Kwanini Nyerere anaendelea kuongoza kutoka kaburini?

Kwanini Nyerere anaendelea kuongoza kutoka kaburini?

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,331
Jenerali Ulimwengu | Toleo la 321 | 16 Oct 2013 | Raia Mwema

WIKI hii iliyopita imekuwa na mijadala mingi kuhusu mtu aliyeiaga dunia miaka 14 iliyopita lakini, pamoja na kuwa ni marehemu, amebakia kuonekana kama kiongozi wa kweli wa watu wake.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amekuwa na mvuto usiokuwa wa kawaida miongoni mwa Watanzania wa rika zote, na hata miongoni mwa watu wa nje ya nchi hii waliomjua binafsi na waliomsoma na kum-google.

Katika kuadhimisha maisha yake, watu wengi wamejaribu kufanya tathmini ya kile ambacho hasa kinamfanya mzee huyu aliyelala kijijini kwake Butiama aendelee kuwa na ushawishi mkubwa kiasi hicho, na kila aliyetoa maoni yake amekuwa na lake la kusema.

Nimesoma mahali kadhaa, na pia nimesikia kwenye mijadala ya redio, watu wakistaajabu kutokana na uwezo wa mtu aliyefariki muda wote huu kuwa anaendelea kuiongoza nchi kutoka kaburini.

Hatuna sababu ya kustaajabu kuhusu hili. Ingawaje haiwatokei binadamu wengi, lakini si ajabu kwa mtu aliyeishi maisha ya aina fulani kuendelea kuwa na ushawishi mkubwa hata baada ya kifo chake. Hii imetokea mara nyingi pale wanapoondoka watu waliofanya mambo makubwa wakati wa maisha yao, na hususan wale waliotenda mema.

Kwa hakika, hivyo ndivyo wanavyokuwa watu walioanzisha imani za kiroho zilizovuta hisia za wafuasi wengi, na imani hizo zikazidi kukua, kusambaa na kutangaa hadi zikafika sehemu ambazo waanzilishi wake hawakujua kwamba zipo sehemu za aina hiyo. Ndivyo ilivyo kwa imani za dini zilizotoka Mashariki ya Kati na hivi sasa zimetandaa ulimwenguni kote.

Viongozi wa kisiasa pia wanaweza kuwa na ushawishi kama huo wakiwa wamelala kaburini, na wakati mwingine wafuasi wao waliowarithi hujaribu kuwatumia ili wapate kukubalika mbele ya halaiki. Nahisi hiki ndicho chanzo cha kuwajengea makaburi ya aina ya makumbusho (mausoleum) na kuifanya miili yao ionekane kama wamelala tu, hawakufa.

Nyerere amezikwa Butiama, kama ilivyo ada ya imani yake ya kidini, lakini jina lake limeanza kuwa na ladha ya kinabii, kama vile alianzisha imani ya kidini ambayo wafuasi wake wanataka kuinedeleza na kuieneza kote wawezako kufika.

Nimesema hapo juu kwamba hata nje ya nchi wako wafuasi wa Nyerere wanaochukua sura ya waumini wake. Jaji Mkuu wa Kenya, Dk. Willy Mutunga amenukuliwa akisema kwamba yeye ni "mwathirika wa virusi vya Azimio la Arusha" na kwamba ni muumini wa sera za Nyerere. Si tofauti sana na imani za kidini, na wako wengi wa aina hii.

Inawezekana kwamba hali hii inasababishwa na ukame wa viongozi tulionao, si hapa nchini kwetu tu, bali katika bara la Afrika na duniani kote. Inawezekana ni kutokana na ‘nostalgia', kw amaana ya kukumbuka kwa kujutia siku za nyuma na kuziona kama zilikuwa bora kuliko hizi tulizo nazo. Lakini inawezekana kuna jambo jingine.

Nimewahi kuandika mara kadhaa kwamba Nyerere hakuwa malaika, na kwamba alitenda makosa mengi katika kuiongoza na kuitawala nchi hii. Yumkin, hilo ndilo linatuthibitishia kwamba kwa hakika alikuwa binadamu, la sivyo tungemwita mungu.

Tofauti kati yake na wengine ni kwamba alitenda makosa aliyoyatenda katika jitihada za kuiendeleza nchi yake na kuwainua wananchi wake kutoka katika masikini na unyonge. Hakutenda makosa yaliyotokana na utashi wa kujitajirisha yeye na familia yake wala kwa nia ya kusimamia maslahi ya mitaji mikubwa ya "wawekezaji" na waporaji kutoka nje.

