Tangu zamani ndoa ilikusudiwa kuwa ya mume. Zama za haki sawa kwa wanandoa zimekuja na mengi, hivyo kudumu kwa ndoa ni majaaliwa. Mke akijinyenyekeza kwa mume ndoa itasimama, lakini akijifanya kuwa na haki sawa, ujue ama mume ajifanye bwege, ama ndoa ivunjike.
Pia mabinti wengi siku hizi wanaingia kwenye ndoa na mtazamo wa ndoa za kwenye filamu na Facebook. Wanapofika ndani, uhalisia unakuwa tofauti, wanahisi mapenzi hakuna, wanaanza kuchepuka na kuhatarisha ndoa zao. Wanasahau kuwa kitendo cha mwanamume kutoa mahari na kumuoa kati ya wanawake wengi ni zawadi inayozidi zote.
Kingine ni kubadilika kwa structure ya ndoa. Mke alikusudiwa kuwa msaidizi wa mume, aitunze na kuilea familia wakati baba akitafuta. Tangu kuingia kwa mfumo wa wanawake tunaweza ndoa nyingi zimekuwa shakani. Mke na mume hukutana jioni nyumbani, huko mke ashindako hukutana na vishawishi na mafunzo mbalimbali ambayo taratibu huua upendo uliopo kwa mume na kumuona hatoshi ama hafai kabisa, na hapo huamua kutafuta liwazo nje. Huku kujidanganya huthibitika pale talaka itokapo, mwanamke huyu hukosa matunzo kwa hivyo vidume vilivyokuwa vikimdanganya. Kimsingi maisha ya mke mfanyakazi au mfanyabiashara yamerahisisha sana wanawake kuasi ndoa zao kwa kuzidiwa na ushawishi na hivyo kupelekea talaka. Kama kweli unataka kuwa salama kwenye ndoa yako, ni heri ukafuata mfumo wa ndoa za Zanzibar, i love them. Ila kama unataka kuunda kampuni ya ujasiriamali kwa kina la ndoa, basi tafuta mfanyakazi ama mfanyabiashara, alimradi usiwe tu na pressure.
Kifupi ndoa inayodumu inajengwa kumzunguka muoaji, mwanamume, lakini ndoa za wanawake tunaweza mara nyingi hugeuka vita kuu ya tatu ya dunia. Mume atafute kwa ajili ya familia, mke alee na kuitunza familia (akiwemo mume) ndio mpango halisi wa familia. Watoto wawe chini ya uangalizi wa mama, sio house girl au day care.
KUWA MAKINI NA MWANAMKE UNAYETAKA AWE MKEO, VINGINEVYO UTAISHIA KULIA NA KUSAGA MENO.