Kwanini nayapinga makafara?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,417
Reaction score
829,763
Tumeshajadili kwa mapana sana habari za makafara athari zake na ubaya wake na kwamba ukishaanza hii habari huwezi kuacha utaanza na kafara dogo mpaka kubwa kabisa na mwishowe kila kitu huwa hadharani. Mwisho wa ubaya ni aibu kubwa

Unapotafuta mafanikio kwa maana ya mali nyingi fanya kazi kwa bidii ujuzi na maarifa huku ukiomba kudra za mwenyezi Mungu, usitafute njia za mkato za kuumiza na kuteketeza roho zisizo na hatia kwa manufaa binafsi huu ni uchoyo na kujiona bora kuliko wengine....kama unataka njia ya mkato ya mafanikio isiyo na maneno kubali kutoa damu yako au kiungo chako...kuna wengi wanaishi na madonda makubwa mwilini na wanapeta

Kafara la utajiri ni baya...licha ya laana ya kuteketeza roho zisizo na hatia lakini kila kafara lina kikomo cha matumizi (expire date)
Iko hivi kila kiumbe kina umri wake wa kuishi hapa duniani, na muda ukifika kiumbe hivyo hufa, kwahiyo unapotumia kiumbe chochote kwa kafara unakikatisha maisha yake kabla ya muda wake....kwahiyo kibinadamu kitakufa lakini katika ulimwengu wa roho kitakuwa hai mpaka muda wake ufike ndio kife rasmi.

Hapa ndio huona kila baada ya miaka kadhaa watu hutoa kafara ili kuboost zile nguvu...ubaya wa hili ni kwamba jinsi utajiri unavyoongezeka ndivyo pia aina ya kafara hubadilika yaani kuku, mbuzi, ng'ombe na hatimaye binadamu.

Makafara yanatesa makafara ni mabaya ndio maana ni kawaida kuwaona baadhi ya watu kila wiki au kila mwaka kutoa makafara ya kuchinja wanyama ili kuuhami utajiri wao.

Kafara ni maagano ya kuzimu kama unafikiri kuzimu kunashiba damu umeula wa chuya...kama hujawahi kufanya tafadhali usifanye...kama mambo yanaenda Kombo usiogope wala kukata tamaa siku hazigandi na Mungu yupo utasimama tena.

Usiingie kwenye vifungo na mateso ya milele yenye laana ya damu uliyomwaga iso hatia
 
Hakika elimu haina mwisho! Binadamu tunajua kidogo sana kuliko tusivyovijua!

Vingi tunaambiwa ni vibaya au ni vizuri bila kuambiwa kinagaubaga kwanini ni vibaya au kwanini ni vizuri na hata ikitokea tunaambiwa huambiwa nusunusu
 
Kafara ni nini?
Agano ni nini?
Mkataba ni nini?
Kafara ni sadaka ya damu kwa mizimu/ mashetani au Roho chafu zilizo kinyume na Mungu.
 
Kafara ni nini?
Agano ni nini?
Mkataba ni nini?

Kafara ni sadaka ya damu kwa mizimu/ mashetani au Roho chafu zilizo kinyume na Mungu.

Agano ni makubaliano yanayoingiwa Kati ya mtoa kafara na mtolewa kafara, ili mtoa kafara aweze kufaidika kwa mambo kadha wa kadha iwe utajiri, mafanikio nk.

Mkataba ni hati fungani inayobeba masharti na adhabu atakazopata mtoa kafara iwapo ataenda kinyume na agano.
Adhabu za kuvunja maagano huathiri mvunja Agano na vizazi vyake vyote.
Mateso Mengi ya watu wa Leo yamwtokana na adhabu ya kuvunjwa kwa maagano Kati ya mababu na mizimu yao.
 
Kafara ni nini?
Agano ni nini?
Mkataba ni nini?
Kafara ni sadaka ya damu kwa mizimu/ mashetani au Roho chafu zilizo kinyume na Mungu.

