Kwanini nchi za Magharibi hupenda kukopesha zaidi nchi Maskini kwenye miradi ya huduma za jamiii badala ya Uzalishaji?

Hivi ni kwanini nchi za Magharibi hupenda kukopesha zaidi nchi Maskini kwenye miradi ya huduma za jamiii badala ya Uzalishaji?

Mikopo italipika vipi wakati pesa nyingi wanatukopesha kwa ajili ya huduma za jamiii?

Na kwanini tunapenda kupokea? Kwanini tusiwaambie watukopeshe zisaidie kwenye Uzalishaji zaidi?
Faida inayotokana na uzalishaji inaishia kwa wachache, ndio maana wanasaidia kwenye maeneo ambayo yanawagusa wengi.
 
Hivi ni kwanini nchi za Magharibi hupenda kukopesha zaidi nchi Maskini kwenye miradi ya huduma za jamiii badala ya Uzalishaji?

Mikopo italipika vipi wakati pesa nyingi wanatukopesha kwa ajili ya huduma za jamiii?

Na kwanini tunapenda kupokea? Kwanini tusiwaambie watukopeshe zisaidie kwenye Uzalishaji zaidi?
Sina shida hata kidogo kukupa hadhi ya GT kwa mada za namna hii siku hizi mkuu YEHODA.

Na mimi nitachangia kwenye mada yako hii nzuri kwa kusema kwamba haijalishi wanakopesha upande gani. La msingi na muhimu zaidi ni hao wanaopokea msaada/mkopo huo jinsi wanavyoutumia kwa manufaa.

Chukulia mfano wa ELIMU.
Tanganyika wakati inapata uhuru, hata makatibu mhtasi maofisini hawakuwepo. Kulikuwa na ma-engineer wangapi, manesi wangapi, n.k., n.k.

Na la msingi zaidi, hawa watu waliopata elimu kwa mkopo, hawa watu wametumika ipasavyo kweli ili mkopo huo uonekane ulikuwa na manufaa kwetu?
Hawa watu wameweza kupata akili za kuendesha shughuli za kuiletea maendeleo nchi (unakokuita wewe kuzalisha).

Tusiwalaumu wanaotoa misaada/mikopo, tujilaumu wenyewe tunaopata mikopo/misaada kwa kushindwa kwetu kuitumia vizuri ili "IZALISHE."
 
Lengo la hao wakopeshaji halijawahi kulenga kutukomboa kiuchumi.

Kama kuna mtu ana maoni tofauti atuambie ni nchi gani hawa jamaa waliikopesha na kuisaidia sasa hivi imesimama kama yenyewe haihitaji misaada wala mikopo tena, ataje moja tu.
Na kwa nini utarajie "ukombolewe kiuchumi" na watu wengine? Inaingia akilini hiyo?
 
Hivi ni kwanini nchi za Magharibi hupenda kukopesha zaidi nchi Maskini kwenye miradi ya huduma za jamiii badala ya Uzalishaji?

Mikopo italipika vipi wakati pesa nyingi wanatukopesha kwa ajili ya huduma za jamiii?

Na kwanini tunapenda kupokea? Kwanini tusiwaambie watukopeshe zisaidie kwenye Uzalishaji zaidi?
Huduma za jamii zikiimalika ndio utazalisha..unaanza na quality ya human resources ndio huo uzalishaji itapatikana kinyume na hapo hata wawekezaji hupati.
 
Na kwa nini utarajie "ukombolewe kiuchumi" na watu wengine? Inaingia akilini hiyo?

Suala la kuingia au kutoingia akilini tuliweke pembeni kwa sasa, na hiyo ni kwa sababu kama nchi, tunapewa hiyo mikopo na mingine wameitungia majina inaitwa mikopo yenye masharti nafuu.

Kwa kua wanaoichukua kisingizio ni maendeleo, hapo ndio nikasema hao wanaotupatia hizo pesa za maendeleo, umasikini wetu ndio mtaji wao.
 
Ya aina ipi maana tunanufaika na mikopo ya kilimo kupitia mpango wa kilimo bora ya world bank...
Eeee, Eti!

Kwa hiyo? Tuilaumu 'Word Bank', kama hatupati mafanikio?

Mkuu, hili ni swala nyeti kweli kweli. Labda ungeeleza kidogo au utoe mfano (specific) wa mkopo uliokwishatolewa kwa upande huo, na tujadili nini kilitokea.
 
Yani hujui kuwa Tanzania ni moja wa mnufaika wa mikopo ya kilimo bora na world bank... Mbona umeandika kama una data Sana kuhusu maswala ya kilimo
 
Yote hayo watu weupe watupu Hakuna nchi ya kiafrika hata moja na hawajawahi kopa kwa ajili ya huduma za jamii
Ungesema unataka mataifa ya Africa, tungekuwekea.

Mauritius, Botswana na Namibia, ni mifano mizuri.
 
Tuelimishe Taratibu zote hizo mikopo? Kama Mikopo basi Magufuli alifanya mageuzi makubwa kuwa tukope miradi ya uzalishaji lakini ujenzi wa madarasa na elimu bure na hospitali tutumie pesa za ndani sio Mikopo

Kukopa kwa akiki ya kugharimia pure huruma za Jamii Ni nchi kujitia umaskini
Umezaliwa lini?

