Wanabodi,
Mie nashangaa sana kwanini huyu anayejiita Pasco hapendi chochote kinachofanywa na serikali ya Magufuli. Mbona sijahawi kuona akikosoa matendo mabaya ya watendaji serikalini na wafanyabiashara waliokuwa wanakwepa kodi?
Mbona hata hajawahi kusema chochote juu ya Richmond? Mie nadhani hata kama tuna mahaba na serikali iliyopita na machafu yake, basi tutoe sapport kwa serikali iliyopo ili ifanye kazi yake kama amabavyo wananchi tunataka..
Nilifikiri uwenyeji wako hapa jukwaani kwa takribani miaka 8 ungetosha kukufanya uwe na hoja zenye kuakisi ukongwe wako,kinyume chake umekuwa na michango ya hovyo kabisa.Hivi hadi Pasco ambebe huyo mtakatifu wako mgongoni ndiyo uone anamuunga mkono au la??Unataka mtu afanyeje ili aonekane anamuunga mkono huyo mtu wako?
Kutofautiana katika baadhi ya mambo na kukubaliana katika mambo ya msingi ni kanuni ya kimaumbile,ukiona mtu anakubaliana na kila jambo lifanywalo na mwanadamu mwenzake,hizo ni dalili za mtu huyo kutokuwa na matumizi sahihi ya kichwa chake.Badala ya kukitumia kichwa chake kufikiri,ameamua kukitumia kuoneshea mitindo ya nywele.
Yawezekana watu tukatofautiana katika mambo fulani,lakini tofauti zetu zisichukuliwe kuwa ni chuki juu ya yule uliyeamua wewe kumpenda katika kila jambo alifanyalo.Zipo hoja nyingi tu zilizoletwa hapa jukwaani na Pasco,zinazoonesha kuuunga mkono utendaji wa Mh.JPM,lakini kuna hoja pia alizozileta zinazokosoa utendaji wa JPM,sasa ulitaka misimamo ya watu juu ya JPM isibadilike?Kama wewe umeamua kuwa na ufuasi na ushabiki wa kikondoo hata katika mambo ya msingi ambayo sote tunaona hayapo sawa,huo ubaki kuwa msimamo wako,usiwalazimishe watu wapende kila kitu kifanywacho na serikali mithiri ya jeshi la policcm linalowalazimisha watu walisifie hata katika mambo ambayo yanaonekana dhahiri kuwa yanafanywa kwa mlengo wa kukibeba chama tawala.
Jamii iliyoacha wajibu wake wa kufikiri na kupanga kwa mustakabali wa ustawi wake,badala yake ikaamua kuwa mshangiliaji wa ghiriba za kisiasa,ni jamii mfu na isiyo na maono.Tusipoziruhusu fikra zetu kufikiri sawa sawa na kuyaruhusu macho yetu na ubongo wetu kuunda taswira sahihi ya yale tuyaonayo,kamwe hatutaweza kutambua jema na baya,tutabaki kuwa washangiliaji wa mambo ya kipuuzi na yasiyo na majibu ya changamoto zinazotukabili kama Taifa.Ukondoo wa namna hiyo unapatikana kwa makada wa aina yako tu,makada waliokunywa maji ya bendera kiasi cha kuvigeuza vyama vyao kama dini ya Mwenyezi Mungu,huo ni upumbav zaidi ya upumbav wenyewe.Badirika.