Kafara ni kutoa uhai wa kiumbe hai kwa nia ya kufanya agano ili ufanikiwe mambo yako yaliyokwama
Mkataba hauna tofauti na agano, ni aina ya lugha tuu
Kuna baadhi ya makafara pia hufanana na matambiko tofauti ni kwamba tambiko ni kurekebisha mambo yaliyoharibika na kunia mema wakati kafara ni kumtafuta kufanikiwa kwa njia mbaya na za mkato
 
Elimu nzuri sana hii,tuamini Mungu tu kila kitu kinawezekana kwake.
 
kafara na mafanikio zina mahusiano gani?
 
Yale yaliyofunuliwa kwa wanadamu tunayafanyia kazi, yale tuliyofumbwa tunayaacha kama yalivyo. Vinginevyo ukitakakufahamu kila kitu utapasuka kichwa tu. Ingawa hujaeleweka nini lengo lako la kuleta crip hii. Au je unafanya utafiti juu ya suara hilo?
 
Kwani bila hzo kafara huwezi kufanikiwa?ipi njia sahih yakumiliki utajiri bila hzo kafara?je matajiri wote wanatoa hzo kafara?msaada pls?
 
Mbuzi anayechinjwa lazima atimize Miezi 6, Kondoo mwaka 1, Ng?ombe miaka 3, Ngamia miaka 5

Mkusanyaji S. Hussein

NENO UDHIYYAH la Kiarabu linatokana na mzizi wa herufi tatu daad-haa-alif, ambazo huwakilishwa kama d*h.*aa yenye maana ya katikati ya Asubuhi.

Maana ya kilugha ya al-udhiyyah ni mnyama anayechinjwa siku ya Id-ul-Adha. Kisheria, udhiyyah maana yake ni mhanga unaofanywa kwa nia ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu katika siku mahususi na kwa kutimiza masharti fulani.

Mnyama yoyote achinjwaye siku nyingine kwa ajili ya Mwenyezi Mungu si udhiyyah. Hata mnyama anayechinjwa siku ya Idd Kubwa lakini bila kuelekeza nia kwa Mwenyezi Mungu kama vile mnyama anayechinjwa kwa ajili ya kuuzwa buchani, huyo si udhiyya.

Kuchinjwa huko kwa udhiyya katika masiku ya kuchinja (ayyam al-nahr, tarehe 10, 11, 12 na 13 ya Dhul-Hijja) ni jambo lililoamrishwa katika Uislamu kuwa ni sehemu ya ibada ya Hijja.

Qur?an, Sunna na Ijmaa vyote vinathibitisha jambo hilo. Kwa upande wa Qur?an, Mwenyezi Mungu, katika sura ya 108-Al-Kawthar, aya ya pili, anasema, ?Basi swali kwa ajili ya Mola wako, na uchinje (kwa ajili ya Mola wako)?.

Hiyo ni amri iliyotolewa kwa Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ambayo inasimama kama amri kwa waumini wote. Kwa upande wa Sunna ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, ilikuwa ni mila yake na mila ya Maswahaba wake na wafuasi wao waandamizi kuchinja mnyama (mara nyingi kondoo) katika Siku ya Idd Al-Adha.

Zipo riwaya nyingi mno za Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, zinazothibitisha kuwa Mtume na Maswahaba wake walichinja Siku ya Idd na kuwaamrisha wengine kufanya hivyo.

Hekima ya Al-Udhiyyah haiwezi kufahamika kwa wanadamu kwa ukamilifu. Hata hivyo, sehemu fulani ya hekima hiyo yaweza kufahamika. Mosi, ni ishara ya shukurani kwa Mwenyezi Mungu kwa kuumba.

Pili, ni uhuishaji wa mila ya Ibrahim (as), Baba wa Manabii. Hivyo, Muumini anapochinja, anakumbushwa namna Ibrahiim (as) na Ismail (as) walivyotii kwa subira kubwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Utii wa Ibrahim kukubali kumchinja mwanawe kipenzi, na utii wa Ismail kukubali kuchinjwa ni masomo kwa Waumini kwamba wawe tayari kuvitoa vipenzi vyao na kuyatoa muhanga maisha yao kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Tatu, Al-Udhiyyah ni tendo linalopingana waziwazi na wale wanaosema kuwa ni haramu kwa wanadamu kuchinja wanyama na kula nyama kwani kitendo cha kuwachinja kinawaumiza wanyama na kinahujumu utukufu wa maisha yao.

