Kwanini Nyerere hakuendeleza kusini kwa miaka mingi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Nyerere hakuendeleza kusini kwa miaka mingi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Insurgent, Jun 23, 2012.

 1. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwanini Nyerere hakuendeleza kusini kwa miaka mingi?
  Kwanini sehemu nyingi zenye Waislamu wengi hazikuendelezwa kwa miaka mingi? (Hii ni tokea ukoloni)
  Jadili.
   
 2. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Sababu ya ukweli ni hii:

  Waarabu walikua middle class katika ranking ya kibaguzi ya mkoloni. Walikua wasaidizi wa mkoloni katika kukamata watumwa na walikua wanauza watumwa, hivyo maeneo walikokuwa wengi wakoloni waliwaachia kumiliki. Shule za mwanzo zilikua za mission na walikua wanafundishia kanisani. Shule hizi zilijengwa sehemu ambayo wakoloni waliishi kama vile kagera na kilimanjaro. Sehemu ambazo mwarabu aliachiwa, kwa vile hakuwa na malengo ya kutawala bali biashara, hakufanya la maana.

  Sio tu kwamba elimu haikutolewa kwa hayo maeneo ya waarabu pekee, bali hata maeneo ambayo watu walikua na tamaduni zenye nguvu sana kupambana na mkoloni hawakupata shule. Mfano ni maeneo ya Wamaasai.

  Nyerere alijitahidi sana katika maeneo ya kusini kwasababu hakukua na shule nyingi za mkoloni alizotaifisha kama maeneo mengine. Huku alianza upya! Watu ambao sijui walichokifanya kusini ni Mzee Mwinyi na JK. Mkapa kawajengea daraja angalau mikoa hiyo imefunguka.

  Endelea kujadili ukizingatia kwa makini kauli mbiu yako "Any man who reads...lazy habit of thinking"
   
 3. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Watu wa kusini ni wavivu sana,ata uwafanyeje..
   
 4. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hakuna sehemu katika Tanganyika ambayo Waarabu waliachiwa watatwale, na kama walikuwa sio watawala wangezijenga vipi hizo shule?!
  Ukweli wenyewe huyu jamaa ndiye aliye introduce ubaguzi wa Kidini, Kikabila na Kiukanda Tanzania.Kabla yake haijulikani katika historia ya Tanzania kuwa na ubaguzi.
  Aliyowafanyia Waislamu kila mtu anayajua, hakuacha hapo akaendelea na Wachaga, mwisho akawarudia watu wa Pwani na kudiriki kusema kuwa hakuna watu wanaoitwa Waswahili, aka invent neno Tanzania BARA ili kuwafuta Wapwani katika historia ya TZ! hii ni kwa gharama ya neno Tanganyika eti kwa sababu tu alikuwa hajui maana ya neno Tanganyika!
  Kibaya zaidi jamaa alikuwa si Mtanzania na vitendo vyake pia si vya Kitanzania. Maoni yangu binafsi:
  Haka kajamaa kafutwe katika Historia ya Tanzania.
   
 5. hodogo

  hodogo JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 239
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina hakika kwa bahati mbaya ukifikishwa hospitali, hata madakitari walio katika mgomo lazima watakuhudumia wewe kwa kukulaza ICU! Mjadala wako unatia shaka kwamba kama kuna darasa ulihudhuria basi ni yale madarasa aliyoasisiwa na huyo unayemponda! Unapojadili jambo hili halihitaji uwe na elimu ya kupitiliza. Jukumu la kuyaendeleza maeneo yote ya nchi hii lilikuwa jukumu la Mwalimu. Mwalimu aliikuta Nchi imegawanywa kikanda. Naona nijipe muda kukufundisha historia. Kulikuwa na ukanda wa kutoa Makarani, walimu na watumishi wa Maofisini, Ukanda huo ni pamoja na maeneo ya Kilimanjaro, kagera , Mbeya hasa Unyakyusani kuyataja kwa uchache, Pia kulikuwa na ukanda walikotoka askari, hapa utaona Mara, Iringa, Ruvuma kuyataja pia kwa uchache. Sasa kuna ule ukanda maarufu uliotengwa kwa ajili ya Manamba, Maeneo hayo ni pamoja na maeneo ya Manda, Baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya hasa Usafwani na karibu ukanda wote wa kusini!

