DaveSave
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 440
- 645
LIMEULIZWA swali katika group moja la WhatsApp ambalo nimo, nimelijibu kule ila kwa faida ya wengi, nalitolea ufafanuzi na hapa.
Swali ni kwa nini Rais ambaye ni Mkuu wa Serikali anapewa hadhi kubwa ndani ya Bunge ambao ni mhimili mwingine, lakini Jaji Mkuu hapewi wakati ni kiongozi wa Mahakama?
Najibu; Tanzania inafuata mfumo wa Semi Presidential Model of Government (mimi huwa naita Nusu Urais).
Rais ni Mkuu wa Serikali lakini sio mtendaji wa Serikali. Mtendaji ni Waziri Mkuu.
Ukichukua tafsiri hiyo ya Rais kuwa Mkuu wa Serikali, utakuwa sahihi kuona mkanganyiko huo. Why Bosi wa Serikali (mhimili wa utendaji) aingie ndani ya Supreme Organ (Bunge, mhimili wa sauti na matakwa ya wananchi) na kupewa hadhi kubwa?
Nimesema Tanzania ni Semi Presidential System. Rais ni Mkuu wa Serikali ila sio mtendaji. Kubwa zaidi ni kuwa Rais ni Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu.
Sasa, hadhi anayopewa Rais bungeni sio ya ukuu wa Serikali, bali ni Mkuu wa Nchi.
Ndio maana ukienda bungeni, utakuta picha ya Rais Magufuli juu ya Ndugai. Ni kwa sababu Magufuli pale yupo kama Mkuu wa Nchi.
Mahakamani picha ya Rais Magufuli ipo. Ni kama Mkuu wa Nchi, sio Mkuu wa Serikali.
Katika nchi zenye kufuata Parliamentary Democracy, kisha mamlaka ya Mkuu wa Nchi na Mkuu wa Serikali yametenganishwa, huwezi kuona huo mkanganyiko.
UK, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu ni Malkia/Mfalme. Mkuu wa Serikali ni Waziri Mkuu.
Ndio maana huwezi kukuta picha ya Waziri Mkuu mahakamani UK wala ndani ya Bunge. Ni Malkia/Mfalme.
Unaweza kuwa na Parliamentary System na bado kukawa na muingiliano. Ni kama Afrika Kusini. Wao wana Parliamentary Model of Government, lakini Rais ndiye Mkuu wa Serikali na ndiye Mkuu wa Nchi.
Binafsi napenda Parliamentary Model of Government yenye kutenganisha mamlaka ya Mkuu wa Nchi na Mkuu wa Serikali.
Hata BBI Kenya wamependekeza kuwa na Parliamentary System ili kuachana na Presidential System (Mfumo wa Urais) ambao wapo nao.
Presidential System ni mfumo kama wa Marekani. Kinachowabeba wale ni uimara wa taasisi zao za kibunge (Congress), Baraza la Wawakilishi na Seneti.
Presidential System Rais anakuwa Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu, Mkuu wa Serikali, Mtendaji Mkuu wa Serikali, maana hana hata Waziri Mkuu.
Nimeshaliandika mara nyingi kwenye akaunti zangu Facebook na makala zangu gazetini Mwananchi. Nadhani wengi hawasomi au wanasahau.
Binafsi naamini kuwa hata mgogoro wa Muungano na vilio vya Wazanzibari, suluhu yake ni nchi kuwa na Parliamentary System yenye kutenganisha kofia ya Mkuu wa Nchi na Mkuu wa Serikali.
Wala hatuhitaji Serikali Tatu zilizoleta mgogoro na kusababisha hasara ya Bunge la Katiba 2014.
Nchi inahitaji Serikali mbili lakini chini ya Parliamentary System.
Serikali ya Tanganyika yenye Waziri Mkuu wake ambaye ndiye Mkuu wa Serikali na Mtendaji Mkuu wa Serikali. Kisha Serikali ya Zanzibar yenye Waziri Mkuu.
Serikali Tanganyika inafanya kazi yake ya kuhudumia Tanganyika. Serikali ya Zanzibar inahudumia Zanzibar bila kuingiliana. Kila Serikali inakuwa huru.
Halafu tunakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye hatakuwa Mkuu wa Serikali, bali Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu.
Rais hatakuwa na sauti kwenye Serikali yoyote, bali anasimama kama kiungo wa Muungano, mlinzi wa nchi na usalama. Atakuwa na mamlaka ya kuvunja Bunge, kama mkuu wa nchi.
Ndimi Luqman MALOTO