Kwanini NHIF inaweka sheria ngumu kwa wanachama wake

Hapana kwa hapo kosa Sio la daktari wala Hospitali kosa lipo Hapo BIMA NHIF..

Hospitali hawawezi kukutambua wewe usipokuwa na Bima na hataukileta Copy ni lazma Iwe verified na Bima ili kupata uhakika

Kwa kusema kosa ni la NHIF hauoni kwa mikakati hiyo ni dhahiri wana lengo la kumkwamisha mteja wao zaidi ya kumsaidia??

Kama unaweza kutoa hela bank pasipo card za bank?? Kwanini usiweze okoa uhai wa mtu kisa tuu card??

Nilijaribu kuwaza kwa wanaopata ajali kwa bahati mbaya labda card ikapotea au akiwa ameiacha mbali na alipopatia ajali itamlazimu aingie mfukoni au akose huduma kisa tuu card??

Wewe unaona NHIF NA HOSPITALI WALICHOKUBALIANA NI SAWA??
 
Hivi mkuu, nina swali nikichukua kadi yako original ya bima nikienda hospitali napata huduma?. Huu utaratibu ni suluhisho kwenye sekta hii nyeti ya afya imagine nimetoka kibaha nimekuja town kkoo kwa mahitaji mbalimbali ghafla napata tatizo na kadi ipo nyumbani hivi vituo vya afya na hizi bima wanashindwa kuja na njia mbadala ya verification?

Njia waliyokuja nayo ndio kama hiyo lengo ni kukwamisha tuu wateja wao,

Dunia ipo mbele sana kama mtu anaweza kwenda ofisi za Tigo/Voda na aka renew line kwa kutaja namba za NIDA na kuweka fingerprint, kwanini kwenye afya za watu wafanye masihara hivi??
 
Fraud kivipi wakati ukiingiza namba kwenye NHIF portal inakuletea details za mgonjwa pamoja na picha?? Pamoja na hayo nilishakua na file hospitalini hapo ukaachilia hayo nilikua pia na kitambulisho cha taifa, leseni ya udereva, cha mpiga kura na card za benki. Kwanini hawakutaka kunisaidia kwa namna zote hizo kama kweli NHIF wana lengo la kumsaidia mwanachama wao na sio kumkandamiza??
Uko sahihi na ndicho nilichokuandikia hapo Juu kuwa NHIF ndyo wanamakosa na Hivyo vyote huwa haviitajiki kinahitajika Check number Tu ukienda NHIF...

Ila Hospitali wao hawana kosa Maana Walitakiwa wapokee. Taarifa inaitwa "Verification Status" Kutoka NHIF ili wao wajiridhishe hakuna Tatizo lolote ili waendelee na matibabu..
Kwahyo waliokulostisha ni hao NHIF
 
Hivi mkuu, nina swali nikichukua kadi yako original ya bima nikienda hospitali napata huduma?. Huu utaratibu ni suluhisho kwenye sekta hii nyeti ya afya imagine nimetoka kibaha nimekuja town kkoo kwa mahitaji mbalimbali ghafla napata tatizo na kadi ipo nyumbani hivi vituo vya afya na hizi bima wanashindwa kuja na njia mbadala ya verification?
Siku hizi ukienda kwenye Hospitali Kubwa za Mikoa lazma kuna Kijisehemu wapo tawi la NHIF (Kwa mkoa huo) wanafanya Verification..
SO inawezekana pia..japo si kila sehemu imefika kwasababu NHIF inawatumishi wachache sana
 
Uko sahihi na ndicho nilichokuandikia hapo Juu kuwa NHIF ndyo wanamakosa na Hivyo vyote huwa haviitajiki kinahitajika Check number Tu ukienda NHIF...

Ila Hospitali wao hawana kosa Maana Walitakiwa wapokee. Taarifa inaitwa "Verification Status" Kutoka NHIF ili wao wajiridhishe hakuna Tatizo lolote ili waendelee na matibabu..
Kwahyo waliokulostisha ni hao NHIF

Verification status ya nini wakati namba ninayo na utambulisho niko na vitambulisho vingine?? And what if ingekua ni emergency na sina uwezo wa kufika NHIF?? Au kama ingekua ni weekend pia nisingeweza kupata msaada kisa tuu card haipo??
 
