Kwanini Ndoa za siku hizi zinavunjika sana?

Kwanini Ndoa za siku hizi zinavunjika sana?

Siku hizi ukiishi maisha halisi kupata mke au mume ni ngumu watu wanaoa/wanaolewa na wanaoigiza maisha ndoa zinaishia kuwa movie.
 
Inategemeana ndoa na ndoa;
inaweza kuwa kukosa pesa,
inaweza kuwa tamaa ya kuzini yaani uchepukaji,
kushindwa majukumu ya ndoa,
utoto au kutokomaa akili,
vuguvugu la haki za wanawake,
na mengineyo.
 
Nianze kwa kutoa pole kwa JOZEE CHAMELION na JANJAROO, kwa niaba ya wengine, ambao ndoa zao hivi zime-rest in peace.

Nimekuja na hoja fikirishi kuwa ni nini kinaikumba taasisi hii muhimu kwa maisha na uhai wa familia na Taifa? NDOA.

Enzi za mababu na mabibi mafundisho ya ndoa yalipewa kipau mbele sana katika jamii. Utakumbuka tulikuwa na JANDO na UNYAGO. Lengo la mafundisho haya ilikuwa kumuandaa kijana kubeba na kukabiliana na majukumu ya utu uzima. Naweza kusema kuwa kwa wakati wa sasa jambo hili zuri limeachwa kabisa.

Lakini pia watu wanaoana kwa msukumo wa tamaa za mwili (ngono), Utakuta mtu anamuoa mwanamke kwakua tu ana tako, macho mazuri, ni mweupe na kadhalika au anaolewa na mwanaume kwa kua ana pesa au kazi nzuri, vyote hivi vina bashasha tu katika warmth ya ndoa lakini kamwe sio misingi ya ndoa imara na bora.

Aidha ieleweke, Ndoa ni ya watu wawili waliooana. Wanandoa wanaporuhusu kuingiliwa na wasiohusika, kama mawifi, mashemeji, wazazi na wanajamii, wasitarajie mwenendo mzuri wa maisha ya ndoa yao. Na hili ni pamoja na kuwa na ndoa tegemezi, kama kula kwa wazazi na kuishi kwa wazazi.

Kadhalika watu wengi hawajui kuwa sio kila mwanaume au mwanamke ana weza kuwa mwenzi wako. Mwanaume mnyenyekevu hawezi kuishi na mwanamke kichaa, au wa swala tano akaishi na mlevi na kinyume chake. Ndio maana tunaaswa kuwa fanya makosa yoyote maishani lakini sio kukosea kuoa au kuolewa!

Hali kadhalika watu hawajui NDOA ni darasa endelevu. Kila siku ni lazima uifanye ndoa yako kuwa mpya, kuipa ubunifu mpya. Ndio maana katika ndoa, watu hutunukiwa cheti kwanza masomo badae.

Ni vema pia kuelewa ndoa huenda na dhana ya mchezo wa Jig-saw-fit. Kwamba mapengo ya mmoja yanazibwa na mazuri ya mwingine. Ni lazima kusaidiana, kuimarishana na kutiana moyo. Si vema kuviziana na kutafuta mabaya ya mwingine.

Muhimu pia kujua Ndoa ni tendo la ndoa.
Hili linapaswa kufanywa kikamilifu sio kupapasa papasa. Mke au Mume mzuri ni lazima awe malaya sana (fundi mzuri) wa mahaba na tendo awapo faragha na mwenzie.

Mwisho ila si mwisho kwa umuhimu, wana ndoa wanapaswa kuombeana mema kila wakati.

Tukumbuke ni wajibu wa Mume KUMPENDA Mkewe na Mke KUMTII Mumewe.

Karibuni kwa kuelimishana ili tuondoe aibu hii.

Janjaro ndoa chali hata habari
 
Mimi nampenda Sana mke wangu Mary
MUNGU azidi kukubariki
Namin kweli utakuw na aman siku zote za maixha yak MUNGU akupe akil akupe mali akupe na buxara mke wangu.acha Hawa wengine wagombane na ndoa zao wasivunje wenyewe.Mary wengi wanaweza kuwa wanakutaka lakini Mimi na bahati Sana kukupata.nakupenda Sana MUNGU anajua.Nashukuru unathamini mafanikio yangu Mary nakuhaidi ntajitahid Sana kwa uwezo wangu tuko pamoja.we ndo mwanamke mwenye uchungu na Mimi mke wangu kipenz
Naamini Mary kasikia kaka
 
Mkuu Come27 ni kweli bado nakunywa maziwa kwa wazazi, nikifanikiwa kuoa ntaku tag kiongozi.
 
Mimi nateseka sana na hili jambo
Najuta sana kwanini nilimpenda
Wengi wanaumizwa na hili lakini ni ngumu kusema. Kama una ujasiri fafanua kidogo tujaribu kukupa ushauri kulingan na scenario yako. Mwenyezi Mungu atasikia kilio cha wanaume baada ya kuporwa mamlaka kwa kutumia nguvu ya dola.
 
.....tatizooo tunapenda kuanza na papuchi kabla ya kuwekeza kwenye urafiki..." building a friendship is more important than starting with sex than building a friendship for expectant couples" ..........mkichokana mwarejea pasha kiporo moto wakati nyama ni ile ile isipokuwa mabucha ni tufauti
Point sana hii vijana wanatakiwa wawe marafik kwanza ila wanajenga ndoa kwy Msingi wa papuchi, hapo lzma ivunjike tu
 
Point sana hii vijana wanatakiwa wawe marafik kwanza ila wanajenga ndoa kwy Msingi wa papuchi, hapo lzma ivunjike tu
Siku hizi mwanamke kuolewa ni ajira. Wanalilia sana, lakini wakishaingia ndani wanachomoza makucha yao, ni ngumu kuficha tabia ya mtu muda wote. Pia tatizo la kuvumilia kwa wanawake na wanaume. Kwa kawaida ukianza urafiki wa kawaida na mwanamke, atakuchukulia kama kaka yake, na akilijua hilo siku sio nyingi atakutambulisha boyfriend wake. Utaishia kuwashuhudia kwa macho tu
 
Back
Top Bottom