Mkuu chuo kinasaidia sana, thugh we cant rule out effort za mtu binafsi...mfano wa chuo ni katika uwezo wake wa kusimamia mwanafunzi katika taaluma. Hii unaweza hata kuona katika dissertation, mfano dissertation za law nyingi za Tumani, ukiziangalia wanafunzi wanakopiana dissertation hizohizo....wakati pale Mlimani faculty of law its not the case.
Nakubaliana na wewe ila si mia kwa mia. Utambue kuna vipanga vile vile wamesoma DIT, Mzumbe, Nyegezi na IFM pamoja na kwamba vyuo hivyo admission requirements zilikuwa si tight sana. Si kila mtu aliingia vyuo hivyo kwa credits za chini, ila aliingia kwa vile vyuo hivyo vilikuwa vinatoa fani anayoitafuta. Kuna suala la application pia kupotea pale mlimani, au kuchelewa kuomba, wengine wa mikoani hasa nyakati za nyuma , sasa mtu hawezi akakaa anasubiri wakati miaka inaenda. Kuna watu waliingia na
one nzuri za combination ngumu katika vyuo hivyo nilivyotolea mfano, na kuna watu waliingia na 2 au 3 za
combination rahisi pale mlimani na waka-graduate. Sasa haya mambo ni ya kuangalia kwa marefu zaidi, hatuwezi kuwa generic tu. Kuna watu wanasomea kupata maisha na kuna watu wanatafuta sifa ili wakatangaze kijijini kuwa walifika chuo kikuu na watu wamekwenda na maji kwa mtindo huo. Mtu anakwenda mlimani kusomea kitu ambacho hakilipi mtaani, matokeo yake anakaa hana kazi miaka 3 na anakuwa frustrated na kuanza kunywa gongo halafu chali! Sasa haya mambo ni ya kuangalia, cha muhimu ni kuona mbele! At the end bao la maisha ndio lina-matter! Moreover, kipanga wa
one (combination ngumu) ya enzi za Mwalimu ni kipanga tu, hata mkienda kazini, yuko likely kujifunza haraka hata kama alisomea chuo kibovu as long as ana cheti kinachostahili! After all haya mambo ya bussiness studies na humanities, si masomo mahumu sana!
ANGALIZO: Kuhusu chuo kibovu: vyuo vingi Tanzania, curriculum zake is a hard nut to crack, labda tofauti itakuja kwenye usimamizi. Walimu wengine wanaachia wanafunzi kwa sababu tofauti na nyingi, na roho njema ikiwemo. Mwingine ananaamua kumwachia mtu akajihangaikie huko, ajivue lawama ya kummaliza, na wengine wanatoa hela au K, sasa zote ni dynamics na haziko restricted kwa chuo kimoja!