Kwanini nitampa kura yangu Lowassa Oktoba 25

Kwanini nitampa kura yangu Lowassa Oktoba 25

Mimi binafsi nitampigia tu Lowasa,maana hakuna msafi ccm,miaka tulowapa nchi watuletee maendeleo wameshindwa kufanya hvyo kwa kiasi tunachotaka,acha mabadiliko yachukue nafasi,watanzania tusisubiri mpk mzungu aje kitushauri tuwaondoe Hawa ccm
 
Ntampa kwasababu ni mwizi like serious i will vote for lowassa simply because ni mtuhumiwa ufisadi....wasafi wametufikisha wapi
 
Kashfa moja ya Richmond isingefanya waliomkata wamkate au waone hafai. Atakuwa na madudu mengi. Mengine labda kwasababu ya uhusika wa wengi ndo maana hayasemwi.

Nikiwa msomaji na mfuatiliaji mkubwa wa mambo ya wakubwa ntakuwa wa mwisho kuamini kuwa anahusika na ufisadi wa Richmond peke yake.

Tafuta habar, tafakar kesho hutokaa udanganywe kirahisi ewe mdanganyika

Siwayataje kwa sababu sio mwenzao tena. Hata wanandoa wanapoachana ndio wakati wa kuweka maovu ya kila mmoja hadharani. Washenzi tu hao debe tupu haliachi kuvuma.
 
Kashfa moja ya Richmond isingefanya waliomkata wamkate au waone hafai. Atakuwa na madudu mengi. Mengine labda kwasababu ya uhusika wa wengi ndo maana hayasemwi.

Nikiwa msomaji na mfuatiliaji mkubwa wa mambo ya wakubwa ntakuwa wa mwisho kuamini kuwa anahusika na ufisadi wa Richmond peke yake.

Tafuta habar, tafakar kesho hutokaa udanganywe kirahisi ewe mdanganyika

naomba tuambie wadanganyika ayo mdudu
 
Kama kitu hukijui ni bora ukae kimyaa!!!! ukaomba wanaojua wakakupa data, coz usilolijua ni giza nene kwako. Ikulu sio pango la wezi
 
Yule Richmond. Huyu Escro wewe ni Epa au mwengine MV Dar es salam scam au kilwa road scandal su yule kauza nyumba za serikali kwa bei za wizi ....hawa wote ni mahadidi wa mali za umma wote hakuna msafi..lakini tunaweza kufumba macho kwani kumpata safi kabisa ni mgumu ..lakini ni vigumu kumpa kura mtu au chama ambacho kina finyanga haki za raia wake. N vigumu kumpa kura wale walotia ndani masheikh zaidi ya 15 .
Ni vigumu kukirejesha chama kinachoendesha serikali tena huku kikifunga masheikh wale bila ushahidi wa maana. Nafsi yangu inaniambia hio sio haki na dhambi kubwa sana kuwasaidia kurudi tena madarakani wanyanyasaji. Ni dhahiri kila mpenda haki anachukizwa na uonevu huu na waislam wana haki ya kusema sasa inatosha

Mkuu bado kuna ile issue ya rada na mzee wa vijisenti, bado MEREMETA!! CCM imeoza kwa ufisadi, nilikupenda Sana CCM ila sina budi kukuacha maanaumezidi kuiba na kupenda tumbo yako na family yako zaidi. Kura yangu na familia yangu Ni kura 8 Ni kwa lowasa. Bora nimpe yule ninaeaminishwa ni fisadi kuliko nimpe yule msafi anaenadiwa kama yule mmachinga aliyepita na kujimilikisha Kiwira pamoja nguvu mpiya kazi mpiya(Baba riz) maana athari zao nimeziona.
 
Ntampa kwasababu ni mwizi like serious i will vote for lowassa simply because ni mtuhumiwa ufisadi....wasafi wametufikisha wapi

chukua like ya kwenye SIM mkuu, umenena jambo
 
Lowasa lazima awafurumushe majizi pale magogoni
 
Juzi nimeenda hospital ya serikali (palestina -sinza) ninayo kadi ya bima ya afya ila nilikereka kidogo nilie kiukweli. Dr alinitibu ila dawa kulikuwa hamna hata Panadol walah, baada ya kutibiwa nikaandikiwa dawa za kutumia nikachukue dirisha la dawa kufika dirisha la dawa muhudumu aliniandikia nikachukue dawa Tip top pharmacy Manzese, yaani kidogo nilie kiukweli! Nikamuuliza naomba hata Panadol nimeze nikiwa pale na ilikuwa ni saa 7 usiku, alinijibu "hamna" hivi binadamu si unapoteza maisha!! Maisha bora mliotuaminisha yapo wapi?? Leo mtu aniambie CCM nitamwelewa! RIP CCM, haiwezekani viongozi wa ccm muibe mabilioni then mimi mwananchi niteseke hata dawa hospital nikose!! unipe gharama Mara 2 eti ya kufata dawa sehemu nyingine!! Wakati nyie mnagawana kodi zetu! CCM ni marehemu mtarajiwa na kila mtu aseme Amina
 
Mimi ni miongoni ya waliokuwa wanamchukia lowassa na sitaki kusikia lowassa na ccm. Hakika sasa namwelewa lowassa lakini bado sitaki kusikia ccm. Wanihakikishie kama lowassa anavyohakikisha kuwa mamlaka ya juu ilimzuia kufuta richmond. Hilo la kulinda serikali isianguke namsamehe pamoja na kuwa najiuliza hivi angeteuliwa na ccm angetuambia ama ilikuwaimetoka? Ama ndio maana ccm waliamua kumtoa mhanga (sacrifical ram) kwa nguvu zote wakijua atawaadhibu?!
 
