Kwanini ninagombea Ubunge wa EAC - My Case!

Narejea kauli ya prof wange hivi karibuni kuwa " wagombea wapimwe uwezo wao kwanza".. Nina mashaka juu ya uwezo wako wewe achia mbali jina pengine linaweza kukusaidia. Nimesoma statement yako hapo juu.....mmm inaonekana lugha uliyoitumia haipandi sawa sawa. Next time, jaribu kuwasilisha ujumbe wako kwa lugha ambayo unai"master" sawasawa. Hiki chuo ulichosoma DMTU ni kipi hiki, kwani najua kuna chuo kinachoitwa DMTI. Anyway nakutakia kila la kheri.
 

Nafasi nyingi ni za kubebwa huwezi kuzipata kama KANUMBA!
 
Yani viza itolewe kenya harafu mgawane mapato, mhh. Mtai juaje viza ngapi zimetolewa labda nielimishe hapo?
Wakenya wanapenda kucheza sana na saikoloji mie siamini sana hata news yao ya ku strike oil turkana, ni saikoloji game ili tuingie kingi.

MkamaP,

..kuna mpango wa one tourist visa kwa nchi za EAC.

..sasa wengine ndiyo tunauliza mapato yatagawanywa namna gani??

..wakati wanadai hiyo one tourist visa, Kenya wanaeneza propaganda kwamba Kilimanjaro International Airport is not safe!!

..kuna ujanja-ujanja mwingi sana unaendelea na tunahitaji watu ambao wanaweza kuwa-face wa-Kenya na kuwaambia ukweli.
 
maelezo yako hayana maana mkubwa unaweza kuwahadaa watu wasiolewa but not interlectuals ur realy wrong with ur move mzee weka mambo wazi hatupendi story
 

Kwenye red hapo, maana yake nini maana huwa nasikia nitazamapo picha za kidhungu!
 

Tena juzi juzi hapa Kenya Airways ilikua inapanga kutumia US $ 3.6 billion katika kununua ndege mpya 68 na kupanua routes, katika kipindi cha miaka 5 ijayo. Nia ya shirika ni kusambaa zaidi Afrika na Asia (hususani India na China).
Pia kumbuka toka April ya mwaka jana Kenya Airways walikua wameshaingia makubaliano na Boeing, ili kununua 787 Dreamliner 8.

Kenya Airways eyes $3.6bn expansion in five years


Kenya Airways Eyes USD$3.6 Bln Expansion
 
maelezo yako hayana maana mkubwa unaweza kuwahadaa watu wasiolewa but not interlectuals ur realy wrong with ur move mzee weka mambo wazi hatupendi story

Duh! Jamani tupende kuandika kwa lugha yetu ya taifa.
 

Mkuu
Nafikiri mapato hayaendi kwa kugawana kila nchi inayotoa viza ndo mapato yake. Hata hivyo tatizo sio viza tatizo ni soko la utalii Tanzania linakufa, pili mahoteli yatakufa, tatu uwanja wa ndege vitakufa, wakiruhusu tu hiyo viza.
 

Kitufe cha like sikioni mkuu... Le baharia ni mweupe sana kichwani ndio maana. Uwa anakimbia changamoto zinazo mkabili, me pia aliwai kuniblock baada ya kumkosoa. Angakuwa ni mod humu ndani wengi tungechezea ban
 
Mkuu
Nafikiri mapato hayaendi kwa kugawana kila nchi inayotoa viza ndo mapato yake. Hata hivyo tatizo sio viza tatizo ni soko la utalii Tanzania linakufa, pili mahoteli yatakufa, tatu uwanja wa ndege vitakufa, wakiruhusu tu hiyo viza.

MkamaP,

..sasa tufanye nini wa-Tanzania??

..Kenya wanampango wa kujenga airport Taveta wakati sisi hatuna mpango wowote ule wa kuimarisha KIA.

..Kenya wameanza kujenga bandari itakayokuwa na gati 32, sisi tunasusua kuongeza gati mbili[ya 14 na 15] bandari ya DSM.

..wenzetu wanajenga bomba la mafuta, na reli kuelekea Sudan ya kusini, sisi tumelala tu. Kwanini hatujengi reli kwenda Rwanda,Burundi,mpaka Kisangani. Zaidi kwanini hatu-propose Tazara iende mpaka Lubumbashi???

.
 

Mkuu,
Mfano haya madini yetu yamekuwapo toka enzi za Mwalimu na akasema yaacheni mpaka watz wapate elimu ya kutosha, lakini naona tukayavamia kabla elimu haijatosha.

Vivyo hivyo, kwa hii nafikiri tungoje ama tusiingie kabisa ktk mtego huu, mpaka pale tutapoona interest za nchi zinalindwa na hasara ya matokeo haina impact ktk uchumi wa nchi na mstakbali wake.
 
Our security and economic interests ?
Do you even know the impact of free movement to a country like ours?
Can you at least tell us what's the real unemployement rates of EAC member states?
Nadhani mkuu ukipiga porojo na wabunge wa CCM utaweza kupata, ila hutaniwakilisha mimi.
 
We unafikiri huo ni ujanja?
Tukiamua, hao watalii wote wataopitia Taveta tunawatoza kodi ya maana.
Kuhusu hizi multinational projects mkuu, ni lazima uangalie stability ya hizi nchi. Ni hasara tu.
 
We unafikiri huo ni ujanja?
Tukiamua, hao watalii wote wataopitia Taveta tunawatoza kodi ya maana.
Kuhusu hizi multinational projects mkuu, ni lazima uangalie stability ya hizi nchi. Ni hasara tu.

kobello,

..But I am yet to see one bold project, si kwa Mkapa, wala Kikwete.

..OK, kama DRC,Rwanda,Zambia, siyo stable how about solving tatizo la umeme.

..Kenya ananunua umeme toka Ethiopia, kwanini sisi tusizalishe na kujitosheleza na kuuza kwa Kenya??

..I mean what r we doing kwa hii trade deficit kati yetu na Kenya? What r selling to Kenya other than raw materials??

..angalia education system yetu? what have we been doing tangu mwaka 1997 wakati jumuiya inafufuliwa? Tunakuja kukurupushwa baada ya kuambiwa turuhusu free movement of labor na graduates wetu wanaonekana hawana viwango?
 
We unafikiri huo ni ujanja?
Tukiamua, hao watalii wote wataopitia Taveta tunawatoza kodi ya maana.
Kuhusu hizi multinational projects mkuu, ni lazima uangalie stability ya hizi nchi. Ni hasara tu.

Sasa kodi utawatoza je ya maana? wakati wamesha integrate kodi ya wote iwe std, visa una free roam. Sasa utawakamatia wapi mkuu?

Nafikiri nao wanafahamu hilo ndiyo maana wanapush yote kwa wakati mmoja.
 
Mfano kama Tanzania wakidhamilia kabisa tukapata umeme wa uhakika, tukajenga bandari ya kisawasawa mtwara, DAR na Tanga.
Harafu tukaweka ma-treni ya umeme:
-kutoka Tanga mpaka mpakani mwa kenya,
-kutoka Mtwara mpaka mpakani mwa nchi zote za kusini
-Kutoka Dar mpaka DRC, Rwanda na Burundi
-Uwanja Wa ndege charge ikapungua kwa namna yake.
Naamini Kenya watagoma kuungana na kufanya soko la pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…