The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 19,254
- 42,873
Japan, Ujerumani na Korea Kaskazini.
Ahsante mkuu, ukiongelea hizo nchi za wenzetu walishatuacha kitambo sana.
Mleta uzi amejikita zaidi kwenye hizi nchi masikini nyingi zikiwa bara la Africa.
US mwenyewe sio kwamba hakopi, anakopa ila anaamua akope kwa ajili ya nini na atatumiaje mkopo wake.
Shida hapa sie nchi masikini, unapewa mkopo na kupangiwa namna ya kuutumia huo mkopo.
Mara zote hua nashauri serikali zetu zingetumia muda mwingi kupembua vipaumbele vyao kama nchi kisha waamue wanataka wakope kwa miradi ipi itakayoleta tija.
Uliona wapi tumepigwa kwenye deal la radar na ikaamuliwa kwamba tulipigwa, mnaambiwa mnarudishiwa pesa yenu lakini iende kwenye madawati au kununua vitabu, seriously? Utasema kweli huyo mtu ana nia njema na maendeleo ya nchi yenu?
Kwanini wasiwarudishie tu pesa mkaamua wapi muielekeze kulingana na vipaumbele vyenu?