  Kwa raslimali fedha chache alizokuwa nazo wakati anaanza kuiongoza nchi hii hakuna mjadala maeneo yaliyokuwa tayari yanamiundo mbinu ya kueleweka maendeleo yalionekana dhahiri. kwa mfano mashule yalikwisha kuwapo katika maeneo yale yaliyolengwa kutoa watumishi wa maofisini. Ndio maana Mwalimu aliamua watoto wasisome kikanda, haikushangaza kumwona mtoto toka Mtwara amepangiwa Old Moshi na alikuwa tayari kumsafirisha kwa gharama za Serikali ili akaipate hiyo Elimu!

  Jambo lingine lililo dhahiri ni kwamba Waarabu Hawakuthamini elimu! Angalia mifumo ya Elimu kule Zanzibar, ukanda wote wa pwani ukiondoa maeneo ambako wamisionari wa Kikristo waliishi, Tabora na hata Kigoma utaona hayohayo. Kwa nini akusomeshe wakati wewe ni bidhaa? Kwa msimamo huo ulitegemea Mwalimu afanye muujiza gani? Zaidi sana alikazana kupiga vita matabaka ya kikabila na kikanda yaliokuwa yamejengeka sana wakati wake.

  Usimlaumu Nyerere Walaumu waliokupa hiyo itikadi inayokumbatia ubaguzi kwa misaingi ya Kidini!
   
 6. M

  Mgelukila JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Historia imeeleza vizuri alikuta ukanda,hata hivyo alijitahidi kuedeleza akataifisha shule lkn wakoloni hawakujenga sana maeneo ya pwani alikwepo mwarabu ndiye wa kumlaumu maana aliangalia biashara tu ,
  Hata hivyo aliakikisha rais wa awamu ya 3 anatoka kusini ili kuzidi kuwakomboa, na mkapa amethubutu kujenga dalaja tatizo ni mwinyi na kikwete hawajafanya lolote.
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hakuendeleza Kagera either na Moshi alizuia kuendelea alisimamisha Maendeleo yake.

  Acha Fitina zako. wewe Haufai kwenye nchi hii unaleta uadui na chuki
   
 8. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  sehemu zenye Waislamu wengi ni zipi?huko kwingine Nyerere alitujengea vibanda?hivi hamjui wakati wa Nyerere mikoa fulani iliwekewa QUOTA ya kuingia SEKONDARI ilhali mingine ikipewa UPENDELEO?Kama Nyerere alijipenda vile mbona hakuijenga BUTIAMA,kikabakia kijiji tu?MMEONA HAPA MAENEO YA CHALINZE KUELEKEA WAMI takribani kilometa 15-20, JK alichopafanya?Lete mjadala mwingine,kumsingizia Nyerere tabia zenu mbaya huku PWANI ni mada isiyofaa JF
   
 9. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Pamoja na uvivu wao, lakini wamekutawala (Mzee Mkapa na Kawawa)!
   
 10. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hakuna personal attacks na kusingiziana hapa, tunamjadili mtu hivyo hapana shaka yoyote yatatajwa yale yote yanayomhusu aidha yanapendeza au hayapendezi, ndio ilivyo wakati akijadiliwa mtu!
  Kuhusu kutoijenga Butiama, unaonaje mtu akikwambia kuwa alikuwa haithamini kwa sababu si M-TZ? yaani uzalendo wake una mashakamashaka?
  Binafsi sioni ubaya wowote kama Mkapa, Mwinyi, JK au kiongozi yoyte yule akijenga kwao, yeye akijenga kwao, huyu akijenga kwao, mimi nikijenga kwetu ndio maendeleo yanavyoendelea nchi nzima! mwisho wa yote ni Tanzania na Mtanzania yoyote yule anaweza kuitumia hiyo mindombinu.
   
 11. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Kwa hiyo Nyerere aliendeleza wapi?

  Mwinyi aliendeleza wapi?