Richmond hata kama lowassa anahusika hainihusu. MIMI NAMCHAGUA LOWASSA KWA KUWA MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENDI. NAKUMBUKA NILILIA SANA LOWASSA ALIPOJIUZULU KWANI KAMA SIYO YEYE SIJUI NINGEKUWA WAPI.
NIMESOMA SHULE ZOTE HADI CHUO CHA KATA. KAMA ASINGEZIJENGA NINGEKUWA WAPI??
NAMCHAGUA LOWASSA KWA KUWA ANAJUA JINSI NINAVYOTAABIKA.
MUNGU AKUSAIDIE SANA LOWASSA
 
Kila ninapokwenda kuwatembelea ndugu zangu walioko kijijini machozi hunilenga,naumia kuona UKATA wao umetokana na mfumo papa wa kifisadi na kulindana kwenye DHULUMA wa serikali iliyoko madarakani!
 
Kila ninapokwenda kuwatembelea ndugu zangu walioko kijijini machozi hunilenga,naumia kuona UKATA wao umetokana na mfumo papa wa kifisadi na kulindana kwenye DHULUMA wa serikali iliyoko madarakani!

Na Lowassa alikuwa sehemu ya udhalimu huo akipora ranchi za serikali, viwanja na nyumba. Kajilimbikizia mali isiyo na mfano ye na familia yake. Tuliyopambana na ufisadi huo tuna faili ya uchafu wake wote na hatutajisahaulisha au kushiriki kumsafisha.
Mkuu, tusipoacha unafiki na siasa za kuogopana na kulindana hatutafikia lengo kuu la kujenga misingi imara ya taifa.
Kumweka Lowassa mgombea wa Ukawa bila ye kutubu au kukiri makosa yake ni tusi kwa wale wana mageuzi wote waliopambana na udhalimu, ufisadi na dhuluma.
 
..labda ushauri watu wasipige kura mwaka huu.

..kwasababu hata Magufuli naye ana ufisadi wake wa kuuza nyumba za serikali kwa bei sawa na ya gari mkweche.
 
..labda ushauri watu wasipige kura mwaka huu.

..kwasababu hata Magufuli naye ana ufisadi wake wa kuuza nyumba za serikali kwa bei sawa na ya gari mkweche.

Huu ni uchaguzi baina ya fimbo na rungu!
 
..labda ushauri watu wasipige kura mwaka huu.

..kwasababu hata Magufuli naye ana ufisadi wake wa kuuza nyumba za serikali kwa bei sawa na ya gari mkweche.

Huwezi kulinganisha ufisadi wa Magufuli na wa Lowassa. . Sitaifanya kazi ya CCM lakini subiri waanze kuanika faili yake including upelelezi dhidi yake na familia yake wa vyombo vya nje kama Serious Fraud Office (SFO), offshore accounts zake nk. Kama ni ardhi na nyumba Lowassa kapora sana na zitaibuliwa..
Wakimaliza Magufuli ataonekana malaika .. na watu watachagua the lesser evil.
Tutaendelea kuwa pamoja na utakumbuka maneno yangu, mkuu ..
 
Hongera kwa kupenda mabadiliko
 
Attachments

  • 1438736048503.jpg
    1438736048503.jpg
    36.5 KB · Views: 66
Na Lowassa alikuwa sehemu ya udhalimu huo akipora ranchi za serikali, viwanja na nyumba. Kajilimbikizia mali isiyo na mfano ye na familia yake. Tuliyopambana na ufisadi huo tuna faili ya uchafu wake wote na hatutajisahaulisha au kushiriki kumsafisha.
Mkuu, tusipoacha unafiki na siasa za kuogopana na kulindana hatutafikia lengo kuu la kujenga misingi imara ya taifa.
Kumweka Lowassa mgombea wa Ukawa bila ye kutubu au kukiri makosa yake ni tusi kwa wale wana mageuzi wote waliopambana na udhalimu, ufisadi na dhuluma.

Mahakama zipo hazipo?au hizo mahakama pia huna imani nazo?amesema mwenye ushahidi kuwa alihusika na Richmond ampeleke mahakamani kesho asubuhi.

Na mimi nasema hakuna kitu kibaya duniani kama kuaminishwa jambo pasipo kulifanyia uchunguzi!Unamkumbuka yule kijana mhasibu wa Tanesco aliyebambikwa kesi ya mauaji baada ya kurudi kutoka Malaysia ambako alithibitisha hakuna kampuni iliyosajiliwa yenye jina ......iliyokuwa na share IPTL?Kama sio mambo hadharani ungekuta amehukumiwa kunyongwa kwa kesi hewa.
 
Mbona mna-focus na Richmond peke yake?
Je faili lake la SFO ya Uingereza ambayo serikali ilimkingia kifua unalijua? Narudia subiri kampeni ianze. Tuliokuwa ktk vita hivi dhidi ya ufisadi tunajua kinachojificha nyuma ya utajiri wa Lowassa. Mkuu, usione Dr Slaa mjinga kuamua kujiuzulu na kujiweka kando. Nakuhakikishia Lowassa hawezi kumnyoshea kidole Magufuli kuhusu ufisadi. Na timu ya CCM will have Lowassa for breakfast.
Mnalilia apelekwe mahakamani? Unafikiri wanashindwa wakiamua? Na si kwa kumwonea Lowassa bali kwa kuwa walimvumilia kwani alikuwa mmoja wao.
Hii movie ndo kwanza imeanza mkuu. Ni mtego CCM wamewaweka Ukawa and they walked right into it. Dr Slaa kashtukia mapemaaa!
 
Back
Top Bottom