Njia waliyokuja nayo ndio kama hiyo lengo ni kukwamisha tuu wateja wao,

Dunia ipo mbele sana kama mtu anaweza kwenda ofisi za Tigo/Voda na aka renew line kwa kutaja namba za NIDA na kuweka fingerprint, kwanini kwenye afya za watu wafanye masihara hivi??
Binafsi lawama zangu mimi huenda kwa serikali, nchi hii serikali haitilii maanani huduma tunazopewa wananchi wake,

Nenda town leo hii utakuta wahindi wengi tu wanafanya biashara na ukifika kwa kweli mteja ni mfalme nunua sasa ukishakamilisha malipo mkuu ndo byebye na muda mwingine bidhaa zinakua na hitilafu ila ukirudi hawana msaada na wewe, lakini serikali hakuna jitihada inazozifanya kulinda watu wake.

Na madhali umeweka suala la afya naweka na hii nukuu hapa chini ilikua mjadala juzi tu kama sio jana

Hii katika bitu nasikitika ni kua licha ya serikali ya chama cha kijani kutokubali kutoa walipo, hawataki hata kutetea maslahi ya wananchi wao kwenye huduma zinazofanywa na third parties, yani ukisoma comment watu wengi wanasema hayo malalamiko juu ya hizo kampuni ni mengi ila serikali haizibani hizo kampuni mwisho wake wananchi tunakua watu wa kupigwa tu kila sekta

Kwenye uzi huu
 
Siku hizi ukienda kwenye Hospitali Kubwa za Mikoa lazma kuna Kijisehemu wapo tawi la NHIF (Kwa mkoa huo) wanafanya Verification..
SO inawezekana pia..japo si kila sehemu imefika kwasababu NHIF inawatumishi wachache sana

Kuna watu wanaishi zaidi ya km300 ndipo wakute hospitali za mikoa au ofisi za NHIF??

Hoja yangu kubwa hapa ni kwamba NHIF inajitahidi sana kumkwamisha mwanachama wake kuliko kumsaidia.
 
Kwa kusema kosa ni la NHIF hauoni kwa mikakati hiyo ni dhahiri wana lengo la kumkwamisha mteja wao zaidi ya kumsaidia??

Kama unaweza kutoa hela bank pasipo card za bank?? Kwanini usiweze okoa uhai wa mtu kisa tuu card??

Nilijaribu kuwaza kwa wanaopata ajali kwa bahati mbaya labda card ikapotea au akiwa ameiacha mbali na alipopatia ajali itamlazimu aingie mfukoni au akose huduma kisa tuu card??

Wewe unaona NHIF NA HOSPITALI WALICHOKUBALIANA NI SAWA??
Kama nilivyosema kosa lipo Kwa NHIF, Japo kwa mgonjwa anayekuja Akiwa hoi..
Ndugu zake itawalazimu washughulikie Verification..

NHIF siku hizi imekuwa Disorganised sana ndo maana ulisikia hata Private waligoma kutokuhudumia Wagonjwa wa NHIF kwa sababu ya Bei ndogo ya Dawa wakati dawa sasa hivi zimepanda..

So kwa kumalizia ulikuwa na uwezo wa kwenda kulalamika kwa Branch manager wa NHIF hapo kuhusu huyo mtumishi au Kwenda kwa Supervisor wake
 
Sema mimi hata hospitali nawalaumu🤣

Nishaendaga hospitali moja ya karibu, na balaa umeme ukawa umekata na kwakua ilikua jioni generator lilichelewa kuwashwa hivo ikabidi waandike details kwa mkono ili umeme ukirudi watumie computer huduma tulipata lakini kadi tuliacha mapaka kesho yake nikachelewa kwenda , muda nafika wakawa wameshasaini ili nhif wasigome lipa

NHIF kuna kazi kubwa sana pale
 
Verification status ya nini wakati namba ninayo na utambulisho niko na vitambulisho vingine?? And what if ingekua ni emergency na sina uwezo wa kufika NHIF?? Au kama ingekua ni weekend pia nisingeweza kupata msaada kisa tuu card haipo??
Nataka kukuuliza swali mkuu Umewahi kusafiri Nje?
Vipi unaweza ukawapa Kitambulisho badala ya Pasport au visa wakakukubalia?

Taarifa hizo kwao hakuna japo unaweza ukawapa namba na wakaangalia wakakuona lakini nani wa kuthibitisha kwamba wewe ndiyo mtu sahihi? Ni Ubalozi wako na ndo maana watakupeleka ubalozi wako utapewa Karatasi ya Kuthibitisha kwamba ni kweli hivyo vitu ulikuwa navyo!

Sasa umenielewa.?

Ndo maana hata kuna baadhi ya Sehemh ili upekeke baadhi ya Nyaraka Huwa lazma ziwe zimethibitishwa na watoaji Unafikiri kwanini?

Vipi kama Taarifa hizo amechukua mtu mwingine na kuja nazo kutibiwa?