Nne, Al-Udhiyya inabainisha kuwa njia ya huruma zaidi ya kumuua mnyama ni kumchinja. Na tano, Al-Udhiyya inazidisha shukurani ya Muumini kwa Mwenyezi Mungu kikiwa ni kiashiria cha namna Mwenyezi Mungu alivyoutiisha ulimwengu kwa wanadamu na kuuhalalisha uhai wa wanyama kwao ili wapate manufaa mbalimbali.

Kwa undani wake, udhiyyah ni ibada iliyokokotezwa katika Sunna ya Mtume, swallallahu alayhi wa sallam. Ni Sunna Mu?akkadah, hivyo ndivyo idadi kubwa ya Maulamaa wanavyosema.

Masharti yake ni pamoja na mtu anayechinja lazima awe Muislamu, awe mkaazi, na asiwe msafiri, awe mtu mwenye uwezo kifedha, awe mtu mzima na mwenye akili timamu.

Masharti ya kuswihi kwa Udhiyyah ni pamoja na mnyama anayechinjwa awe yule anayefugwa; ng?ombe, kondoo, mbuzi, nyati maji na kadhalika, mnyama anayechinjwa lazima awe ametimiza miezi 6 ikiwa ni mbuzi, mwaka mmoja ikiwa ni kondoo, miaka 3 ikiwa ni ng?ombe, na miaka 5 ikiwa ni ngamia, mnyama asiwe na hitilafu hasa zile zinazoweza kuathiri nyama yake.

Muda wa kuchinja huanzia Alfajiri, hata hivyo, uchinjaji uanze baada ya Swala ya Idd. Sunna ya kuchinja ni kuiacha damu ya mnyama imwagike. Ugawaji wa nyama ni kwamba; theluthi moja ni sadaka ya masikini, theluthi moja ni zawadi kwa majirani, ndugu na jamaa, na theluthi moja kwa ajili ya nyumbani kwa mtu mwenyewe.

Mgawanyo uwe sawasawa lakini kama mahitaji ya nyumbani ya mchinjaji mwenyewe ni makubwa, basi mchinjaji achukue sehemu kubwa. Au kama ana ndugu fukara wa nasaba, basi sehemu kubwa wawape ndugu. Kama yeye mwenyewe si muhitaji wa nyama hiyo, basi sehemu kubwa atoe Swadaka.
 
Kwani bila hzo kafara huwezi kufanikiwa?ipi njia sahih yakumiliki utajiri bila hzo kafara?je matajiri wote wanatoa hzo kafara?msaada pls?

Soma kwa lakini nilichoandika soma rudia kwa makini kila mstari na hitimisho nililotoa
 
Mungu Alitengua kumchinja mtoto wa ibrahim,lkn kwa waislam waliambiwa wachinje kondoo, mbuzi ili mradi uchinje kila ifikapo mwezi baada ya hijja.


Baada ya Yesu Kristo maagano na makafara yote yalikoma...kwa wale wakristo wanajua namaanisha nini
 
Yale yaliyofunuliwa kwa wanadamu tunayafanyia kazi, yale tuliyofumbwa tunayaacha kama yalivyo. Vinginevyo ukitakakufahamu kila kitu utapasuka kichwa tu. Ingawa hujaeleweka nini lengo lako la kuleta crip hii. Au je unafanya utafiti juu ya suara hilo?
Lupaya kwanza rekebisha hii kitu crip na suara, hii ni mada au topic na si crip/ clip halafu ni suala/swala na si suara
Soma mwanzo wa mada mpaka mwisho utajua nini lengo ila kama umeshindwa tangu mwanzo sijui kama utaweza ukirudia
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…