Kwanini nchi za Magharibi hupenda kukopesha zaidi nchi Maskini kwenye miradi ya huduma za jamiii badala ya Uzalishaji?

Masikini ni masikini tu hata kuongeza akili hawezi. Sasa kama wamekukopesha za huduma badili zile mnazozalisha wenyewe kupeleka kwenye maendeleo. Umeenda kumkopa mtu pesa ya maendeleo nyumbani kwako akakulazimisha kuwa atakukopesha kwa ajili ya chakula na mambo mengine yasiyo ya kimaendeleo basi wewe pokea alafu ile ya kwako uliyokuwa nayo kwa ajili ya chakula ipeleke kwenye maendeleo
 
Hivi ni kwanini nchi za Magharibi hupenda kukopesha zaidi nchi Maskini kwenye miradi ya huduma za jamiii badala ya Uzalishaji?

Mikopo italipika vipi wakati pesa nyingi wanatukopesha kwa ajili ya huduma za jamiii?

Na kwanini tunapenda kupokea? Kwanini tusiwaambie watukopeshe zisaidie kwenye Uzalishaji zaidi?
Tafuta kitabu fulani kinaitwa "economic hitman" utayajua kwa undani.
 
Watu waliofilisika akili wana malalamiko mengi yasiyo ya msingi kama huyu mleta uzi.
Wanabaki na kazi moja tu ya kutupa lawama kila pande kwa kila watu.
Masikini ni masikini tu hata kuongeza akili hawezi. Sasa kama wamekukopesha za huduma badili zile mnazozalisha wenyewe kupeleka kwenye maendeleo. Umeenda kumkopa mtu pesa ya maendeleo nyumbani kwako akakulazimisha kuwa atakukopesha kwa ajili ya chakula na mambo mengine yasiyo ya kimaendeleo basi wewe pokea alafu ile ya kwako uliyokuwa nayo kwa ajili ya chakula ipeleke kwenye maendeleo
 
Umezaliwa lini?

Viwanda karibia vyote wakati wa uongozi wa Mwalimu, vilijengwa kwa mikopo:

1) viwanda vya nyuzi na nguo
2) Kiwanda vya bia na sigara
3) Matairi
4) Kiwanda cha kuunganisha malori ya scania na matrekta aina ya valmet
5) Na vingine vingi - vyote vilishindwa kujiendesha kwa sababu mbalimbali, kubwa kuliko zote, ukosefu wa weledi.

Wakati huo hao waliotoa mikopo ya ujenzi wa hivyo viwanda, hawakua na manufaa au daida zilizotokana na hivyo viwanda ukiachilia mbali rejesho la pesa za mkopo wao?

Ahsante kwa kuweka kumbu kumbu sawa mkuu.
 
Maana yake ni kwamba nimekudharau tokana na historia yako. Au unataka nikukumbushe?
Ilimradi hauvunji taratibu na sheria za JF, unawezakufanya chochote mkuu.

Uzuri ni kwamba dharau zako za hapa JF hazina madhara yeyote kwangu.
 
Yani hujui kuwa Tanzania ni moja wa mnufaika wa mikopo ya kilimo bora na world bank... Mbona umeandika kama una data Sana kuhusu maswala ya kilimo
Mimi sikuzungumzia maswala ya WB katika bandiko langu, ni wewe uliyeibua hilo. Sasa weka hayo unayoyajua ya mkopo wa WB katika kilimo bora ili tuyajadili.
 
Hivi ni kwanini nchi za Magharibi hupenda kukopesha zaidi nchi Maskini kwenye miradi ya huduma za jamiii badala ya Uzalishaji?

Mikopo italipika vipi wakati pesa nyingi wanatukopesha kwa ajili ya huduma za jamiii?

Na kwanini tunapenda kupokea? Kwanini tusiwaambie watukopeshe zisaidie kwenye Uzalishaji zaidi?
1) Kwanza sijui kama ni kweli unachodai. Hujaonyesha namba yoyote.
2) Pili kama ni kuhusu maazimio ya kibiashara, ukitaka kukopa onyesha kwamba una mpango safi. Hakuna mwenye akili timamu atakayechangia kwa mradi wa kununua ndege kwa kampuni iliyofilisika tayari. Unahitaji mifano mingine?
3) Najua (sina namba tayari) kwamba wafadhili wengi wanatoa mikopo nafuu au misaada moja kwa moja kwa ajili ya miundombinu.
4) Kuwekeza katika elimu ni busara ukitaka kumaliza uhusiano wa misaada. Mfano nchi hii inahitaji idadi kubwa ya wajenzi wanaoweza kuona na kujali kama ukuta unasimama wima au unanyooka, mafundi gari ambao wanasafisha injini kabla ya kubadilisha spea, fundi chuma anayeweza kufuata vipimo hadi asilimia ya milimita, wauuguzi walioelewa maana ya usafi na kwamba kazi ya barakoa si kutunza shingo . . . . kwa jumla watu waliojifunza kutunza wakati kwa sekunde na kadhalika. Maana kama huna watu hao, hutaendesha wala mitambo wala mashine wala kampuni zaidi ya miaka michache hadi mambo yanaporomoka tena....
 
Pamoja na hayo yote yanayofanywa na lichama lako ila bado unasimama kidete na kulitetea
 
Ni suala la kupanga tu kama wao wanatukopesha kwenye miradi ya kijamii basi zakwetu tuzielekeze kwenye uzalishaji.
 
Back
Top Bottom