Kwanini Ndoa za Harusi hazidumu?

Kwanini Ndoa za Harusi hazidumu?

Ni kweli kabisa ndoa zinofanywa kwa harusi kwenye kumbi /mjumbani huwa nyingi hazidumu. Mimi nilifunga ndoa bila harusi na tumeishakaa mda mrefu, mdogo wake mke wangu yeye ndoa yake ni utata mtupu.

...kafunge ndoa wewe acha imani potofu...
 
Nimewahi kuhudhuria ndoa nyingi za harusi lakini cha kushangaza ni kwamba nyingi hazidumu zinawahi kuvunjika. Hivi ni kwa nini?

...nyingi maanayake nini ? Fanya utafiti leta takwimu usilete shigongoizm jukwaani. Kama observation ndo ya staili hii na mimi nakwambia nyingi nilizoshuhudia na kuhudhuria hakuna hatamoja iliyovunjika,huu ni ukweli wala sitanii ndo maana takwimu za uhakika ni muhimu sana...
 
Nimewahi kuhudhuria ndoa nyingi za harusi lakini cha kushangaza ni kwamba nyingi hazidumu zinawahi kuvunjika. Hivi ni kwa nini?

sio kweli, swali lako nisawa nakusema kwanini albino hawafi, jibu wanakufa ila hawasemi albino kafa, wanasema jafari kafa. mfano tu.
 
...nyingi maanayake nini ? Fanya utafiti leta takwimu usilete shigongoizm jukwaani. Kama observation ndo ya staili hii na mimi nakwambia nyingi nilizoshuhudia na kuhudhuria hakuna hatamoja iliyovunjika,huu ni ukweli wala sitanii ndo maana takwimu za uhakika ni muhimu sana...

yangu ina10yrs, najaribu kuivunja haivunjiki. naunga mkono mchangiaji.
 
^^
Kwa sababu hizi;
1. Wanandoa wa siku hizi hususani miaka ya kuanzia 2000s wanafikiri ukiingia katika ndoa, ndo basi tena kila kitu kimeisha, wanadhani maisha ya ndoa ni rahisi tu
2. Wengi wanadhani wakipata harusi basi wameshinda ndoa. Wanapongezana, wanakula, wanafurahi, majaribu yanapoanza wanatafuta milango ya kutokea
3. Mabinti wengi wanatafuta harusi kupata uhalali, wakidhani ndio usalama. Wakishapata harusi, wakaingia ndani, visa, dharau, kujisikia vinaanza maana cheti cha ndoa kinamlinda wanasahau cheti cha talaka hakipo mbali
4. Harusi nyingi zinaambatana na mengi. Matatizo machache kati yake ni chuki zisizo na maana, kuoneana vijicho, zawadi zenye mapatano ya kishirikina, kutofungwa kwa mawasiliano na X's wa wanandoa wapya!
SI HARUSI ZOTE HULETA MATOKEO YA NDOA ZA AINA HII, NI CHACHE TU ^^

Nakubaliana na wewe katika hayo maelezo uliyotoa.
 
unakwepa gharama za harusi ama???? me sijakupata ujue au umakariri
 
Hivi Harusi ni nini?
Wataalam wa kiswahili naomba mnisaidie maana hii kauli ya NDOA ZA HARUSI bado sijaielewa vizuri.

Ndoa ni pale watu wawili wa jinsia tofauti wanapohalalishwa kiimani au kiserikali kugegedana kwa lengo la kuanzisha familia. Harusi ni sherehe zinazofanyika baada ya ndoa, mnaweza kufunga ndoa bila harusi, yaani mnakwenda Kanisani, Bomani au msikitini, mnafunga ndoa mkiwa na wasimamizi/mashahidi wenu, mkimaliza mnarudi nyumbani kimya-kimya.
 
Unapozungumzia harusi unamaanisha nini haswa? Sherehe? Ni hivi, ndoa ni makubaliano na maagano kati ya mtu mume na mtu mke ya kuishi pamoja na kuendeleza uumbaji wa Mungu, HARUSI ni hali ya mwanaume na mwanamke kuanza maisha ya ndoa rasmi wakiwa pure na hasa mwanamke; harusi ni bikra na ndo maana ya kuvishwa nguo nyeupe siku ya ndoa. Siku hizi harusi ni chache ila ndoa.
 
Ndoa ni pale watu wawili wa jinsia tofauti wanapohalalishwa kiimani au kiserikali kugegedana kwa lengo la kuanzisha familia. Harusi ni sherehe zinazofanyika baada ya ndoa, mnaweza kufunga ndoa bila harusi, yaani mnakwenda Kanisani, Bomani au msikitini, mnafunga ndoa mkiwa na wasimamizi/mashahidi wenu, mkimaliza mnarudi nyumbani kimya-kimya.



Kwahiyo mtu akisema sherehe ya Harusi anakuwa hayupo sawa kwa kiswahili sanifu? Siyo Kwamba Harusi inajumuisha vyote Ndoa na sherehe zake?
 
Kwa hiyo unataka uvute ndani bila harusi? Kafunge ndoa na fanya harusi usikwepe sherehe. Tehe tehe
 
Nimewahi kuhudhuria ndoa nyingi za harusi lakini cha kushangaza ni kwamba nyingi hazidumu zinawahi kuvunjika. Hivi ni kwa nini?
Ni kwa sababu wewe hujafunga na unawatia nuksi waliokwisha funga ndio maana zinavunjika!
 
Back
Top Bottom