Kwanini Ndoa za siku hizi zinavunjika sana?

Kwanini Ndoa za siku hizi zinavunjika sana?

BEHOLD

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
5,091
Reaction score
10,773
Nianze kwa kutoa pole kwa JOZEE CHAMELION na JANJAROO, kwa niaba ya wengine, ambao ndoa zao hivi zime-rest in peace.

Nimekuja na hoja fikirishi kuwa ni nini kinaikumba taasisi hii muhimu kwa maisha na uhai wa familia na Taifa? NDOA.

Enzi za mababu na mabibi mafundisho ya ndoa yalipewa kipau mbele sana katika jamii. Utakumbuka tulikuwa na JANDO na UNYAGO. Lengo la mafundisho haya ilikuwa kumuandaa kijana kubeba na kukabiliana na majukumu ya utu uzima. Naweza kusema kuwa kwa wakati wa sasa jambo hili zuri limeachwa kabisa.

Lakini pia watu wanaoana kwa msukumo wa tamaa za mwili (ngono), Utakuta mtu anamuoa mwanamke kwakua tu ana tako, macho mazuri, ni mweupe na kadhalika au anaolewa na mwanaume kwa kua ana pesa au kazi nzuri, vyote hivi vina bashasha tu katika warmth ya ndoa lakini kamwe sio misingi ya ndoa imara na bora.

Aidha ieleweke, Ndoa ni ya watu wawili waliooana. Wanandoa wanaporuhusu kuingiliwa na wasiohusika, kama mawifi, mashemeji, wazazi na wanajamii, wasitarajie mwenendo mzuri wa maisha ya ndoa yao. Na hili ni pamoja na kuwa na ndoa tegemezi, kama kula kwa wazazi na kuishi kwa wazazi.

Kadhalika watu wengi hawajui kuwa sio kila mwanaume au mwanamke ana weza kuwa mwenzi wako. Mwanaume mnyenyekevu hawezi kuishi na mwanamke kichaa, au wa swala tano akaishi na mlevi na kinyume chake. Ndio maana tunaaswa kuwa fanya makosa yoyote maishani lakini sio kukosea kuoa au kuolewa!

Hali kadhalika watu hawajui NDOA ni darasa endelevu. Kila siku ni lazima uifanye ndoa yako kuwa mpya, kuipa ubunifu mpya. Ndio maana katika ndoa, watu hutunukiwa cheti kwanza masomo badae.

Ni vema pia kuelewa ndoa huenda na dhana ya mchezo wa Jig-saw-fit. Kwamba mapengo ya mmoja yanazibwa na mazuri ya mwingine. Ni lazima kusaidiana, kuimarishana na kutiana moyo. Si vema kuviziana na kutafuta mabaya ya mwingine.

Muhimu pia kujua Ndoa ni tendo la ndoa.
Hili linapaswa kufanywa kikamilifu sio kupapasa papasa. Mke au Mume mzuri ni lazima awe malaya sana (fundi mzuri) wa mahaba na tendo awapo faragha na mwenzie.

Mwisho ila si mwisho kwa umuhimu, wana ndoa wanapaswa kuombeana mema kila wakati.

Tukumbuke ni wajibu wa Mume KUMPENDA Mkewe na Mke KUMTII Mumewe.

Karibuni kwa kuelimishana ili tuondoe aibu hii.
 
MKUU CHANZO KIKUBWA KINAWEZA KUWA NI NYAKATI HIZI ZA MWISHO.
WATU WANAANZA MAPENZI KATIKA UMRI MDOGO MNO,WANADATE NA WATU MBALI MBALI KIASI KWAMBA AKIWA KATIKA NDOA ANAFANYA KULINGANISHA WA NYUMA NA WA KWENYE NDOA.LAZIMA NDOA IVUNJIKE
KINGINE NI TAMAA NA HAPA KILA MTU ANAJUA SIDHANI KAMA NINA KIPYA CHA KUCHANGIA HAPA
 
Mimi nampenda Sana mke wangu Mary
MUNGU azidi kukubariki
Namin kweli utakuw na aman siku zote za maixha yak MUNGU akupe akil akupe mali akupe na buxara mke wangu.acha Hawa wengine wagombane na ndoa zao wasivunje wenyewe.Mary wengi wanaweza kuwa wanakutaka lakini Mimi na bahati Sana kukupata.nakupenda Sana MUNGU anajua.Nashukuru unathamini mafanikio yangu Mary nakuhaidi ntajitahid Sana kwa uwezo wangu tuko pamoja.we ndo mwanamke mwenye uchungu na Mimi mke wangu kipenz
 
Tatizo kubwa nikwamba mpaka mdada anakuja kuingia kwenye ndoa anakua kesha cheza mpaka ligi kuu alafu unaye kuja kumuoa unamrudisha ndondo cup hapo lazima ndoa iwe ngum. Nadhani wakubwa wenzangu mmenielewa
 
Maisha magumu,hakuna anayependa kula ugali mkavu kila siku.Mtu anavumilia mwaka 1,2,3 hamna kitu; lazima atafute pa kuzeekea vizuri.
 
Tatizo kubwa nikwamba mpaka mdada anakuja kuingia kwenye ndoa anakua kesha cheza mpaka ligi kuu alafu unaye kuja kumuoa unamrudisha ndondo cup hapo lazima ndoa iwe ngum. Nadhani wakubwa wenzangu mmenielewa
Kwani hakuna namna ya kumjua aliewahi cheza ligi kuu?
 
Saabab kubwa no kuto kumuhofu Mungu kati ya wanandoa hmna SBB nyingine!!
 
Back
Top Bottom