Kwanini penzi la mbali linanoga kuliko la karibu?

Kwanini penzi la mbali linanoga kuliko la karibu?

A4.

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
670
Reaction score
109
Wadau nimeona niwashirikishe hili jambo ili wale wataalam wa malavidav watupe utaalamu wao
kwanini Penzi la Mbali huwa linanöga kuliko penzi la karibu nikiwa na maana kwamba;

kama una mpenzi wako mnaishi umbali wa kuweza kusitisha shughuli zako japo kwa siku mfano arusha-dar ili muonane, hisia zake ni kubwa na kuheshimiana kunakuwepo sana kuliko yule wa pale mtaani?

Wanandoa ambao hawakai pamoja wengi wao wanaheshimiana zaidi kuliko wale wanaoishi pamoja?

Mkianzisha mahusiano katika hali yoyote kabla ya kuonana au kufahamiana mnaonyeshana lv sana, ila mkikutana tu hata kama ni sms mlikuwa mnatumiana zinapungua?

Ni Theory gani inafaa kutumika hapa?
 
Lack of intimancy theorem -overexpected /estimated
 
Wa mbali Anatia hamu,siku mkikutana hata kama alikuudhi hamna muda wa kukumbuka ugomvi ni mahaba tu!!!
Wa Karibu ukimuudhi January ataongea mpaka December inakuwa kero tu
 
Mi kwa kweli long distance siwezi.

I want to be with my beloved and take care of him.
 
fimbo ya mbali haiui nyoka.....

sio kweli....... Hyo ni mitazamo na mawazo chakavu ya watu...... Lakin ukiingia kiundan haina ukweli kwa asilimia nyingi. Be frexible
 
ni kweli.. , kama tu wote hamchepuki. Linanoga na linakua na hisia kali na hamchokani. From experience.

wapi wewe? Ingekuwa ukichepuka kuna alama kama tick inakutokea usoni nadhan usingejisemea hilo. Mnazoeana, mnachokana, hata halinogi tena hilo penzi. Mnalala kitanda hicho mwaka mzima hata kama mna upendo kiasi gani! Kajaribu kuiba siku moja then utakuja kusema huku.
 
fimbo ya mbali haiui nyoka.....

hata pilao ni tamu ila hutopata utamu kama utalila kila siku. Inabd siku zingine ule hata matembele ubadil ladha ya mdomo.
 
Niko na experience ya relation ya mbali mwanzoni ilinipa ugumu sana saiv nimekubaliana na hali nainjoy nko naona ni sawa kwangu. sio shida wala hakuna shida yoyote
 
hata pilao ni tamu ila hutopata utamu kama utalila kila siku. Inabd siku zingine ule hata matembele ubadil ladha ya mdomo.

kwani ukibadili mapishi hupati ladha tofauti!?

Kama utaibadili mwenzi kila wakati ili upate ladha tofauti utabadili wangapi?!
 
Back
Top Bottom