Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Wanabodi,
hili linaniumiza kichwa!
Mapinduzi yaliofanyika Zanzibar ya kuuondoa utawala wa Sultan, kama inavyosomeka kwenye nyaraka za CCM, yalifanikiwa bila ya kumkamata Sultan Jamshid mwenyewe.
Bahati nzuri alikimbilia Kenya lakini alikataliwa na Kenyatta kuingia Kenya na hivyo kuamua kuja Dar es Salaam. Awali ilionekana safari hiyo ni kama " from frying pan into the fire". Ilikuwa kinyume chake, Nyerere alimpokea yeye na familia yake na kumpa hifadhi ya muda mpaka pale safari yake kwenda Uingereza uhamishoni ilipoiva.
Wakati huo huo, Waziri mkuu Mohammed Shamte, mshirazi mzanzibari na baraza lake lote la mawaziri waliwekwa kizuizini bila ya kufungufuliwa mashtaka kwa miaka kumi(10) katika Magereza tofauti nchini Tanganyika.
Sasa hapa ndipo ninapojiuliza, mantiki iko wapi? Wakati Shamte na baraza lake la mawaziri wakiteseka kwenye magereza ya Tanganyika kwa miaka kumi na hatimae kumalizika kwa kufa mmoja baada ya mwengine ,Jamshid kaachiwa huru na sasa yuko Uingereza, na kwa mujibu wa maandiko matukufu ya CCM anataka kurudi Zanzibar kuja kurudisha Usultani!
Kwa nini Nyerere asimfunge Jamshid pamoja na akina Shamte wakati aliepinduliwa hasa ni Sultani Jamshid?
Au iliopinduliwa hasa ni serikali ya wazanzibari wazalendo ya akina Shamte na hivyo ya Jamshid yalikuwa ni funika kombe tu.
Au hii kete ianyatumiwa na CCM kuhusu Jamshid ni geresha kuona yale matunda ya Mapinduzi na matumaini yake yameyeyuka na hakuna mwengine wa kumbebesha lawama moja kwa moja?
Nisaidieni wana bodi ,na hasa Maskani ya Kisonge na hasa mkereketwa mkubwa wa CCM, BarakaShamte, mtoto halali wa alieukuwa Waziri Mkuu, Mohammed Shamte.