Aliishi maisha ya mtu wa kawaida; alipenda kuvaa kama mtu wa kawaida; alichukia anasa na tabia za kujipamba mithili ya tausi; magari yake yalikuwa si yake bali ya dola, na yalikuwa magari ya kawaida kabisa; alichukia mbwembwe zisizo na maudhui. Alipenda kufanya kazi, wakati mwingine kazi za ngwamba ambazo watu wengi huzikimbia.

Misimamo yake ilikuwa imara na isiyoyumba, na ndiyo maana wawakilishi wake nje ya nchi waliweza kutoa matamko yaliyofanana bila kuwasiliana juu ya wanachokisema, kwani bosi wao alikuwa anaeleweka. Na tusisahau kwamba hii ilikuwa ni katikati ya malumbano makali kuhusu mapambano ya ukombozi wa Afrika, na diplomasia yetu ilibidi ipambane na diplomasia ya kinafiki ya nchi za Mgharibi maswahiba wa makaburu.

Nakumbuka nilipokuwa naanza kazi kama mwanahabari jijini, nikiwa na mijadala isiyoisha na mwanahabari mwandamizi, tulikua tukijiuliza iwapo baada ya Mwalimu tungeweza kumpata mtu wa kumrithi. Tuliona kwamba ingekuwa vigumu kumpata mtu ambaye angekubali majukumu mazito kama hayo.

Muonekano wa kazi ya kuongoza nchi wakati ule ulikuwa muonekano wa majukumu matupu, si raha. Nani angekubali kuishi vijijini na Wagogo na Waha kwa mwezi mzima, na kuamka kila siku saa 11 alfajiri kwenda kushinda analima kwa jembe la mkono?

Nani angekubali kila siku kuwa katika kampeni vijijini na mijini kuhimiza kisomo cha watu wazima, uzazi wa mpango, kilimo cha kisasa na kila aina ya kampmeni za ‘kipedagogia' kwa watu wake?

Diplomasia ulikuwa ni uwanja mwingine ambako Nyerere alitoa mchango mkubwa kuisogeza Afrika mbele, hasa katika masuala ya ukombozi na kutofungamana na upande wo wote. Aidha alikuwa msitari wa mbele katika kudai mabadiliko ya mifumo ya kiuchumi wa kimataifa (NIEO), na juhudi zake zinakumbukwa duniani kote.

Alikwenda mara chache sana kuhutubia Baraza Kuu la Umoja waMataifa (UNGA), lakini kila alipofanya hivyo hotuba yake ilibakia kuwa ni mpango wa kufanyiwa kazi na Umoja wa Mataifa kwa mwaka uliofuata. Alikuwa kiongozi miongoni mwa viongozi wa dunia.

Wiki ijayo nitasimulia kisa kimoja cha kushangaza, lakini kilichonipa fundisho maridhawa juu ya diplomasia ya Mwalimu, kisa ambacho kingeweza kuwafunda pia watawala wetu wa leo na wa kesho.
 
Hakuwa fisadi, period.
Ufisadi ni dhambi ya mauti. Kama nyerere aliweza kujenga viwanda vya nguo na vya simenti wakati ambapo kulikuwa na jembe la mkono tu. Na akaweza kuondoa kodi ya kichwa ilhali hakuwa na makampuni ya simu na ya uchimbaji madini ya kukamua kodi. Akaweza kujenga udsm na kusomesha watu bure huku akiwalisha siagi na mikate ya mayai. Akaweza kujenga hospitali na kutoa matibabu bure kwa kiwango kilichowezekana kiteknolojia kwa wakati huo!

Huyu mtu ataendelea kuishi kwa miaka mingi kwa sababu in no time soon is there any glimpse hope kuwa atatokea walau wa kufanana nae.
 
Jakaya anakwenda kila mwaka nani anamsikiliza zaidi ya familia yake na mafisadi anaowapa utajiri wa nchi hii. Tena nasikia alienda hadi Canada, huyu nkwere kweli anatia aibu na vipanzi vyake vimo humu JF vinajaribu kumdhalilisha mwl. Thubutu! JK atasahaulika kama Mwinyi aliyetuletea hili jinamizi.