  Mkapa aliendeleza wapi?

  Kikwete anaendeleza wapi?
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Alijenga wakatoliki na kanisa katoliki kwa kutumia pesa za umma (st. nyerere mungu akurehemu)
   
 13. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Be specific!
   
 14. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  Na hawa marais wengine wameendeleza wapi?
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Out of topic..
   
 16. T

  Topical JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kapeleka pesa za umma kanisani (katoliki for 24yrs) na kuwajaza wakatoliki wenzake wachote pesa za umma..

  hatimaye kaambulia mwenye heri (st. nyerere mungu akurehemu)
   
 17. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180
  That is very simplistic, general and unfounded. Be specific please, otherwise that is only the manifestation of unfounded hatred!

  Hao marais wazuri wengine wamewafanyia nini?
   
 18. Akagando

  Akagando JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 536
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Udini hautaisha Tanzania,Mkuu kuendelea kwa Watu wa kusini ni uamuzi wao sababu Hakuna sehemu katika Tz ambayo Mwalimu Julius K. Nyerere alipendelea sana.
  Hata uzi wako huko kidini sana.
   
 19. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,147
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu kama hiki kwenye ukristo.huko kwenu ndiko mnajilipua ili kuiona pepo naona zanziber mmeanza mazoezi ya kujifunga mabomu kwenye umati wa watu

  pili swala maeneo flani kutoendele ni matatizo ya wakoloni kwani wao walikuja kutafuta mahitaji ya viwanda vyao kwakile kinachoitwa monopolistic demand
  kwa hali hii usitegemee waje watoe maendeleo nchi nzima(kwa faida ya nani?)
  wakoloni wa mwanzo (wajerumani) walijenga reli baadhi ya maeneo kwa sababu zao.. Mbona haikujengwa Bukoba..
  Na ukumbuke wakoloni walitenga maeneo kutona na mahitaji yao kwa mfano Kigoma na Rukwa yalikua ni lobor zone haya ni maeneo maalumu kwa kutoa vibarua wa mashamba yao.. Sasa maeneo kama haya yasingeweza kuendelea..

  Maeneo kama kagera kule wakoloni walipokuja walikuta kahawa zimeanza kulimwa zamani hivyo wakaendeleza kwa mfumo wa peasant economy.. Na shule zilikua kama motisha ili wasomeshe waliitaji wazalishe kahawa kwa wingi..

  Ndugu yangu shule niliyosoma mimi inatwa Nyakato iko Bukoba na ilijengwa mwaka 1927.. Na hii ni ya Nyerere..?, shule imesomesha wengi kama waziri kagesheki na nazir karamagi..

  Unajua kule Bukoba na kule kilimanjaro zile associations zilizoundwa kwa ajili ya kahawa zilitumika kusomesha watoto wa wakulima hata kabla ya Nyerere..

  Hivi unajua hata kabla ya kuanzisha katani pale Tanga wajerumani walifanya utafiti wa kisayansi na aina nyingi za katani zilishindikana zikakubali aina chache
  hii inaonesha hawa jamaa walikua hawakulupuki..

  Unajua mwaka 1888 wamepigana sana vita na waarabu wa Tanga hasa Abushiri na bwana heri kwasababu ya watumwa pale pangani
  sasa eneo kama hili wasingeweza kuwekeza sana..

  Ndugu yangu soma historia ya nchi yako.mwl Nyerere hausiki na maeneo hayo kutoendelea,tena kama si yeye kule Bukoba na kilimanjaro wasomi wangekuwa wengi zaidi (kuna malalamishi kwamba wahaya wamefelishwa kwa makusudi kupunguza speed yao katika elimu..
   
 20. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2012
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,451
  Likes Received: 288
  Trophy Points: 180

  Kama na hao wengine hawajaendeleza Kusini na huko kwingine kunakotajwa, ni muhimu kuhoji pia. Issue ni maendeleo ya Kusini na sehemu zenye waislamu wengi.

  Tunataka tuone kwa nini ni Nyerere anatajwa tu, si Mwinyi, Mkapa wala Kikwete? Au Kusini wameendelea sasa?
   
Loading...