Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
Raisi Magufuli ni mwenyekiti wa SADC, kwa muktadha huo ni kiongozi mkubwa katika ukanda huu wa kusini mwa Afrika.
Leo nchi ya Zimbabwe imepata msiba wa kufiwa na muasisi wa Taifa huru la Zimbabwe, Je ni kitu gani kimemfanya raisi Magufuli ambaye ni mwenhekiti wa SADC asiende kwenye msiba wa mpigania uhuru huyo?
Majuzi rais mstaafu mzee Mwinyi alitueleza kuwa wakati yeye akiingia madarakani nchi yetu ilikuwa na uhaba mkubwa mno wa fedha za kigeni na hali ilikuwa mbaya sana lakini serikali ya Mugabe ilitusaidia sana kwenye wakati huo wa shida. Je si ingekuwa vizuri raisi wetu japo kukumbuka uhusiano huu mzuri kwa kushiriki msiba wa kiongozi huyu mpigania uhuru?
Wakati wa kifo cha baba wa Taifa, Mugabe alikuja msibani kulia nasi na kutupa pole Watanzania, kwa nini sisi raisi wetu hajaenda kwenye msiba huu mzito?
Wakati wa uongozi wa Mugabe kama rais wa AU, alishiriki kikamilifu katika kuutambulisha mchango wa Tanzania kwenye harakati za Ukombozi wa Afrika, ni yeye aliyeendesha kampeni ya kuuita ukumbi mmoja wa mikutano wa AU kwa jina la Nyerere. Hii ni baada ya kizazi hiki kuanza kusahau mchango wa mwalimu katika liberation.
Je kwa nini raisi Magufuli Personally kwa niaba ya Watanzania hajaenda kuhani msiba?
Tunajua yupo makamu wa raisi, lakini Makamu wa Raisi siyo Raisi. Na hata nchi nyingine zenye maraisi nazo zina makamo wa raisi pia, lakini je kwa nini wameenda maraisi wenyewe na siyo makamu wao?.