mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,743
- 7,257
Habari wakuu, kwanza nitoe pole kwa raia, viongozi na vyombo vya ulinzi kwa yanayoendelea kibiti. Hata kama kwa kosa gani bado halifanani na uhai wa mtu. Polisi wanauawa, viongozi wa kiserikali na chama tawala wanauawa, raia wasio na hatia wanauawa ( wengine wanauawa na polisi kwa kudhaniwa tu), viongozi wa upinzani pia wanadai kutekwa wengine kupotes na kuuawa pia na vyombo vya dola. Kwa ufupi ni kuna hali ya sintofahamu japo naamini hili swala liko mwishoni na washukiwa kutiwa nguvuni.
Lakini mara nyingi kama sio mara zote taarifa zimekuwa zikiripotiwa kwanza na gazeti la Mwanachi. Je vyombo vingine vya habari vikiwemo vya serikali hamchukulii umuhimu wa kutafuta habari na kufatilia matukio hayo ili kuutarifu umma? Kwani Mwanachi wanawezaje kuwa karibu mpaka kupata taarifa vyombo vingine vikashindwa? Kama wamepeleka waandishi wakapiga kambi huko wengine mnashindwa nini? Kama wamejiwekea utaratibu wa mawasiliano na watu au vingozi wa huko, je ninyi mnashindwa nini? Karibu Kila habari ni Mwananchi tu! Hata kuhakikisha kwa viongozi wa vyombo vya ulinzi baada ya tukio kutokea nalo ni linashindikana? Kwa mfano wakianza kutupa taarifa za uongo ili kututia hofu na kuonesha kuna kuongezeka kwa tishio la usalama.
Wauaji siku zote hutaka kuwatia walengwa wao khofu na kutuma ujumbe, kwa hiyo hutaka habari kuhusu matukio hayo ziwafikie wanajamii. Ndio maana kila baada ya kiongozi mkubwa kutembelea huko au kutoa onyo hufanya tukio.
Nimesahau ni gazeti lipi liliwahi kutuhimiwa na 'Mkuu' kuwa linaandika habari mbaya tu kuhusu serikali.