Kwanini Rais anawalazimisha wafanyabiashara kupandisha nauli za usafiri? Mafuta yameanza kupanda mwaka huu? Rais hajui kuna LATRA na SUMATRA?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,209
42,071
Kimsingi ni wiki ya pili sasa Rais Samia kupitia hotuba yake amekuwa akisisitiza kuwa bidhaa lazima zitapanda na nauli zitapanda kutokana na vita ya Urusi!

Ukweli ni kwamba vita ya Urusi na Ukraine kama ina muda mrefu basi ni mwezi na bidhaa karibu zote zimepanda ni mwaka sasa yani toka mwaka jana bidhaa karibu zote ziko juu!

Rais anasema na nauli lazima zitapanda na ukweli ni kwamba wapandisha nauli na washusha nauli ni Latra ambao kwakweli wamekuwa wakidhibiti kupanda holela kwa nauli hata kama mafuta yakipanda!

Kama swala la kupanda bei ya mafuta lingekuwa linapandisha nauli za usafiri basi ingekuwa balaa maana kila mwezi sumatra hutangaza bei mpya za mafuta na nauli hazijawai kupanda!

Sasa ninachojiuliza kwanini Rais ana walazimisha sumatra na Latra kupandisha nauli kwa kauli zake? Sasa kwa mwendo huu Sumatra na latra wanawezaje kuwazuia au kuwadhibiti wafanyabiashara kupandisha nauli za usafiri ikiwa Rais tunayemtarajia yeye ndio ana hamasisha wafanyabiashara kupandisha bei za mafuta?

Rais kwanini hataki kukaa kimya au kushauriwa kutoingilia mambo ambayo kimsingi hayafahamu vyema na yana haribu sana uchumi na yatawaumiza wananchi!
 
Yeye ndiye mpiga debe wa kupandisha bei bidhaa mbalimbali, mama wa ajabu sana huyu!

IMG_0754.jpg
 
Hiyo ndiyo rangi yao halisi viongozi wetu hao wanaona kila nyanja wao ndiyo wataalam.

Kipindi Covid inatukokota sikuna ugonjwa ulizuka mbeya dokta akatoa ripoti waziri wa afya akamvua wadhifa alokuwa nao

Wao kila kitu ni blaablaa tuu hawakai chini kufikiria chakufanyaa
 
Hatuna rais kwa sas namuombea lolote limpate cjawai ona rais wa HV hat mam angu amemzid vingi San.

Mtu unatokea hadharani kutamka upupuu kweli.

Latra na sumtara wametuzaidia San kuzibit Bei za nauli Kaz wamefanya anatokea mtu ajaui inflation issue anatamaka upupu na watu wanashangiliaa.

Mam unaupiga mwingi balaaa
 
Back
Top Bottom