BTW Ulimwengu pamoja na wenzako wa Rwanda na Burundi bila kusahau Uganda. Wengi wanajitahidi kwa udi na uvumba kuwahadaa Watanzania ati mwl alitaka EAC iwe moja .. .... ... etc etc. ni kweli wakati ule lakini baada ya kuona ishara na nafsi za nchi kama Kenya, kununuliwa na Mabeberu aliamua kufunga mpaka, na kamwe asingeufungua hadi pale Sokoine alipoliongelea hilo jambo kwa kina. Hivi sasa wanafikiri kumbu kumbu zetu ni kama za kwao. Tanzania haiwezi kuwa shamba la bibi mtachotachota hapa na pale lakini siku yaja Watanzania watakapoamua kuchukua kilicho chao na kuwaacha solemba. Tuwaache wale wanaojiona wako kwenye coalition of the willing waendelee.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hakuwa fisadi, period.
Ufisadi ni dhambi ya mauti. Kama nyerere aliweza kujenga viwanda vya nguo na vya simenti wakati ambapo kulikuwa na jembe la mkono tu. Na akaweza kuondoa kodi ya kichwa ilhali hakuwa na makampuni ya simu na ya uchimbaji madini ya kukamua kodi. Akaweza kujenga udsm na kusomesha watu bure huku akiwalisha siagi na mikate ya mayai. Akaweza kujenga hospitali na kutoa matibabu bure kwa kiwango kilichowezekana kiteknolojia kwa wakati huo!

Huyu mtu ataendelea kuishi kwa miaka mingi kwa sababu in no time soon is there any glimpse hope kuwa atatokea walau wa kufanana nae.

Bi dada salute...
 
Wengi wanapigiwa upatu sana but Nyerere alikuwa kiongozi wa viongozi na hatotokea wa aina yake tena...i wish wana wema wa nchi hii kama Mzee Ulimwengu aamue kutangaza nia! His humble,man of his word na ana hekima ya hali ya juu....
 
Halafu kuna watu wanakuja hapa jamvini na kubeza mafanikio mbali mbali ya Mwalimu. Eti DHAIFU kafanya mengi kwa Watanzania kuliko Mwalimu!!!! Pumbaf kabisa.

Hakuwa fisadi, period.
Ufisadi ni dhambi ya mauti. Kama nyerere aliweza kujenga viwanda vya nguo na vya simenti wakati ambapo kulikuwa na jembe la mkono tu. Na akaweza kuondoa kodi ya kichwa ilhali hakuwa na makampuni ya simu na ya uchimbaji madini ya kukamua kodi. Akaweza kujenga udsm na kusomesha watu bure huku akiwalisha siagi na mikate ya mayai. Akaweza kujenga hospitali na kutoa matibabu bure kwa kiwango kilichowezekana kiteknolojia kwa wakati huo!

Huyu mtu ataendelea kuishi kwa miaka mingi kwa sababu in no time soon is there any glimpse hope kuwa atatokea walau wa kufanana nae.
 
Kuna jamaa wanajiita wanaCCM damu na wanaharakati wa kupinga kile wanakiita Mfumo Kristo watakuja hivi punde kumshambulia Jenerali Twaha Ulimwengu!
 
Wote hao wana akili za kushikiwa, mwenye akili timamu na uwezo wa kuchanganua mambo kwa kina hawezi kukosa kuyaona mafanikio makubwa ya Mwalimu kama Rais wa Tanzania pamoja na makosa aliyoyafanya kama kiongozi na yeye mwenyewe aliyakubali makosa yake na kuyazungumzia hadharani, lakini bado mafanikio yake ni makubwa sana ukilinganisha na makosa yake.

Kuna jamaa wanajiita wanaCCM damu na wanaharakati wa kupinga kile wanakiita Mfumo Kristo watakuja hivi punde kumshambulia Jenerali Twaha Ulimwengu!
 
jenerali ulimwengu anakuwa ndumila kuwili; Anamponda mwalimu upande mwingine anamsifia sana;

.......... Hata hivyo jeneral Ulimwengu anatambua kabisa kama siyo mwalimu asingeweza kutia pua tz na ndo maana baada ya
mwalimu alimanusura kiweke.

........... Na kupitia hii nikuulize mheshimiwa sana jenerali ni kwanini uliamua kuuza kile kiwanda chako kwa habari
kwa yule mwanasiasa?.

Heshima sana kwa Mwalimu Nyerere (R.I.P.), sie tuliosoma bure tunatambua umhimu wa mwalimu katika nchi ya tz.

