Kwanini Ndoa za Harusi hazidumu?

Kwanini Ndoa za Harusi hazidumu?

jaffari yogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
685
Reaction score
148
Nimewahi kuhudhuria ndoa nyingi za harusi lakini cha kushangaza ni kwamba nyingi hazidumu zinawahi kuvunjika. Hivi ni kwa nini?
 
Hizi ndoa za harusi zinaangaliwa na wengi kwa hiyo unakuta na wachawi wamo wanaona wivu
 
Unatafuta sababu usifanye harusi? Usikariri. Wanaoishi bila ndoa huachana tena labda zaidi kuliko wanaooa ama kufanya harusi. Waliooana wa dini moja wanaachana sawa tu na wasio wa dini moja.

tafuta sababu kwa nini ndoa hazidumu, sherehe ya harusi haiwezi kuwa kigezo.
 
Watu wengi huoana kwa tamaa zao wenyewe(kwa tamaa ya mali-wanawake au uzuri wa umbo-wanaume) na kiuhalisia tabia zao mbaya,ndoa haiwezi kudumu.
 
Acha kupotosha watu. Umeona ngapi ? Ndoa za haki zotezinadumu kama yangu ina miaka ishirini na ushee lkn bado tunapendana kama vile harusi yetu ni mwezi ujao. Usichukulie mifano ya ndoa za wasanii wa bongo wengi wao misifa na wanawake ni mitumba kwisha kazi wameshajichokea kwa kubadilisha wapenzi
 
Ni kweli kabisa ndoa zinofanywa kwa harusi kwenye kumbi /mjumbani huwa nyingi hazidumu. Mimi nilifunga ndoa bila harusi na tumeishakaa mda mrefu, mdogo wake mke wangu yeye ndoa yake ni utata mtupu.
 
Mie nadhani kuna wanaozilaani maana penye wengi huwa kuna mengi na wenye vijicho wapo.
 
Kumbe!!!
solution ni kuchukuana kimya kimya tu sogea tukae....
 
Nafahamu wengi waliofunga ndoa na kufanya sherehe mpaka leo wako pamoja.
 
Hivi Harusi ni nini?
Wataalam wa kiswahili naomba mnisaidie maana hii kauli ya NDOA ZA HARUSI bado sijaielewa vizuri.
 
Nimewahi kuhudhuria ndoa nyingi za harusi lakini cha kushangaza ni kwamba nyingi hazidumu zinawahi kuvunjika. Hivi ni kwa nini?

Mosi hakuna kitu kinachoitwa ndoa za harusi...

Ndoa ni kitendo cha ukiri au mkataba kati ya mwanaume na mwanamke kuamua kuishi pamoja milele.

Harusi ni mjumuiko wa watu wenye kufanya sherehe baada ya mwanamke na mwanaume kufunga ndoa.

Pili, sina uhakika umetumia kigezo gani kufanya hitimisho ulilofanya kuwa kwa nini nyingi ya ndoa ziambatanazo na sherehe ya harusi huwa hazidumu.

Labda utueleze research yako ina asilimia ngapi ya matukio ya namna hii?
 
^^
Kwa sababu hizi;
1. Wanandoa wa siku hizi hususani miaka ya kuanzia 2000s wanafikiri ukiingia katika ndoa, ndo basi tena kila kitu kimeisha, wanadhani maisha ya ndoa ni rahisi tu
2. Wengi wanadhani wakipata harusi basi wameshinda ndoa. Wanapongezana, wanakula, wanafurahi, majaribu yanapoanza wanatafuta milango ya kutokea
3. Mabinti wengi wanatafuta harusi kupata uhalali, wakidhani ndio usalama. Wakishapata harusi, wakaingia ndani, visa, dharau, kujisikia vinaanza maana cheti cha ndoa kinamlinda wanasahau cheti cha talaka hakipo mbali
4. Harusi nyingi zinaambatana na mengi. Matatizo machache kati yake ni chuki zisizo na maana, kuoneana vijicho, zawadi zenye mapatano ya kishirikina, kutofungwa kwa mawasiliano na X's wa wanandoa wapya!
SI HARUSI ZOTE HULETA MATOKEO YA NDOA ZA AINA HII, NI CHACHE TU ^^
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Nyingi ni ngapi?

Tupe takwimu za ndoa za harusi na zisizo za harusi.
 
Back
Top Bottom