Edward Lowassa, mwanzoni niliposikia tuhuma zako kabla sijazifanyia utafiti nilikubeza ila nimejifunza mengi kwako, hakika unastahili kuwa Rais wa nchi hii. Nimejifunza haya kutoka kwa Lowassa;
1. Ukiwa na vision kubwa isimamie bila kujali dunia au watu wanasemaje, uliutaka urais tangu zamani na umesimamia vision yako na hukukurupuka.
2. Unanidhamu kwa viongozi wako wa dini au neno la Mungu, uliposhauriwa kukaa kimya uliheshimu na ukawa mnyenyekevu.
3. katika maisha lazima uwe na priority katika vision yako, umesisitiza priority yako kabla na baada ya kuhama ccm elimu elimu elimu, mpinzani wako hajawahi kusikika popote akitoa dira ya taifa. Kutoa mitazamo yake na jibu kwa matatizo ya watanznia ametokezea tu kampeni zilipoanza. Anajisifia barabara ambazo hata nchi ikiwa chini ya jeshi lenye nidhamu bado zitajengwa, ndio maana anatoa ahadi moja yenye thamani ya tillioni 44 (refer nipashe ya leo).
4. Confidentiality,
Hii ni sifa kubwa watanzania tunazidi kuipoteza. Leo hata watu wenye heshima wakiwasiliana wakiwastressed kidogo tu wanatangaza ili wapate umaarufu mwepesi. mfano Dr weapon, Mchngj Gwjm, Polpl, mnadhimu Lisu n.k wewe umejua siri za serikali lakini kwa usalama wa taifa na amani unajua uongee nini na kwa wakati gani. Unajua unataka kuwatumikia watanznia wakiwa sio vilema, bila machafuko.
5. Ukizuiwa kupita mlangoni na hata dirishani Bado unaweza kung'oa bati ukatoka utimize kile unachoamini kuliko kubaki na kufa kifo cha aibu na uwezo wako ukapotea. plan B katika maisha haipukiki. Umenifundisha kuna sababu ya kubadilika kama unaona uelekeo uliokuwa sio sahihi. Kubadilika huitaji mwaka ni wakti mwingine ni siku moja au saa tu ya kufanya maamuzi sahihi.
6. Ukishatolea ufafanuzi jambo unasonga mbele Muda ni Mali. ulipojieleza kwa tido miaka hiyo kuhusu richmond ukamaliza kwa kusema the "Historia itawahukumu ". Umeamua kuwaacha wajibishane wao wewe unaendelea na focus yako.
7. Umenifundisha kuwa ukiamua kuhitaji mambo makubwa inakubidi na wewe uwe na moyo au mapafu Makubwa ya kuvumilia mishale ya maadui wa ndani na nje. Kwa mara ya kwanza Mtu mmoja anashambuliwa Kina kona, pande kuu zote za dunia, mitandaoni, magazetini. Umeundiwa kamati ya watu zaidi ya 30 kwa mara ya kwanza katk historia ya siasa ya tanzania lakini umedumu kuwa imara.
8. Unatukanwa kuhusu afya yako, huku ukiwajua kwa undani afya za wapinzani wako. yawezekana zikawa ni mbovu kuliko hata yako....lakini umekaa kimya maana sio sehemu ya malengo yako. Maana kuruka au kukimbia sio kipimo pekee cha afya bora. Baba wa taifa aliondoka airport kuelekea hospitalini uingereza akiwa anatembea akitabasamu mwenye uchangamfu lakini Mwnyz Mungu aliruhusu arudi amelala. JK alipougua wote tulimpa pole ila wewe unaonekana kama mtu unayestahili magojwa na ikibidi kifo wakati hakuna anayejua kama unaumwa .
Mambo haya yamekupa heshima sana, Hata kama ikitokea Umeshinda au kushindwa utaingia katika kitabu cha historia ya siasa Africa.
Lowasa nitakupa kura yangu kabla ya saa nne asubuhi, nitakutafutia na kura nyingine zaidi ya ishirini kwa kushawishi watu kama zawadi kwako.