Mvaa Tai
JF-Expert Member
- Aug 11, 2009
- 6,159
- 4,443
Mara nyingi wakati wa uchaguzi mtu humpigia kura mtu amtakaye awe kiongozi wake akiwa ana sababu mbalimbali, Pia huwa na mtu ambaye asingependa kabisa awe kiongozi wake kiasi kwamba hata angelishindanishwa na kivuri angechagua kivuli(rejea miaka ya nyuma enzi za chama kimoja)
Kura ya mtu ni siri lakini kwasababu hapa Jamvini watu tunajifunza mengi sana kutoka kwa wachangiaji mbalimbali hivyo nafurahi leo hii kutoa siri yangu kwamba nilimpigia kura Dr Slaa na kuwaambia wenzangu kwamba sikumpigia kura Kikwete kwasababu nyingi tuu na nilitegemea hatoshinda lakini ikawa tofauti, zifuatazo ni baadhi ya sababu zilizonifanya nisimchague Kikwete.
1. Namuona kama hana uchungu na nchi yake, naamini anawakingia kifua Wezi wa rasilimali za nchi hata wanapobainika wazi. Mfano wezi wa pesa za EPA pamoja na kwamba wanafahamika aliamuru warudishe pesa walizoiba kisha waendelee kuwa huru japo mpaka wakati wa kampeni hakusema ni nani karudisha na nani bado na amechukuliwa hatua gani mpaka sasa. Kutokana na hili niliamua kumfukuza kazi.
2. Ninamuona kama ni mbabaishaji na mbahatishaji, kitendo chake cha kuunda baraza la mawaziri na baada ya mda fulani kutumia mda mwingi kuhamisha mawaziri toka wizara moja hadi nyingine, inaonyesha kwamba hafahamu uwezo wao hivyo ana bahatisha. Mfano Dr Shukuru Jumanne Kawambwaalimteua kama Waziri wa Mawasiliano, sayansi na teknolojia baadaye akagundua amekosea, akamuhamisha kwenda Wizara ya maendeleo ya miundombinu, hivi sasa huyu mtu ni waziri wa elimu naamini ipo siku atapata mahala sahihi pa kumuweka. Uzaifu huu ulinifanya nimfukuze kazi kikwete.
3. Nina muona kama hana Confidence, Katika kipindi chake kilichopita amekuwa anapenda sana kukaa na kuongea masuala nyeti ya nchi na wazee wa Dar es salaam ambao mimi naamini angewaacha wapumzike maana wamelitumikia Taifa kwa mda mrefu sana sasa na matunda yao tunayaona pia, hivyo angeyageukia makundi mengine kama vile Wawakilishi wa vyuo vikuu na taasisi mbalimbali nchini, Vijana wa Dar es Salaam nakadhalika, pia kitendo cha kukataa mijadala wakati wa kampeni nilihisi hana Confidence ya kushindanisha hoja zake na wenzake, hii pia ilipelekea nimfukuze kazi kikwete.
4. Namuona kama ni mtu asiyejali. Anadaiwa kutamka kwamba wanafunzi kupata uja uzito mashuleni wanajitakia wenyewe, haya si maneno mazuri kutoka kwa mzazi na Rais wa nchi. Hili nalo lilipelekea nimfukuze kazi kikwete.
5. Namuona kama ni muongo, katika kampeni zake za awamu yake ya kwanza aliniambia kwamba atahakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania, japo nilistuka kidogo, lakini nikamuamini tu nikampa kura yangu, kumbe alikuwa ananidanganya. Kwasababu binafsi sipendi mtumishi muongo, hili pia lilipelekea awamu hii nimfukuze kazi.
6. Na hivi karibuni nimegundua kwamba hayupo Serious, hii ni baada ya kutamka hadharani kwamba hamfahamu muwekezaji wa DOWANS, kama Rais wa nchi hamfahamu muwekezaji mkubwa kama huyo sisi wananchi itakuwaje? Hivyo nina shaka ipo siku nchi itauzwa yeye akiwa hana habari.
Hizi ni sababu zangu zilizo nipelekea nisimchague Kikwete naweza kuwa nilimuonea au nilimtendea haki nakaribisha maoni maana yatanisaidia kimsimamo hapo mwaka 2015