Viwanda karibia vyote wakati wa uongozi wa Mwalimu, vilijengwa kwa mikopo:

1) viwanda vya nyuzi na nguo
2) Kiwanda vya bia na sigara
3) Matairi
4) Kiwanda cha kuunganisha malori ya scania na matrekta aina ya valmet
5) Na vingine vingi - vyote vilishindwa kujiendesha kwa sababu mbalimbali, kubwa kuliko zote, ukosefu wa weledi.
 
Lengo la hao wakopeshaji halijawahi kulenga kutukomboa kiuchumi.

Kama kuna mtu ana maoni tofauti atuambie ni nchi gani hawa jamaa waliikopesha na kuisaidia sasa hivi imesimama kama yenyewe haihitaji misaada wala mikopo tena, ataje moja tu.
Asante sana.
 
Suala la kuingia au kutoingia akilini tuliweke pembeni kwa sasa, na hiyo ni kwa sababu kama nchi, tunapewa hiyo mikopo na mingine wameitungia majina inaitwa mikopo yenye masharti nafuu.

Kwa kua wanaoichukua kisingizio ni maendeleo, hapo ndio nikasema hao wanaotupatia hizo pesa za maendeleo, umasikini wetu ndio mtaji wao.
Hulazimishwi kuchukua mkopo, wala huambiwi lazima uchukie mkopo wa kitu fulani.

Haya mashirika ya fedha yana sera zao, yanazikopesha serikali kwenye maeneo ambayo serikali inahusika, na wanakopesha sekta binafsi maeneo yao. Huko nyuma walizikopesha sana nchi za Afrika kwaajili ya miradi ya kibiashara, yote ilikufa.

Hata African Bank, benki yetu haiwezi kuikopesha serikali ikajenge kiwanda cha juice, lakini inaweza kumkopesha Bakhresa kwaajili ya kiwanda cha juice. Itaikopesha serikali kwaajili ya ujenzi wa barabara.
 
Hivi ni kwanini nchi za Magharibi hupenda kukopesha zaidi nchi Maskini kwenye miradi ya huduma za jamiii badala ya Uzalishaji?

Mikopo italipika vipi wakati pesa nyingi wanatukopesha kwa ajili ya huduma za jamiii?

Na kwanini tunapenda kupokea? Kwanini tusiwaambie watukopeshe zisaidie kwenye Uzalishaji zaidi?
Kwani mnalazimishwa kukopa ?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hulazimishwi kuchukua mkopo, wala huambiwi lazima uchukie mkopo wa kitu fulani.

Haya mashirika ya fedha yana sera zao, yanazikopesha serikali kwenye maeneo ambayo serikali inahusika, na wanakopesha sekta binafsi maeneo yao. Huko nyuma walizikopesha sana nchi za Afrika kwaajili ya miradi ya kibiashara, yote ilikufa.

Hata African Bank, benki yetu haiwezi kuikopesha serikali ikajenge kiwanda cha juice, lakini inaweza kumkopesha Bakhresa kwaajili ya kiwanda cha juice. Itaikopesha serikali kwaajili ya ujenzi wa barabara.

Kinacholalamikiwa hapa ndio hizo sera za hayo mashirika.
 
Huduma zenyewe za kijamii unazozingumzia ni huduma za maana basi? Utasikia ni mkopo wa kuboresha elimu, sasa nenda huko ukajionee elimu yenyewe "bora" baada ya mwisho wa mradi uliotekelezwa kwa hela ya mkopo. Kama usipolia utakuwa na roho ngumu sana. Ni upuuzi upuuzi, utoto utoto tu yaani.

Maendeleo ya kweli ya nchi hayatatokana na msaada au mkopo popote pale. Yaani tushindwe kama nchi kuendelea kwa kutumia talanta na raslimali watu na maliasili alizozigawa Mungu kwa ajili ya Tanzania kwa ufanisi na kwa maendeleo, tusubiri mikopo kutoka world bank na IMF ndiyo tuendelee? Umaskini wa mtu na nchi huanzia kwenye akili za watu, basi.
Daaaah!!! Umeandika ukweli kabisa, bado hatujafanikiwa kuwekeza kwenye akili za watu, Kama akili zikikaa sawa basi tunaweza piga hatua haraka sana.
 
Suala la kuingia au kutoingia akilini tuliweke pembeni kwa sasa, na hiyo ni kwa sababu kama nchi, tunapewa hiyo mikopo na mingine wameitungia majina inaitwa mikopo yenye masharti nafuu.

Kwa kua wanaoichukua kisingizio ni maendeleo, hapo ndio nikasema hao wanaotupatia hizo pesa za maendeleo, umasikini wetu ndio mtaji wao.
Naona tutazungushana bure.
 
Umezaliwa lini?

Viwanda karibia vyote wakati wa uongozi wa Mwalimu, vilijengwa kwa mikopo:

1) viwanda vya nyuzi na nguo
2) Kiwanda vya bia na sigara
3) Matairi
4) Kiwanda cha kuunganisha malori ya scania na matrekta aina ya valmet
5) Na vingine vingi - vyote vilishindwa kujiendesha kwa sababu mbalimbali, kubwa kuliko zote, ukosefu wa weledi.
Hapa ndipo ninapokuaminia mkuu Hamatan.
 
Back
Top Bottom