Wakati mwingine tunalalamikia sheria ila zikitumika ipasavyo pia tunalalamika tena..

Narudia Tena hospitali wao walitaka uthibitisho wa Bima kama wewe ni Mnufaika na Bima hiyo kwa sababu hukuwa na Kitambulisho kinacho kuonyesha wewe ni Mnufaika wa bima hiyo kosa lao ni lipi? Kutaka uthibitisho? Namba Ya uthibitisho pekee haiwezi kuwa Uthibitisho..

Swala lingine umesema ingekuwa ni wikiendi usingepata huduma?
Jamani kuna mambo mengine tunalazimisha vitu ambavyo hata wewe mwenyewe nadhani ungekuwa position yako Sijui kama ungepata jibu..

Kwa kujibu swali hilo naomba Ujaribu kwenda ATM siku za Wikiendi Sana sana Jumapili Bila Kadi halafu katoe Pesa kwenye ATM ukiweza utakuwa umejijibu swali lako
 
Sema mimi hata hospitali nawalaumu🤣

Nishaendaga hospitali moja ya karibu, na balaa umeme ukawa umekata na kwakua ilikua jioni generator lilichelewa kuwashwa hivo ikabidi waandike details kwa mkono ili umeme ukirudi watumie computer huduma tulipata lakini kadi tuliacha mapaka kesho yake nikachelewa kwenda , muda nafika wakawa wameshasaini ili nhif wasigome lipa

NHIF kuna kazi kubwa sana pale
NHIF inakingiwa kifua sana Na Odo sijui kwaninu
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Habari za muda huu wadau.

Mimi ni mwanachama wa NHIF kwa taktibani miaka 10 sasa lakini kuna baadhi ya changamoto nilkua nazipitia nyingine nilikua nazisikia kwa wanachama wengine lakini week iliyopita ndipo lilinikuta jambo.

Week iliyopita nilienda hospitali flani ambayo ni mbali kidogo na ninapoishi (100Km+) kwa lengo la kupata matibabu (Hospitali hiyo ndiyo hua nafanyiwaga matibabu mara kwa mara)

Kutokana na dharura iliyonikuta nilijikuta nimesahau kadi yangu ya bima.

Nilifika hospitali hapo majira ya tano Asububi, Na maongezi yalikua kama hivi.

Mimi: Habari dada, naitwa xxxx nimekuja kwaajili ya matibabu lakini kwa bahati mbaya nimesahau card ya BIMA na ninatokea mbali kidogo, je naweza kupata huduma?

Mhudumu: Hapana.

Mimi: Lakini namba za card ya bima ninayo?

Mhudumu: Hapana, mpaka utakapokua na card.

Mimi: Je nikiomba mtu anisaidie kuipiga picha kisha akanitumia naweza kupata msaada.

Nilikaa kama dakika 2 nikiwa nawaza nini cha kufanya huku nikimuangalia yule dada. Ghafla mhudumu mwingine aliyekua pembeni yake akaanza kuongea.

Mhudumu: Labda uende ofisi za BIMA uwaombe wakupe copy ya kitambulusho/utambulisho wa muda ndipo unaweza kupata huduma.

Mimi: Ahsante, Ofisi za Bima zinapatikana wapi hapa.

Yule mhudumu wa pili akanielekeza nikiwa na matumaini ya kupata huduma kwa siku hiyo kwasababu nilikua na ruhusa ya siku hiyo tuu kazini.

Mnamo saa Sita mchana nilifika ofisi za NHIF nikawaelezea yaliyotokea na lengo la mimi kufika pale.
Lakini nilichojibiwa ni kwamba “HATUNA HUDUMA HIYO”

Nikauliza, je nitapaje huduma kwasababu ninapotoka ni mbali, akanijibu mpaka card ipatikane nikasema kama nika report kama card imepotea je naweza kupata huduma ya dharura?

Nilichojibiwa ni kwamba process za kupata card ni lazima niende kituo cha polisi kupata loss report kisha niende kwa muajiri kisha nifike ofisi za NIDA.

JE, KUNA ULAZIMA GANI WA MWANACHAMA KUWA NA CARD ORIGINAL NDIPO APATIWE HUDUMA?
Ili pesa zibaki huko hazina, wazitumbue, kila mfuko una masharti magumu kwa wansnchi, kikokotoo cha hifadhi ya jamii, 33%unapewa, 67% unapewa kidogodogo kila mwezi! Ukifa tu, iliyobaki ni Mali ya ccm
 
Unatibiwa vizuri kama ni emergency yani hospitali hazikatai emergency yoyote, au ungeenda social welfare
 
Back
Top Bottom