Kwanini ni Hatari kwa Usalama wa nchi, Mswada wa sheria ya vyama vya Siasa?.

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Tangu juzi nipo naupitia mswaada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa nchini. Nimechomoa sehemu ndongo ya dodoso hizo ambazo wengi hamtazielewa lakini nitafafanua kidogo kwa lugha nyepesi ili kila mtu ajue nini kipo na kinakwenda kutendeka huko Bungeni juu ya mstakabali wa taifa letu.

Nitumie maneno ya hekima ya Wakili msomi Bob Chacha Wangwe ambae katika uchambuzi wake anasema hivi, Kazi yote iliyofanywa na Wazee wetu katika kujenga nchi ya kidemokrasia na nchi ya vyama vingi inaenda kusambaratishwa na mushwada huu ikiwa utakuwa sheria.

Muswada huu ni kwajili ya vyama vya upinzani peke yake. Hakuna kipengele hata kimoja kitakachoigusa au kuithiri CCM. Hakuna.
Muswada una mambo mengi ya ajabu. Ukipita na kuwa sheria Msajili atakuwa na mamlaka ya kukifutia usajili chama hata akiomba minutes za kikao cha kamati kuu ya chama chochote then kikakataa au kuchelewa kumpelekea. Hii ni kwasababu muswada huu unapendekeza msajili apewe mamlaka ya kupewa taarifa zozote kutoka kwa chama cha siasa.

Msajili atakuwa na mamlaka sasa ya kuamua nani agombee ubunge, udiwani, urais, uenyekiti wa chama, ukatibu mkuu n.k! Yaani kwa lugha nyepesi mwenyekiti wa ACT, Cuf, Chadema atateuliwa na Jaji Mtungi (msajiri wa Vyama vya Siasa).

Msajili atakuwa na mamlaka ya kutoa au kutotoa ruzuku kwa chama chochote cha siasa kwasababu maudhui ya kifungu cha 4(d) yatampa mmlaka hayo.

Kama hiyo haitoshi, litakuwa ni kosa kwa chama kuwa na sera zisizo unga mkono Muungano, Mwenge wa uhuru n.k!

Msajili atakuwa na mmlaka ya kuamua ni nani atoe elimu ya uraia (civic education) na nani aitoe. Yani hata elimu ya uraia sasa itaamuliwa na ofisi ya Msajili wa vya siasa.

Msajili amepewa mmlaka ya kukataa usajili wa chama cha siasa tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo chama ili kipate usajili wa kudumu kilitakiwa kukidhi masharti ya usajili. Huu muswada unasema sasa Msajili anaweza kukataa usajili kwa chama cha siasa bila kutoa sababu.

Mtu yeyote ambaye si mtanzania hatakuwa na ruhusa ya kusaidia chama cha siasa katika kutimiza malengo yake ya kikatiba. In short ni kwamba, hilo litakuwa ni kosa Kubwa kwa mujibu wa ushenzi huu unaoitwa “The Political parties (amendment) Act,2018!

Chama cha siasa kitakuwa hakina ruhusa ya kufanya harakati. Yaani, hata leo NCCR wakianzisha harakati za kupinga mauwaji ya Albino kule Shinyanga watakuwa wamefanya kosa.

Nini hasa athari kwa Taifa za mswaada huu ukipitishwa na Bunge lenye wabunge wa ccm ambo wao chama ni muhimu kuliko Taifa? Kwa maoni yangu nikitumia uzoefu wangu wa uchambuzi wa masuala ya kisiasa na ufuatiliaji wa migogoro mingi ya kisiasa duniani, ni kwamba taifa tunakwenda kulikaribisha kwenye hatari zaidi ya tufikiriavyo, Vyama vya siasa hasa vya upinzani vitakosa njia zote angalau zilizoonekana zinavipa matumaini ya siku moja kushinda kidemokrasia, na badala yake vitatafuta njia mbadala ya kushika madaraka, njia hizo ndizo zinaweza kuwa hatari kwa taifa.

Ninadhani kwasasa sheria ambayo ni muhimu kwa taifa na ni lazima ifanyiwe marekebisho ni, Sheria ya Usalama wa Taifa iliyosainiwa 20 January 1997 na Rais Mstaafu Mzee wetu Benjamiji W. Mkapa. Mfano, kifungu 14 -(1), (2),(3), (4)-(a) na (b). Kifungu cha 15 -(1),(2), (3) -(a) na (b). Kifungu cha 16-(1) (a)na (b), (2) na (3).

Lakini vivyo hivyo kuna sheria ya Jeshi la Polisi nayo inahitaji marekebisho makubwa, na Kuna sheria ya Tume ya Uchaguzi, hii nayo ni janga kwa taifa inahitaji marekebisho makubwa ili tume hiyo itafsirike kisahihi kwamba ni Tume huru ya Uchaguzi.

