Nianze kwa kumpongeza sana Nnape kwa uamuzi wake wa kulisimamia kidete suala la Uvamizi wa Clouds Media , kwani hili lilikuwa ni shambulio la wazi dhidi ya uhuru wa habari nchini, alivamiwa yeye binafsi kwani anasimamia wizara inayohusika na masuala ya habari.
Baada ya Pongezi , nitaweka sababu ni kwanini Nnape sio shujaa wangu, najua anatukuzwa sana kila mahali lakini hilo halinifanyi niache kuweka mtizamo kinzani hapa.
Kwanini Nnape sio shujaa wangu mpaka dakika hii;
1. Alisimamia kusimamishwa kwa matangazo ya Bunge Live, na alipopingwa alikuwa akisimamia msimamo huo bila kujali sauti za waliokuwa wanampinga .Waliokuwa wanampinga walikuwa wanaangalia mbele na walishaona hatari.....Anatakiwa kujitokeza na kuwaomba radhi watanzania kwanza .
2. Alisimamia kupitishwa kwa sheria hatari ya habari -hakuna asiyejua majibu yake kwa wabunge, MOAT,TEF nk walipokuwa wakimuomba muda ili waweze kuwasilisha maoni yao kwa ukamilifu , hii sheria ilipitishwa baada ya wabunge wa CCM wote including Mawaziri kupewa hongo ya shilingi milioni 20 .....Lilisemwa Bungeni si TAKUKURU wala nani aliyeweza kukanusha hili....Nnape auseme ukweli sasa yawezekana akawa shujaa wangu.
3. Amekuwa mjumbe wa Cabinet , najua kuna siri ambazo hawezi kuzisema kwani alikuwa amekula kiapo .Ila kama kuna mambo ya Hovyo yaliyofanyika na mipango ya hovyo ajitokeze sasa na kusema ...aweza kuwa shujaa ......Atueleze hivi yanayosemwa huko mitaani kuhusu Bwaba mkubwa yana ukweli ?
4. Ajitose Bungeni na aanzishe motion ya kumwondoa Madarakani kwa mujibu wa Ibara ya 46 , akianzisha yeye ataungwa mkono , hapo atakuwa shujaa wangu .......Hata kama akikwamishwa ujumbe utakuwa umefika panapostahili.........
Akifanya hayo anaweza kuwa shujaa wangu , lakini sio kwa tukio moja la kusimamia kazi yake eti awe Shujaa .....HAPANA .....Historia ina tabia ya kumuandama mtu taratibu ......aweke historia sawa.