sangara na sato?
Mm nafikir kwasababu ya ladha na kuwa na kuwa na nyama nyngi
Hayo ya shombo yanasababishwa na usafi na usafishaji wa muhusika binafsi. Kiuhakika harufu ya kambale inasisimua hamu akipikwa vyema.Kambale ukimla leo nyumba mzima shombo lake tu kesho.
Kuna mtaalam mmoja wa mambo ya samaki aliniambia kuna fursa ya kufuga samaki wa bahari pembeni ya bahari sema wabongo hatujaichangamkia hii fursa ngoja nimtafute niweke maduka yangu ya samaki songea mbeya dodoma na iringa kwa kuanzia
ntafanya huu mradi hela yangu ya kustaafiaHesabu za kwenye karatasi ni nzuri sana.
Ladha ya samaki wa maji ya chumvi ni hafifu, sokoni huwezi ipambanisha na wa maji baridi. Wangekuwa na soko wafanya biashara wangechangamkia hiyo fursa.Samaki wa baharini- hawafai kuliwa kwa mtu mwenye ubongo timamu.
Radha yao mbaya
Sio watamu
Mwiko kula hawo wadudu
Kabla ya kuanzisha kwa Sheria za Deep Sea fishing regulations ya 2005 inatakiwa upate kibali cha DG wa uvuvi, Kisha wajue sehemu utakayotengeneza aqua culture hiyo ya kufuga samaki, pasiwe eneo la shughuli za kibinadamu,mkondo au njia ya vyombo vya majini. Kisha afisa uvuvi atajua mradi na atapita kukagua mara Kwa mara. Ukimalizana na vibali kazi ni kwako, Ziwa Victoria nimeona wanafanya hii kitu ila baharini bado sijaona.ntafanya huu mradi hela yangu ya kustaafia
Kuna samaki wengine wanapatikana Ukerewe wanaitwa Ngere. Ni watamu hatari.Sasa hawa hawawafikii vitoga, mboju, kambale, ningu,mbete, furu, kamongo n.k.
😂😂Katiba mpya itamke bayana bila kificho kuwa samaki wa baharini wafikishwe bara pia.
sangara ni samki wa kuletwa sio asili wala sio mtamu mkuu.Ukweli ni kwamba watu wa bara wengi ni antagonistic kutumia bidhaa za bahari. Msukuma ale papa, nguru, taa, tasi? Wao watakwambia wamezoea sato na kidogo sangara.
Kuna msukuma mmoja tulikua tunafanya naye kazi tulikaa pale hotel ya Peacock nikamzoesha kula changu ndio akaanza kuwaelewa samaki wa baharini.
Na hata huko kwao Mwanza utasikia sato....sangara hawawapendi. Ila kimsingi sangara ana mnofu sana. Napenda sangara kuliko sato