Bishop Hiluka
R I P
- Aug 12, 2011
- 7,150
- 14,724
Sekta ya filamu Tanzania kwa sasa inajulikana duniani licha ya matatizo yake,
licha ya mtayarishaji wa filamu wa Tanzania kuendelea kuishi maisha yasiyo
tofauti na mtu mwingine wa kawaida! Hali halisi ya soko la filamu nchini inabana
sana uwezekano wa kuibuka kwa wasanii, watayarishaji au waongozaji wapya...
Sidhani kama kuna mtu atabisha kuwa filamu za kibongo ‘hazitesi' katika ukanda
wa Afrika Mashariki na maeneo ya Maziwa Makuu. Filamu hizi zimesaidia kwa
kiwango fulani kuitangaza nchi hii, kuwatangaza wasanii wa nchi hii, lakini vipi
kuhusu maisha ya wasanii hawa? Je, wanapata stahili yao na wanaishi kwa
kutegemea filamu pekee?
Kinachosikitisha zaidi: utoaji wa hizi filamu zetu imekuwa kama mchezo wa soka
bila refa, sawa na mkutano bila mwenyekiti, darasa bila mwalimu, au nyumba
(familia) bila mzazi…
Wafanyabiashara wanaahidi milioni kumi na tano hadi ishirini na ushee kwa sinema;
watoaji sinema wanalipua kazi; waigizaji hawalipwi vizuri; utengenezaji sinema
unafanywa haraka haraka. Sinema zinatengenezwa kwa wiki moja na zinatolewa
ndani ya mwezi mmoja tu. Haraka haraka…
Wasanii wa filamu wanaigiza bila script wala mazoezi, watengenezaji filamu wengi
wanatumia mwanya huo kula uroda na wasichana wazuri wazuri (ndiyo maana siku
hizi kuwa miss ni kigezo kikubwa cha kupata nafasi ya kucheza filamu, haijalishi
kama una kipaji cha kuigiza au la), sinema zinazotolewa nchini eti zinalinganishwa
na za Wanaijeria! Tangu lini sinema za Wanaijeria zikawa kipimo cha filamu?
Kwa nini tufuate nyayo za Nollywood katika kuzalisha sinema zetu? Kwa kipi hasa?
Hii inatufanya kusimulia hadithi zao; angalia sinema zetu zinavyosimulia uchawi,
zinavyosimulia mapenzi au mikasa ya kijamii utagundua hilo. Tunaiga hadithi zao,
namna yao ya uchezaji, sinema zao ambazo nyingi zimekuwa zikiigwa kutoka
mataifa ya Magharibi na India.
Hivi Watanzania tumelogwa? Hii ni kwa Watanzania wote. Kwanini hatupendi/
hatununui sinema zinazotolewa na Watanzania wenzetu? Kisa? Hazituvutii. Moja
ya sababu ni kwamba zinatengenezwa vibaya kwa kulipuliwa. Lakini kwa nini hata
sinema zinazotengenezwa vizuri bado hatuzinunui? Kwa nini hatuzifurahii? Kwa
nini hatuzitolei maoni na kuzitangaza? Tunachoweza ni kuziponda tu! Hivi hatudhani
kuwa hiyo ndiyo njia kuu itakayotufanya tuendelee kama wenzetu, tunaowaona
Miungu kutuzidi?
Kwa upande wa waandaaji wa filamu tukumbushane kwamba sinema ni sanaa
inayochukua muda. Hatuwezi kutengeneza sinema ikakamilika ndani ya mwezi
mmoja tu. Tujipe muda katika kuifanya kazi kwa ufanisi zaidi. Ingawa wapo
wanaosema kuwa sababu ya kufanya kazi haraka haraka ni kutokana na matatizo
ya pesa ambapo mtu huhitaji kupata pesa haraka ili atatue matatizo yake.
Lakini tunasahau kuwa ukitoa kazi nzuri yenye ubora hukaa na huuzika miaka
nenda miaka rudi, tofauti na kazi zetu ambazo baada ya wiki mbili zinakuwa
hazina tena soko.
Tukumbushane kujipa muda katika uandaaji wa filamu zetu: Mwezi mmoja wa
mikutano kupanga mambo (wapi itapigwa picha, nani atafanya nini, waigizaji
watatoka wapi, watafanya nini), mwezi mwingine kupanga usanii (mazoezi ya
waigizaji, mazingira yao), mwezi mwingine wa kupiga picha. Baada ya miezi mitatu,
mingine miwili ya kuhariri na kusahihisha makosa.
Ndipo sasa kifuate kipindi cha kuitangaza kusudi iuzwe. Ukichunguza sana utagundua
kuwa sinema haiwezi kumalizika chini ya miezi sita kwa mazingira ya Tanzania.
Ndiyo maana wenzetu wanatoa sinema moja tu kwa mwaka lakini pesa wanazopata
wanakula kwa miaka kibao. Sisi tunatoa sinema kila mwezi lakini pesa yake ni ya
kujikimu tu.
Ni wakati sasa umefika tushirikiane, tuzichangamkie na tuangalie sinema zetu,
tuzifurahie na tupeane moyo…