BAK naamini tuko pamoja hapa.
 
alikiuza kiwanda sababu hakutaka kutumika na magazeti yalishakuwa maarufu,na mafisadi ndio walikuwa wakiwanunua waandishi wakati ule.kuliko kutumika akaliuza gazeti.
 
Nimependa hapo kuwa "alifanya makosa lakin makosa yake yalitokea kwa nia nzur,aidha kutokana na kutokufaham vzur hicho anachosimamia au kupotoshwa,lakin alikuwa na nia nzuri TOFAUT na hawa viongoz wetu sasa makosa yao ni ya makusud wanafanya kitu wakijua kabisa kuwa wanakosea kwa maslahi ya nchi ila wapo kivyao zaid
 
Kwa Watanzania (si wote) kuongozwa na mfu aliyeko kaburini ni kitu positive!

...Watanzania baado saaaana!
 
Nimependa hapo kuwa "alifanya makosa lakin makosa yake yalitokea kwa nia nzur,aidha kutokana na kutokufaham vzur hicho anachosimamia au kupotoshwa,lakin alikuwa na nia nzuri TOFAUT na hawa viongoz wetu sasa makosa yao ni ya makusud wanafanya kitu wakijua kabisa kuwa wanakosea kwa maslahi ya nchi ila wapo kivyao zaid

I admit that Nyerere was very intelligent,smart,visionary,philosophical and examplary leader.But his choice of Socialism as a way foward in growing our economy and development as a whole wa a grave mistake,Socialism was killing potentials among Tanzanians who were forced to live as Socialists (very ordinary life),Nyerere's Socialism disrupted private enterprises which are key to innovation and delivery of high quality services & products,Having private sector mean you are providing people with alternative choices of products & services at affordable prices.Tanzania was very poor,Infrastructures were very poor.Economically speaking we were very poor.
 
Mwalimu ni tunu na ataendelea kuwa tunu kwa taifa hili pendwa wote wanaokuja lazima wajifunze kitu toka kwake.
 
Mwalimu ni tunu na ataendelea kuwa tunu kwa taifa hili pendwa wote wanaokuja lazima wajifunze kitu toka kwake.

Yeah Viongozi wana jambo moja au mawili muhimu tu ya kujifunza kutoka kwa Hayati Nyerere nayo Uadilifu na Uzalendo....
 
Halafu kuna watu wanakuja hapa jamvini na kubeza mafanikio mbali mbali ya Mwalimu. Eti DHAIFU kafanya mengi kwa Watanzania kuliko Mwalimu!!!! Pumbaf kabisa.
hata funza wa maiti wanawazidi hao mbulula wanaosema hivyo! HAKUNAGA KAMA BABA NYERERE NA HATATOKEA! waliofuata baada yake ni wezi na mashetani! especialy tuliyenaye sasa hivi, hana mfano, ni jangili kabisa!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwl Nyerere pamoja na talanta ya uongozi aliyokuwa nayo, alibahatika kusoma ulaya wakati ambao nchi za ulaya zilikuwa zinafanya mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa baada ya vita ya pili ya dunia. Binafsi nafikiri kuwa Mwl Nyerere wakati anasoma masomo ya Uzamili pale Edinburg kuanzia mwaka 1951, alijipata ndani ya maabara ya political economy reformation, ndio maana maneno aliyokuwa akiyasema miaka ile wengi wetu hatukumwelewa mpaka tunavyoona matokeo ya alichosema yanavyotokea leo hii.

Mungu amrehemu Mwl Nyerere
 
I admit that Nyerere was very intelligent,smart,visionary,philosophical and examplary leader.But his choice of Socialism as a way foward in growing our economy and development as a whole wa a grave mistake,Socialism was killing potentials among Tanzanians who were forced to live as Socialists (very ordinary life),Nyerere's Socialism disrupted private enterprises which are key to innovation and delivery of high quality services & products,Having private sector mean you are providing people with alternative choices of products & services at affordable prices.Tanzania was very poor,Infrastructures were very poor.Economically speaking we were very poor.

I'm compelled to agree with your argument that Mwl Nyerere failed on development economic policies. Nevertheless, I cannot stop wondering why did that happen because he had close friendship with Malyasian and Indonesian PM by that time. Possibly the African politics by then clouded his imagination on Tanzanian economy.
 
Back
Top Bottom