Kumbuka madhila haya ya kuuwa demokrasia hayataathiri vyama vya upinzani tu, bali kila mtanzania ataikumbatia chuki kifuani mwake, na siku akiona mwanya wa chama au makundi yanayotumia njia haramu kushika madaraka, ataamua kuungana nayo.

Yako mambo ni lazima tujiridhishe kabla ya kukubali uhalifu huu wa kisiasa unaotaka kufanywa kupitia bunge letu tukufu, Kwanza tujiridhishe sababu kuu ya msingi ya kuleta mswada huu nini? Je sheria iliyopo inamapungufu kiasia cha kuona bora kuleta hii? Je ni kipi kipaumbele kati ya kutunga katiba mpya ya nchi ambayo Umma ulishaanza mchakato wake na bunge hilihili likanajisi mchakato huo, au nikufuta mfumo wa kidemokrasia nchini? Sheria hii dharimu ni kwa maslahi ya nani?

Mswada wa Sheria Mpya ya vyama vya siasa unaondoa rasmi uwezekano ama uhalali wa CCM kutoka madarakani kwa njia ya kura. Kimsingi mswada huu unahatarisha taifa na kulisogeza kwenye viashiria vya uhaini ama uasi, tusiruhusu wabunge kutumia Bunge letu tukufu kulipeleka taifa huko kwenye viashiria na hatari za machafuko. Wabunge angalieni Taifa kwanza kuliko vyama vyenu.

Na Yericko Nyerere

Nyaraka hii chini....
 

Attachments

  • New Doc 2018-11-16 11.34.32.pdf
    10.5 MB · Views: 92
CCM wanaweza kuona kuwa ni njia nzuri ya kuwabana wapinzani lakini kumbe ndio kaburi lao.
 

Attachments

  • tapatalk_1542480427628.jpeg
    tapatalk_1542480427628.jpeg
    29.8 KB · Views: 112
  • tapatalk_1542480427628.jpeg
    tapatalk_1542480427628.jpeg
    29.8 KB · Views: 81
Ni nini mnakifanya huko cha siri zaidi ya kueneza sera za chama chenu mpaka muhofie kumpa taarifa za chama msajili wa vyama?

Kuna mahali kwenye huo muswada pametaja vyama vya upinzani pekee..

Huu ni upotoshaji
 
Dawa yao ccm ni sisi chadema kushinda uchaguzi ili hiyo sheria nasi itulinde kuliko kulilia tu watoto wa kiume!


Cdm kushinda uchaguzi sio tatizo kwani imeshashinda sana, ila kutangazwa ndio tatizo. Na kwa taarifa yako hizo sheria ni matakwa ya jiwe. Ukiangalia tabia za jiwe, hivi sasa ndio zinageuzwa na wasomi wetu kufanywa sheria za nchi. Hilo bunge liko hapo kupitisha (rubber stamp) utashi wowote wa jiwe. Katika mazingira haya ni dhahiri tutawaunga mkono watu wowote kutoka nje kuhakikisha taifa letu linaondokana na hili jinamizi. Kwa leo mtaona ni mzaha kwani ni nadra walevi wa madaraka kunusa hatari iliyo mbele yake.
 
Ni nini mnakifanya huko cha siri zaidi ya kueneza sera za chama chenu mpaka muhofie kumpa taarifa za chama msajili wa vyama?

Kuna mahali kwenye huo muswada pametaja vyama vya upinzani pekee..

Huu ni upotoshaji


Ccm sio chama cha siasa hivyo hizo sheria haziihusu. Andaeni machafuko kwa mikono yenu kwa kutii hisia za mtu mmoja.
 
Dawa yao ccm ni sisi chadema kushinda uchaguzi ili hiyo sheria nasi itulinde kuliko kulilia tu watoto wa kiume!
Uchaguzi gani huo wa CDM kushinda???Labda muwaondoe police, NEC ibadilishwe na katiba mpya kinyume chake hakuna kitu
 
Dawa yao ccm ni sisi chadema kushinda uchaguzi ili hiyo sheria nasi itulinde kuliko kulilia tu watoto wa kiume!
Kuna siku tutaimba wimbo mmoja.. Endelea kutetea hyo keki ya taifa ambayo mnaila wachache... Kuna siku tutaamua tuile wote.. Cjui utaficha wapi hicho kipara
 
kiukweli hapa msajiru wa vyama vya siasa anakwenda sasa kuwa msajiri kwelikweli na sio msajiri kivuli kama iivyokuwa awali

I wish I could be msajiri wa vyama
 
Back
Top Bottom